Epuka na saidia kuepuka vitendo vya uonevu (bullying) na kikatili dhidi ya watoto

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
4,513
3,554
Habari za wakati huu wapendwa wa JamiiForums. Bila shaka mko vizuri. Ambao mko Wadhaifu Mungu awape heri.

Iko hivi, Napenda kuzungumzia kuhusu Uonevu (Bullying)

Uonevu ni hali ya kufanya kitu fulani kwa mwingine kama vile kumdhalilisha, kumpiga au kumdhuru kwa namna yoyote ile hata bila sababu ya msingi. Ilimradi umkere mtu huyo mtu wewe ndio roho yako inafurahia hasa pale atakapoonyesha matokeo hasi, kama kughafilika au kuonyesha kuumizwa na kile umemfanyia.

Wengi wa watu wamepitia hasa wakiwa watoto maeneo ya mashuleni ambapo hufanya na baadhi ya watoto, kwa sababu wakifanya hivyo ndio wanasikia raha.

Hii sasa hupelekea mhanga kujihisi vibaya na kujiona hana thamani. Na kuweza kuchukua maamuzi magumu kama vile kujidhuru mwenyewe au kuwadhuru wengine pia kama ni shule mtoto anakuwa haipendi tena. Pia hali hii humfanya mhanga kuathirika kisaikolojia na afya ya akili asipopata usaidizi mapema.

Bullying inaweza fanya kwa yeyote. Lakini huweza kuwa na madhara makubwa kwa mtoto mpaka pale anapokuwa mkubwa.

My concern ni kwa watoto walio chini ya miaka kumi na nane. Kwa sababu ili mtoto akue vizuri anahitaji mazingira mazuri ya ukuaji yenye fursa sawa yasokuwa na vikwazo kama hio uonevu.

Sasa basi, ni jukumu la wazazi na jamii kwa ujumla inayowazunguka watoto kuhakikisha inalinda watoto dhidi ya uonevu au ukatili wa aina yoyote kwa watoto.

Haijalishi unafanywa na nani. Kama umeona ni jambo baya linafanyika kwa mtoto ni vema kuchukua hatua sahihi kuweza kuzuia hilo. Ikiwamo kuripoti polisi au sehemu ambayo itakuwa na usaidizi.

KUMBUKA
Kila mtu ana maoni yake mwenyewe juu ya mambo tofauti.
Unyanyasaji unapotokea unaweza kusababisha maamuzi magumu kwa yule aliyeonewa, kama kujidhuru mwenyewe.

Tunatofautiana juu ya jinsi tunaweza kushughulikia vitu. Wacha tuwe na kikomo. Saidia kujenga jamii inayozingatia ubinadamu.

Funguka Vunja ukimya kwa juu ya uonevu na ukatili kwa watoto.
Saidia kujenga jamii imara inayojiamini.

Taifa bora litajengwa kwa jamii ambayo imekuzwa katika mazingira bora ya malezi na kujiamini.

Acha uonevu na ukatili na uhimize wengine kufanya hivyo.
 
Umeongea jambo jema sana,
Mie pia ni muhanga wa hizo bullying,
Nikiwa darasa la kwanza hadi la pili, ilinifanya hadi nichukie shule, nilipofika darasa la sita nikafanyiwa bullying tena, nilimpiga yule mtoto na mbao almanusura niue walai,
Ikawa mwanzo na mwisho wa wale mabazazi kutuonea kisa tu walikua wakubwa kwetu,

Wazazi wawe karibu sana na watoto, mtoto akilalamika kuonewa basi mzazi usifumbie macho ufatilie, au mzazi ukiona mtoto hapendi shule ni vema kufatilia shida nini usianze kumuadhibu mtoto bila kujiridhisha.
 
Umeongea jambo jema sana,
Mie pia ni muhanga wa hizo bullying,
Nikiwa darasa la kwanza hadi la pili, ilinifanya hadi nichukie shule, nilipofika darasa la sita nikafanyiwa bullying tena, nilimpiga yule mtoto na mbao almanusura niue walai,
Ikawa mwanzo na mwisho wa wale mabazazi kutuonea kisa tu walikua wakubwa kwetu,

Wazazi wawe karibu sana na watoto, mtoto akilalamika kuonewa basi mzazi usifumbie macho ufatilie, au mzazi ukiona mtoto hapendi shule ni vema kufatilia shida nini usianze kumuadhibu mtoto bila kujiridhisha.
Nimependa hio.
Hio ni moja ya njia kukomesha bullying,. Ku act zaidi yao.
 
Back
Top Bottom