Mwakumbuka Gurubiti za kijiti cha chelewa, Mabumunda je?? Good Good je? mwakumbuka tulikuwa twala mapera kwa wingi sana??
Nakumbuka hizo enzi nasoma Lake Primary School - Isamilo na Nyanza Primary pia nilisoma jamani kaaaaa sijui kama mwalimu Tumbo yupo mpaka leo
sana I see yaani nimemaliza primary nikijua kukata na kushona nguo hata kama ilikuwa ni kwa kutumia mikono lakini ni elimu tosha, kulikuwa na cookery hadi secondary. Pia kulikuwa na hiyo useremala na bustani za nyanya mbogamboga hadi ufugaji kwa hiyo ulikuwa ukitoka shule unajua kilimo cha kisasa kwa kiasi Fulani unaweza anza kujitegemea kabisa. Mitaala imebadilishwa weee hata sijui tunaenda wapi?Ukweli kabisa Mama Joe nakumbuka shuleni kwetu walifundisha mpaka ufundi, useremala, kutengeneza vigae vya kuezekea, na waliofanya vizuri walizawadiwa zana za kufanyia kazi!..SIPATI PICHA LEO TUNGEKUWA WAPI KAMA TUNGEKUWA NA MFUMO MZURI WA ELIMU!
Mwakumbuka Gurubiti za kijiti cha chelewa, Mabumunda je?? Good Good je? mwakumbuka tulikuwa twala mapera kwa wingi sana??
Nakumbuka hizo enzi nasoma Lake Primary School - Isamilo na Nyanza Primary pia nilisoma jamani kaaaaa sijui kama mwalimu Tumbo yupo mpaka leo
Nakumbuka asubuhi unawahi namba, mkononi una fagio la chelewa, kidumu cha maji, mbolea, maua and sometimes panga, fyekeo au jembe! du enzi zi la full Kayumba tulikomaje? sio sasa hivi watoto wetu hawajui lolote!!!!
sana I see yaani nimemaliza primary nikijua kukata na kushona nguo hata kama ilikuwa ni kwa kutumia mikono lakini ni elimu tosha, kulikuwa na cookery hadi secondary. Pia kulikuwa na hiyo useremala na bustani za nyanya mbogamboga hadi ufugaji kwa hiyo ulikuwa ukitoka shule unajua kilimo cha kisasa kwa kiasi Fulani unaweza anza kujitegemea kabisa. Mitaala imebadilishwa weee hata sijui tunaenda wapi?
Na ole wako usahau dada yake Juma anaitwa nani (Roza) kwenye Kiswahili kwenye vitabu vile 'Tujifunze Lugha Yetu' Kwenye English lazima ujue Mr & Mrs. Daud na watoto wao Musa na Neema wanaosoma Mtakuja Primary School. Those were the good old days!!!!
tukienda kwenye soka hatukusahau kushangilia kuwa Joshua! joshua! joshua! namna huyo! ukitoka nione!. mtu akimkata mtama unamjibu wewe, wewe usiniumizie!
mkuu nashukuru kwa kutukumbusha ya enzi zile!
...Wamo humu wa Mfaranyaki Primary School, Songea LY Class ya 1974...Sijakosea, 1974 ???? ππ
duh nilikuwa naogopa sana viboko, ajabu nilianzia shule ya Nyakahoja hapo Isamilo hawakuwa wanachapa kabisa ukikosa kuna kusimama nje ya staffroom hadi jioni....ajabu tulikuwa tunaogopa sana tunaita prison....mtu analia kweli na wote tunawaona wameadhibiwa kweli...kuja hama mkoa nikaenda kwa kayumba duh chamoto nilikiona! Kikubwa tulikuwa tunafundishwa kiasi huitaji tuition na unafaulu national exam ka kusoma tu mwenyewe nyumbani. Go tell this to my kids lol...Enzi hizo ukitoka shule bila kuchapwa unamshukuru Mungu
Mnatoka saa sita na nusu kwenda kula home, saa nane mnatakiwa mrudi shule, jua kali halafu unafika home unakua hakuna msosi, anambulia kunywa maji then unageuza
Sitasahau halaiki ya mwaka 1986 kuzima mwenge kitaifa mkoani mwanza, tulihenyeshwa balaaa
mmm kweli kulikuwa na kazi za ajabu...ila ukiwa mtii na msafi unapewa kazi ya kutunza ofisi za walimu au maktaba nashukuru niliponea maana vile vyoo unatoka na perfyum kali...Umesahau kufagilishwa vyoo na kulimishwa mjini.
Ahahahahahhhh, dah yaani nimecheka kwa sauti hadi wenzangu wamenishanga, Hakyanani nimekumbuka mbali sana. Halafu kukariri tebo darasa la pili, nakumbuka mkimuona tu mwalimu ametoka ofisini darasa zima mnasimama mnaanza kuimba tebo, akiingia darasani wote mnanyamanza anaanza kuuliza mtu mmoja mmoja, ole wako ushindwe kujibu, utajuuuta kumfahamu mwl Samson lol!
Darasa la tano sitakuja kusahau hesabu za vipeuo, K.D.S na K.K.S wapi mwl Bunango, ulinichapa sana mama lakini ahsante ulinisaidia na kunifanya niwe hapa nilipo leo
Ram,
Huyo mwalimu Bunango alikufundisha wapi na miaka ipi? Halafu kulikuwa na hesabu ya kangaroo darasa la 5 (au la 6???)