EPA stories

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,020
577
SOurce: Yahoo friends
Kuna taarifa zinasema kuwa; Mkapa baada ya kusakamwa sana na UFISADI,
siku moja akiwa nje ya nchi, alikutana na Mwandishi mmoja ambaye
alikwenda huko kwa ajili ya kupokea Tuzo, baada ya kusalimiana
walialikana katika Mgahawa na kunywa Chai ambapo Mazungumzo yao baada
ya kujuliana hali yalikuwa hivi;

Mkapa: Vipi Siasa za kwetu, hali ikoje.
Mwandishi: Zipo zinaendelea tu.
Mkapa: Hongera kwa kuchukua tuzo, kwani huu ndiyo uandishi niliokuwa
nikiusema wakati wa utawala wangu ila hamkunielewa tu.
Mwandishi: Asante. mbona umekuwa kimya sana.
Mkapa: Ahaa! Nimeamua, tena wewe si mwandishi bwana sasa leo nakupa
mtihani. naomba Muulizeni Kikwete anaifahamu vipi EPA?
Mwandishi: Kwani ilikuwaje mkuu?
Mkapa: Unajua mie nikiwa Madarakani, Kikwete alikuwa akitambulika
ndani ya UWT kwa Codename ya 'Malaika'. Siku Moja kabla ya kuingia
katika Uteuzi wa wagombea wa Chama, nilifuatwa na watu wa Usalama na
kuambiwa kuwa Malaika atashinda. Sikuwa namtaka awe kiongozi kwa vile
nilimfahamu, lakini watu wa Usalama wakaniambia, Mzee hamna namna
kwani ameshakamata mfumo wote wa chama na baadhi ya UWT, Jeshi na
sekta muhimu, hivyo wakanitaadharisha kwamba iwapo nitamzuia nchi
itayumba. Nilishangaa lakini sikuwa na namna zaidi ya kuinusuru nchi,
niliwasiliana na wazee katika chama na kuamua kukubaliana nao
kuiepusha nchi katika matatizo.
Lakini siki chache baada ya Dodoma kumpitisha Malaika, nilifuatwa na
maofisa wake na kuelezwa kuwa Malaika alikuwa akitaka fedha kwa ajili
ya kampeni, Ukweli nilimaka, na kuhoji nitazipata wapi. Wakanieleza
amesema zipo BoT. Niliamua kumuuliza gavana (Balali) kwa simu, kuwa
Chama kilikuwa kikitaka fedha kwa ajili ya Uchaguzi, Balali akajibu
hakukuwa na fedha.
Kutokana na majibu hayo Malaika akamfuata Mkapa na kumueleza anajua
kila kitu na kwamba kulikuwa na Fedha za malipo ya nje alikuwa akiomba
hizo kwa ajili ya kampeni za chama. Nikamueleza Balali ambaye alisema
fedha hizo haziwezi kutolewa mpaka kuwepo na doccument, baada ya
majibu hayo kufikishiwa Malaika na watu wake walifika na kuwasilisha
doccument kwa Balali na kuzitoa fedha hizo.
Mwandishi: Duh...inamaana EPA alicheza Malaika?
Mkapa: Ndiyo maana nakutaka ukipata nafasi muulizeni Kikwete anaijua
vipi EPA?

Source: Habari hii nimeisikia kwa mwandishi mmoja nchini aliyewahi
kushinda Tuzo akimsimlia mtu wangu mmoja wa Karibu nami.

 
Hii habari mbona ipo hapa janvini mda mrefu, hebu angalia post ya last wk yenye kichwa"habari ndo hiyo"
 
Back
Top Bottom