Epuka maisha ya kuigiza

Epuka maisha ya kuigiza

Jayspeed

Senior Member
Joined
Feb 23, 2014
Posts
156
Reaction score
169
KIJANA EPUKA MAISHA YA KUIGIZA

Maisha ya kuigiza kwa vijana wengi wa kitanzania kwasasa ni kawaida sana na wengi ndicho kinachowapotezea dira ya maisha..
Kuna mtu anawaza atakula nini sababu hakuna hela lakini akiona nguo mpya kavaa msanii mkubwa mfano diamond platnumz yupo tayari asile lakini avae nguo zile...Maisha haya ni ya kuigiza bila sababu..

Ukifikiria kipindi diamond platnumz hajafanikiwa kuwa msanii mkubwa alikua havai nguo za gharama alikua anakusanya hela kwa ajili ya kurekodi nyimbo zake na alifanikiwa na sasa anaweza kuvaa nguo za gharama anavyotaka..

Kila mtu anayatamani maisha mazuri na matamu lakini lakini ni lazima upambane ili upate unavotamani
Vijana wengi wanapoteza muda na pesa nyingi sana kwenye maisha ya kuigiza avae aonekane kama nani aongee kama nan wengine hufika mbali na kuacha vipaji au vipawa walivyojaliwa na Mungu na kufanya vingine ili waonekane kama mtu fulani ukweli ni kwamba utafeli kijana mwenzangu maisha hayaigizwi bali yanafanywa kweli....

Muda na akili vijana wanayotumia kupata hela na kununua suruali tishet na kofia kama ya Diamond au simu kama ya juma jux akili hizo na muda huo wangewekeza katika kutafuta pesa kwa ajili ya maisha ya baadae huenda wangeishi maisha makubwa kuliko hao.

Aliwahi kusema mtu mmoja maarufu kwasasa ni matehemu STEVE JOBS mmiliki wa kampuni ya Apple alisema hivi "Your time is limited, so dont waste it living someone else's life." ( Muda wako ni mdogo/hautoshi hivyo usiupoteze kwa kuishi maisha ya mtu mwingine).

Usiishi maisha ya kuigiza kijana mwenzangu muda unaouona mwingi ni mchache sana ishi maisha yako kwa sasa ili baadae watokee watakao kuigiza wewe

Sio vibaya kufata njia za mafanikio aliyopata mtu ila ni vibaya kuishi kwa kumuiga yeye

By Jay Speed
 
kwahiyo unamaanisha nikiona nguo nzuri nimeipenda nisinunue... badala yake niwe ovyo ovyo... ili kila mtu ajue nina maisha magumu... halaf ndo nini sasa..!!!!
Soma vizur na kwa umakini uelewe best
 
nice
 
kwahiyo unamaanisha nikiona nguo nzuri nimeipenda nisinunue... badala yake niwe ovyo ovyo... ili kila mtu ajue nina maisha magumu... halaf ndo nini sasa..!!!!
hujaambiwa kuwa ovyo... kuna tshirt nzuri tu ya 15,000/= kwa nini ukimbilie ya 45000/= wakati uwezo mdogo
 
Sio kila anayefanya hivyo anaigiza wengine anafanya kitu nafsi inapenda hatuwezi kuwa level moja
Jidanganye Kwa kuiga,wakati unammufaisha mwenzako.ata kama uwezo unaruhusu sioni sababu ya kununua kitu Kwa bei ya anasa..!labda hauna majukumu.
 
Sio kila anayefanya hivyo anaigiza wengine anafanya kitu nafsi inapenda hatuwezi kuwa level moja
Najua umeelewa sana sema kuna kitu kidogo ukiambiwa utaelewa zaidi

Unaposema hatupo level sawa sijapingana na wewe hata kidogo ni ukweli kabisa watu ambao wamejaliwa kipato kikubwa zaidi ni marachache sana huwa wanaishi maisha ya kuigiza.... angalia maisha ya vijana wengi wa Tanzania wanaoiga maisha ni maskini kuliko matajiri..

So nachojaribu kukieleza hapa ni ishi kutokana na kipato chako cha kinavotaka na sio kinavyotaka bali na malengo yako uliyojiwekea maishani. Unapoishi nje ya haya mara nyingi unakua unaishi kuwapendeza watu waliokuzunguka lakini sio jinsi malengo yako yanavotaka na mbeleni unakuja kutambua muda ukiwa umeenda...
 
Kuna msemo nadhani ni Bill Gates alijibu baada ya kuulizwa mbona maisha yake hayaonekani kama ni ya mtu tajiri zaidi duniani.

Alijibu hivi "The point is to be rich no to look rich" yaani "Cha msingi ni kuwa tajiri sio kuonekana tajiri"
 
Kuna mtu anawaza atakula nini sababu hakuna hela lakini akiona nguo mpya kavaa msanii mkubwa mfano diamond platnumz yupo tayari asile lakini avae nguo zile...Maisha haya ni ya kuigiza bila sababu..
Hapana hii sio kuigiza. Hii ndio maana halisi ya KUPANGA NI KUCHAGUA. Na kila mtu ana mipangilio yake ya maisha, nini kipaumbele chake kwahio usitegemee watawaza au kuamua kama wewe.
 
Back
Top Bottom