Enzi ya Usichana Wangu Tanzania Was Very Beautiful | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enzi ya Usichana Wangu Tanzania Was Very Beautiful

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by DSN, Aug 3, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Enzi ya Usichana wangu Tanzania ilkua NCHI NZURI sana hiyo ni kauri ya Mbunge kutoka Mwanza Mama Maria Hewa mwenye takribani miaka 60 na ushehe amesikika akiwaambia wabunge wa Jamhuri ya Muungano.

  Mama huyu kilio chake kikuu ni usafiri wa Reli ya Kati toka Dar es Salaam mpaka Mwanza.Anasema wakina Mama Kigogo waliendesha maisha yao kwa kuuza asari na biashara ya vikapu vyao kwenye treni lakini UKOSEFU WA HUDUMA HIYO YA USAFIRI WA ABIRIA KWA NJIA YA TRENI hiyo umeua shughuri na kipato cha Wakina mama hao WA MIKOA YA MOROGORO,DODOMA ,SINGIDA,TABORA,SHINYANGA,MPAKA MWANZA.

  Anasema pia enzi za usafiri wa treni kwa kanda hiyo ya kati na ziwa hata kusikia mlio tu wa treni ya abiria nayo ilikua raha tosha kuwa uenda ukapata MGENI toka Dar es Salaam.

  Mama huyu kanikumbusha wakati fulani jamaa mmoja toka kanda ya ziwa mara ya kwanza anaiona Treni pale Mwanza ikitoka pale Feri,jamaa alishangaa kusikia treni inaongea.Kwa kusikia mwendo wa treni wakati inapochukua kasi ya kuondoka sauti yake "chakachaka chakachaka "na mlio wa sauti ya honi yake phoooooooooooooooo.Jamaa ajawaingiza mtaani wenzie alipoludi kwao kuwa ameona treni inayosema kiluga chao.Mabobishi yake kwa wenzie amesikia treni ilikuwa inasema "chacha mwita marwa!!!!!! chacha mwita marwa!!!!!! chacha mwita marwa!!!!!!!" kisha inamalizia kwa kusema Mulaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!.

  Jamani kwa kanda ya ziwa yote na magharibi treni ni historia kubwa sana,manake hata ndugu zetu waha walikuwa wakiingia mjini dar kwa usafiri huo akifika jijini pale stesheni walikuwa wanataniwa kuwa wanaingia na jina la Karumanzira akiachia tu geti la stesheni Dar es Salaam anamwambia mwenzie asimuite KARUMANZIRA bali amuite BROTHER K kwa kuwa watoto wa mujini wakimsikia anaitwa Karumanzira watamtarai.

  Ilikuwa raha kwa jiji la Dar mitaa ya Kariakoo na Mitaa ya Gerezani Wakazi wa maeneo hayo walikuwa wakisikia Mlio wa honi ya Treni ikiingia Dar es Salaaam walikuwa na shangwe za kelele kama "waleteeeeeeeeeeee wa wabalaaaaaaaaaa haoooooooooo"basi yote hayo yalikuwa na raha zake tele.

  Usemi wa Mheshimiwa Mama Maria Hewa [Mbunge Mwanza] ni kweli enzi ya Usichana wake Tanzania yetu ilikuwa nzuri na raha tele.Kama ujawahi kusafiri na treni uwezi kujua starehe ya usafiri huo.Kukosekana kwa usafiri huo Watanzania wameathirika sana kiuchumi ,kiutamaduni na vimbwanga kibao vya watumiaji wa usafiri huo wengi wakiwa ni Wasukuma, Waha, Wanyamwezi, Wanyiramba, Wahaya, Wakurya, Wajita, Wagogo, Wamanyema na makabila mengine yatokayo kanza za kati,magharibi na ziwa.

  Basi kwa muungano wa makabira hayo ndani ya treni kulikuwa na burudani tosha ukianzia na utani wa kikabila haswa uwe kwenye daraja la tatu la usafiri,basi buludani tupu umkute Mkurya dhidi ya Mnyiramba na Mhaya wote wako ndani ya treni wanakuja Dar es Salaam,Msukuma na Mnyamwezi dhidi Muha na Wanapwani,Wagogo n.k.

  Jamani wewe unaikumbuka safari yako ya treni.Kukataliwa kwa Bajeti Ya UCHUKUZI ni mwanzo mwema wa kuenzi jadi yetu ya Usafiri wa Treni kwa Maslahi ya Taifa.Na kudumisha historia na burudani ya usafiri huo katika kiwango cha kisasa zaidi na wenye tija na manufaa.

  Nawasilisha!!!!!
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,403
  Likes Received: 5,679
  Trophy Points: 280
  tanzania ni bomba mbaya kabla ujazaliwa na mpaka sasa mama maisha ni jinsi gan utakavyoweza kuyakatia denge le mema ya nchi humu duniani
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  sijaokota kitu ndugu.Hebu nifafanulie...
   
 4. l

  luckman JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  More are still coming!nawapongeza baadhi ya wabunge wenye maadili ambao hawataki kuchafuliwa taswira zao kwa kuona ubaya wa ccm na kuukemea !
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,859
  Likes Received: 2,336
  Trophy Points: 280
  itakuwa nzuri tu - subira yavuta kheri - cha msingi wote tuwe na moyo wa mapinduzi ya pili, tukiachana na wanasiasa uchwara ambao wanatuingiza chaka kila kukicha.
   
 6. F

  FUSO JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,859
  Likes Received: 2,336
  Trophy Points: 280
  Enzi za Tren:

  Station ya Salanda: Moshi Hotel, Kuku choma, Pilau la nguvu
  Station ya Kitinku: Kuku mishikaki....
  Station ya Itigi: Igalula na Goweko i: Asali Mbichi
  Station ya Aghondi: Ubuyu na vigoda asilia
  Station ya Bahi: Ubuyu na mikeka
  Station ya TABORA: Abilia chunga mzigo wako - ukizubaa tu WAFWAAAA......
  Station ya Fela: Hapo mzee unaliona jiji Hiloo la mwanza......
  Station ya Mwandiga (Kwa Mh. Zitto): Migebuka bei cheee....
  Station ya Vigunguti to DSM ... Walete haoooooo, waleteee haooo wa kujaaaaa, walete hao wa baraaaaa.....
  Jamani zamani RAHA tupu........

   
 7. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Zito anaikataaa Budget ya uchukuzi,manake kasuru tutafiikaje ndio tunataka tuweze inawezekana.
   
Loading...