Epuka haya majibu kutoka kwa mwanamke!

Tugas

Tugas

Senior Member
166
250
Mwanamke Akikujibu SMS yako Hivi Acha Haraka Sana Kuchat Nae Haraka Sana

Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.

KWA MFANO:

1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo mabaya'', usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ''sina hela dear''

2. Ukimtumia sms ''Maisha yanasemaje kipenzi changu'' akikujibu ''maisha magumu hubby wangu we acha tu'' usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ''nimefulia mwenzio kama nini sijui''

3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa kiasi hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi'' usimuulize kwanini mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani sina kitu mpenzi wangu, simu ilikuwa haina hata hela ya kubeep''

4. Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu? We mkatalie kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa upo serious.

Ni mara chache sana mwanamke akikwambia kuwa mambo mabaya, maisha magumu au mambo hayaendi huwa na matatizo mengine kama kuumwa, misiba.... n.k lakini THE REST ni wapigaji mizinga tu. Akikwambia maisha magumu mjibu ''pole wangu, mambo mengine vipi?''

Ukipewa majibu kama hayo, chagua moja, either usiendelee kuchat nae mpaka badae kidogo au mbadilishie maada ili kukwepa huo mzinga ambao unakuja mbele yako.

Ni akili yangu tu
 
ukuwi

ukuwi

JF-Expert Member
677
1,000
Inamaana huu Uzi haujapata wachangiaji maana niliuona muda umepita kwahyo paka leo watu wameamua kuupotezea
Basi ngoja niwe siti ya mbele kabisa na mimi leo nimewahi siti.
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
29,397
2,000
Looh... You guys are getting reply?
 
Tugas

Tugas

Senior Member
166
250
Inamaana huu Uzi haujapata wachangiaji maana niliuona muda umepita kwahyo paka leo watu wameamua kuupotezea
Basi ngoja niwe siti ya mbele kabisa na mimi leo nimewahi siti.
Wewe unajua vzr kuna watu umewagusa moja kwa moja, lazima watafakari kwanza.
 
A

adolay

JF-Expert Member
11,098
2,000
Inamaana huu Uzi haujapata wachangiaji maana niliuona muda umepita kwahyo paka leo watu wameamua kuupotezea
Basi ngoja niwe siti ya mbele kabisa na mimi leo nimewahi siti.
Wewe sio mchangiaji?
 
Castr

Castr

JF-Expert Member
15,750
2,000
Sasa usiombe ubanwe na nyege. Halafu anayetakiwa kuzitoa ndiyo kakuomba hela na wewe hela huna.

Unaweza tamani kujito.mba
 
Noah de voxser

Noah de voxser

JF-Expert Member
1,118
2,000
Wanaume mmefikia kutuogopa hivyo dah , hayo maneno huenda tunakua na matizo mengine tu na si vizinga banaa
Hahaha maisha hata

Kuna Dada nlimpendaga sana sana sana
Kipind iko sina ajira....kwa kipaji changu nikawa napata japo kidogo.....pia nnaishi home nikawa nnampa yeye hicho kidogo nachokipata....
Akaja pata MTU mwenye Hera nyingi...kaniacha na maneno juu.....et ananambia au nikulipe pesa zako..!?
Wiki tatu mbele akanipgia akanambia usinijue tangu Leo...Fanya yako nfanye yangu.....Mimi nikasema sawa haina tabu..maisha yaendelee

Jana kanambia nisaidie walau...elfu.....(...) Moyo unauma kumyima ila nikikumbuka dah...
 
P

Philibert Buyobe

New Member
4
45
Bora umejiwazia tu ww babe wako waubani kabisa atakupiga mzinga?! Au unaongelea mchepuko
Kwel kabisa kwa mtu wako wa nguvu( mpenzi wako) hawezi kuwaza kukupiga mzinga kias hicho, kiuhalisia atakuwa kibenteni tu. Lakini pia Kama Una malengo naye makubwa tafuta namna ya kumwondolea hizo fikra kwa mfano siku zingine mpigie simu muulizie na umshauri mambo ya ujasiliamali uone je ni MTU anapenda kutafuta ili kuondokana na utegemezi? Au atonekana anapenda tu vya kupewa? Wakati mwingine Kama kuna mahali pengine labda kuna semina yoyote ya vijana na maisha mshirikishe uende naye ajifunze mwisho ataona thamani yako na atakupenda zaidi kuliko ulivyodhani hapo awali, sambamba tu na hilo mkabidhi kwa Mungu katika maombi yako na ikiwezekana uambatane naye kwenda kanisani, Rafiki yangu kwa mwanamke mwenye malengo na wewe lazima kuna kitu atakihisi kuwa unacho wewe tu na wala si mapesa Bali upendo, ambao hajawahi uona kwa mwanaume mwingine, AHSANTE
 
M

Maelau

JF-Expert Member
1,338
2,000
Sasa usiombe ubanwe na nyege. Halafu anayetakiwa kuzitoa ndiyo kakuomba hela na wewe hela huna.

Unaweza tamani kujito.mba
Comment ya hovyo kabisa kuwahi kutokea katika mwaka huu wa jamiiforum.
 
MR KUO

MR KUO

JF-Expert Member
1,174
2,000
Kwanza Sasa hvi hayo maswali yote sidhani Kama Kuna maanaume anayemuuliza mwanamke wake.

Siku hizi ni;

Mambo vipi? Niko njiani nakuja huko uko wapi?

Hello dear leo naomba ukanitembelee hapa Kwangu natuma tax/boda boda Sasa hivi nijibu Kama upo kwako.

Good morning mama, nimekutumia ile elfu 5,10,20,.... uliyoniomba samahani kwa kuchelewa nilikuwa na Mambo mengi. (I Miss you).

NB. hii ni kwa wale ambao dakika moja wanajenga mapenzi na sekunde tano au kumi tu wanayabomoa endapo Mambo yataenda kinyume na matarajio yao.
 

Forum statistics


Threads
1,425,226

Messages
35,085,100

Members
538,249
Top Bottom