Enzi hizo bwana, dah!

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,519
7,556
watoto wengi wa siku hizi hasa sehemu za mijini wana nafasi au uwezo wa kuangalia movies, televisheni majumbani mwao. lakini nakumbuka miaka kama ya 1990 wakati huo naishi CRDB maghorofani (au Kijitonyama hostel za UDsm kwa sasa) chance hizi tulikuwa tunazipata kwenye nyumba za watu wengine tena sanasana kuangalia movies tu, vituo vya tv binafsi hakuna wakati huo zaidi ya TV ZNZ tu. nakumbuka mida fulani ya mchana tukijua tu kwamba jamaa wanacheki muvi hiyo weekend, mtu tunatiririka baada ya kufunguliwa mlango. sometimes wanawakaushia wakiona mnazingua. basi hapo unaweza kukuta sebelu imejaa zaidi ya watu 10. sasa ole ako uwe umemzingua dogo ambaye kwao ndio huwa unakwenda kucheki movie, dogo atakwambia ''nosom bade'' akiwa na maana ''not so bad'' si unajua maneno ya kuokoteza kwenye movie, hutakanyaga ndani kwao, hata ukija na wenzako, wao wataingia wewe atakutosa mpaka ukubali yaishe. dah! hivi haya mambo ushawahi kukutana nayo enzi zako?
 
Back
Top Bottom