Enzi hizo bhana

Madereva wa mabasi hayo walikuwa wanaheshimika sana, na walikuwa ni watu wazima tu na ndo maana ajali zilikuwa chache sana ukilinganisha na siku hizi.

Hilo lilikuwa basi la Railway likitoka Mbeya mpaka Itigi ; linapita Kipembawe na Makongorosi usiku na kuingia Itigi asubuhi kuwahi treni ya kwenda DAR au Kigoma au Mwanza!!!
 
Hilo lilikuwa basi la Railway likitoka Mbeya mpaka Itigi ; linapita Kipembawe na Makongorosi usiku na kuingia Itigi asubuhi kuwahi treni ya kwenda DAR au Kigoma au Mwanza!!!

Zile Leyland DAF zilikuwa ngumu sana...halafu unakuta imejaza watu hadi juu ya 'keria'...na tandiboi yupo huko
 
Hivi mabasi ya UDA yalikuwa yanaendeshwa na wazungu? Na hilo jengo hapo pembeni mwa hilo bus liko wapi hapa Dar? Nina wasiwasi hiyo ni kazi ya photo duka wanaita.

Tiba
 
Daah, mmenikumbusha yale mabasi ya kule kwetu. Pale moshi kulikuwa na mabasi ya trip town miaka ile ya 80 yakienda kiboriloni, majengo, KCMC na maili 6. Nani anakumbuka SHIMAWIMO.
Kulikuwa pia na basi la kwenda kibosho kupitia wildlife college, leyland cd, likiitwa Punguza shida Mabasi kama UTUKA lililokuwa likienda uru kupitia mawella. KAUKI likifanya safari zake uru east a.k.a kishumundu. Mmenikumbusha mbali.
 
Photograph interpretation! Picha haiongeshi enzi hizoooooooooooooooo, ni miaka michache sana hapo nyuma kwa sababu MNARA wa simu unaonekana. Halafu si ule wa ttcl zamani (rangi ya aluminium kama sikosei) Hivyo picha ni ya enzi hizi hizi! Ni mtazamo tu.
 
Kulikuwa na basi moja tu miaka ya sitini mara tu baada ya" UHURU WA BENDERA" linatoka Kariakoo mpaka Kisarawe mali ya muhindi akiitwa NANJI likiitwa "HAPA JE"? Dereva wa gari hili alikuwa bwana mmoja ambae alikuwa mshairi mzuri sana enzi hizo!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…