EPL Matchday – Uchambuzi na tathmini

EPL MATCHDAY 5 –​


1. MANCHESTER CITY 5–3 SUNDERLAND​


Manchester City imeendelea kuongoza ligi baada ya kuifunga Sunderland mabao 5–3 katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa na mabao mengi.

Ushindi huu umeifanya City kufikisha pointi 15 baada ya kucheza mechi tano, ikiwa imeshinda kila mchezo. Sunderland walijibu kwa nguvu na Brian Brobbey akafunga hat-trick, lakini City ikaweza kulinda ushindi wake hadi mwisho.

2. BRIGHTON 3–0 ARSENAL​

Arsenal imepata kipigo chake cha kwanza msimu huu baada ya kufungwa mabao 3–0 na Brighton.

Baada ya kuanza msimu kwa ushindi katika mechi nne za kwanza, Arsenal safari hii haikupata majibu dhidi ya Brighton. Kipigo hicho kimeifanya Arsenal kubaki na pointi 12 baada ya mechi tano.

3. BRENTFORD 3–0 CHELSEA​

Chelsea imepata pigo jingine baada ya kufungwa 3–0 na Brentford.

Brentford ilitumia vizuri nafasi zake na kuchukua pointi zote tatu, huku Chelsea ikishindwa kupata bao katika mchezo huo.

4. TOTTENHAM 2–3 ASTON VILLA​

Aston Villa imepata ushindi wake wa kwanza wa ligi msimu huu baada ya kuifunga Tottenham 3–2.

Tottenham bado haijapata ushindi baada ya mechi tano za ligi, hali ambayo inaendelea kuwa changamoto kwa Spurs katika mwanzo huu wa msimu.

​

5. EVERTON 1–0 IPSWICH​

Everton imechukua pointi zote tatu baada ya kuifunga Ipswich bao 1–0.

Ilikuwa mechi ngumu yenye bao moja pekee, lakini Everton ikaweza kulitunza bao hilo na kumaliza mchezo akiwa mshindi.

6. NEWCASTLE 2–1 HULL CITY​

Newcastle imeifunga Hull City 2–1 na kuipa Hull kipigo chake cha kwanza msimu huu.

Hull ilikuwa imeanza vizuri msimu bila kupoteza, lakini safari hii Newcastle ikaweza kupata ushindi na kuchukua pointi tatu.

7. NOTTINGHAM FOREST 0–1 COVENTRY CITY​

Coventry City imepata ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kuifunga Nottingham Forest 1–0.

Bao la Jay Dasilva lilitosha kuipa Coventry pointi zote tatu.

​

8. LEEDS 0–0 CRYSTAL PALACE​

Leeds United na Crystal Palace zimetoka sare ya bila kufungana.

Leeds imeendelea kuwa haijapoteza mchezo wowote baada ya mechi tano, lakini sare hii imeifanya ikose nafasi ya kuongeza pointi tatu.

​

9. BOURNEMOUTH 0–1 LIVERPOOL​

Liverpool imechukua pointi tatu baada ya kuifunga Bournemouth 1–0.

Alexander Isak alifunga bao pekee la mchezo na kuiwezesha Liverpool kuondoka na ushindi muhimu ugenini.

​

10. FULHAM 1–1 MANCHESTER UNITED​

Manchester United imelazimika kugawana pointi na Fulham baada ya sare ya 1–1.

Fulham ilitangulia kupata bao, lakini United ilisawazisha kupitia Matheus Cunha na kuondoka na pointi moja.

United sasa ina pointi 5 baada ya mechi tano za ligi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…