kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
thread yako imeongelea mambo ya maana kuzidi hata hotuba ya mheshimiwa
Lazima ujifunze:
1. Sayansi Kimu
2. siasa
3. Sanaa
4.jiografia
5.hesabu
6.sayansi kilimo
7.sayansi
8.kiswahili
Wakati wa mapumziko lazima ucheze,
1. Mpira (Chandimu, one touchi, mputo)
2. Netboli na rede
3. Mdako
4. Bong'oa
5. Kula m'bakishie baba
6. Kubanjua Gololi
7.mnataniana kwa kutomoana
8.mnasimuliana movie za kihindi kina amithah bachan,mithun,chuck noris,amjed khan.
9.kucheza kiboleni
Msosi wakati wa mapumziko.
1. Mihogo ya kukaanga na chachandu
2. Aishiklimu
3. Barafu
4. Kashata
5. Bagia (za walimu)
6.vibama
7.gubiti
8.ubuyu wa rangi
9.ukwaju
10.visheti
nguo
1.unavaa kaptula 2 kuzuia maumivu ya viboko
2.unaweka daftari au gazeti ndani ya kaptura basi tigo ikionekana kubwa mwalimu anakuambia vua
tukienda kwenye soka hatukusahau kushangilia kuwa Joshua! joshua! joshua! namna huyo! ukitoka nione!. mtu akimkata mtama unamjibu wewe, wewe usiniumizie!
mkuu nashukuru kwa kutukumbusha ya enzi zile!
thread yako imeongelea mambo ya maana kuzidi hata hotuba ya mheshimiwa
Mwakumbuka Gurubiti za kijiti cha chelewa, Mabumunda je?? Good Good je? mwakumbuka tulikuwa twala mapera kwa wingi sana??
Nakumbuka hizo enzi nasoma Lake Primary School - Isamilo na Nyanza Primary pia nilisoma jamani kaaaaa sijui kama mwalimu Tumbo yupo mpaka leo
mkuu senksi kwa thread taaamu zangu ilikuwa wakati wa mapumziko tunapiga one touch au gombania goli. mpira wake tuliokuwa tunautumia tukiuita pumbu soksi yaani unatengenezwa kwa soki. unajaza makaratasi kwenye soksi unaifunga soksi kwa kamba si mchezo. na kule kwetu songea kuna ule mpira unaitwa MUHOGO MPIRA yaaani unatengenezwa kwa ute wa muhogo ni km GOZI lenyewe lkn unkua mlaini kidogo
wewe umesoma songea mfaranyaki,lizaboni au bomba mbili pia kuna shule moja maarufu pale inaitwa misufini!!hiyo one touch nimecheza sana primary pale iringa jamani utoto we acha tu yaani life ilikua simple sana kulikuwa na umiseta na umitashumta!
kaka nimesoma MAHENGE primary school pale jirani na TTC matogoro aah kaka imanikumbusha mbali sana hasa embe maji na embe bolibo halafu nilihamia pale std three nikitokea JANGWANI pr school SUMBAWANGA nikakutana na washkaji wamepinda kinoma walikuwa watoro wa shule vibaya mno wengine wakikaa sehemu inaitwa KWA KUCHILE nyuma ya kambi ya jeshi ya CHANDAMALI hawa walikuwa wataala mno wa kusepa so walikuwa km ishirini hivi wakiitwa KUCHILE LIST mara nyingi walikuwa wakija shule km kuna graduation au mechi kati ya shule na shule. HAWA JAMAA siku moja mchana wakaniambia twende tukale ndizi kwenye shamba la bibi mie na njaa yangu nikasepa nao kumbe lile shamba ni la chuo cha ualimu MATOGORO bwana weeee tukaingia swaafi nikakuta jamaa walishavundika ndizi long time so walikuwa wazoefu kule. tukatafuna km mkungu na nusu hivi mara mlinzi huyooooo tjatoka baluuu hao shuleeee kumbe yule mlinzi anatu track akaja shuleni kumbe alitushika vizuri tulivyo eeeh bana eeh zoezi la utambulisho lilipopita jamaa alitambua wanne kati ya sita tukabaki wawili tu wale waliotambuliwa ndo wakaaribu kabsaaaa wakatutaja na sisi duuuh tukala fimbo za kufa mtuu mbaya zaidi mza na yeye alikuwa mwalimu akifundisha shule nyingine taarifa zikamfikia dingi akapewa jukumu nikikula fimbo tenaaa home dah yaani toka siku hiyo nikabadilisha na marafiki hahaa

Aaah ilikuwa zamani hiyo kweli mambo c yale tena...tuliosoma Chang'ombe Pr school nafikiri tunakumbuka tukiwa mstarini wale wenye kesi ya uhaini ndo walikuwa wanapitishwa pale asubuhi kuelekea mahakamani....
uwanja wa Taifa kuruka ukuta....
Lazima ujifunze:
1. Sayansi Kimu
2. siasa
3. Sanaa
4.jiografia
5.hesabu
6.sayansi kilimo
7.sayansi
8.kiswahili
Wakati wa mapumziko lazima ucheze,
1. Mpira (Chandimu, one touchi, mputo)
2. Netboli na rede
3. Mdako
4. Bong'oa
5. Kula m'bakishie baba
6. Kubanjua Gololi
7.mnataniana kwa kutomoana
8.mnasimuliana movie za kihindi kina amithah bachan,mithun,chuck noris,amjed khan.
9.kucheza kiboleni
Msosi wakati wa mapumziko.
1. Mihogo ya kukaanga na chachandu
2. Aishiklimu
3. Barafu
4. Kashata
5. Bagia (za walimu)
6.vibama
7.gubiti
8.ubuyu wa rangi
9.ukwaju
10.visheti
nguo
1.unavaa kaptula 2 kuzuia maumivu ya viboko
2.unaweka daftari au gazeti ndani ya kaptura basi tigo ikionekana kubwa mwalimu anakuambia vua
Umesahau BULGA
hahaaaaaaa mashamba ya matogoro nayajua sababu nimesoma pale na tumelinda sana yale mashamba dah umenikumbusha mbali kambi ya jeshi chandamali yaani mimi songea sio home ila nimesoma ttc pale na nimeishi sana kule na kucheza mipira vijijini na pale town kuna timu ilikua inaitwa bogota unaikumbuka?