Enyi wanaume mliooa na mnao tarajia kuoa

Enyi wanaume mliooa na mnao tarajia kuoa

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,474
Reaction score
4,007
  1. Mpende mke wako mzuri, usimkaripie mke wako ukiwa unaongea nae inamuumiza sana,
  2. Usimuongelee mkeo ubaya kwa mtu yeyote, mke wako atakua kile ambacho unamuita,
  3. Usimpe mwanamke mwingine upendo anaostahili mke wako, huo ni uasherati,
  4. Usimlinganishe mke wako na mwanamke mwingine maana kama huyo mwanamke alikua anakufaa basi Mungu angekupa umuoe,
  5. Uwe mpole, mvumilivu na msikivu kwa mkeo, maana yeye mwenyewe amevumilia mengi na amejitolea na ameacha vingi ili awe mkeo, inamuumiza sana unapokua mkali na kumkera,
  6. Usimfiche chochote uwe mkweli na muwazi kwake, mmekua kitu kimoja na hivyo ni msaidizi wako, usiweke au pasiwepo na siri yoyote kati yenu,
  7. Usiseme kitu kibaya kuukosoa mwili wake kama inawezekana mrekebishe, amejitolea uzuri wake na mwili wake kukuzalia wew watoto, amejipanga vizuri ili akusalie watoto, au ameshindwa kupata watoto na ameamua akuvumilia kuwa na wewe kwa kipindi kigumu kama hiki, ni binadamu pia mwenye moyo, sio mwili tu,
  8. Usiulinganishe mwili wake na thamani yake, mthamini hata pale mtakapofikia uzee,
  9. Usimkaripie kwenye umati wa watu, suluhisheni matatizo yenu chumbani mkiwa wenyewe,
  10. Mshukuru kwa kuwalea watoto wenu vizuri au kuwalewa watoto mlio nao ndani kwenu, nyumba yako pamoja na wewe kwani amejitolea kufanya hayo yote,
  11. Mapishi ya wanawake hayafanani na hayawezi kufanana, furahia mapishi ya mke wako sio rahisi kumpikia mtu milo mitatu kwa siku kwa siku 365 kwa mwaka kwa miaka mingi mlioishi wote au mtakaoishi wote,
  12. Usiwaweke ndugu zako kabla yake, yeye ni mke wako ndiye anaekaa na wew, lazma umpe kipaombele kabla ya ndugu zako,
  13. Wekeza katika ukuaji wake kiroho, mnunulie vitabu, na chochote ambacho kitamsaidia kukua kiroho atembee na mwenyezi Mungu siku zake zote, hicho ndicho kitu cha pekee unachoweza kumfanyia mke wako,
  14. Tumia mda wako ukiwa nae kujifunza quran/ bibilia na kusali,
  15. Tenga muda wa kukaa nae, kucheza nae na kufurahia uwepo wake, kumbuka, utakapofariki, yeye ndiye ataaesimama pembeni ya kaburi lako huenda marafiki zako
    wakawa na kazi nyingi na kushindwa kuhudhuria,
  16. Usitumie pesa zako kumrubuni au kumpelekesha, pesa zako ni za kwake pia, mmekua kitu kimoja na ni mrithi wa kila ulicho nacho ulieunganishwa nae na mwenyezi Mungu,
  17. Usifichue madhaifu yake, utakua unajifichua na wewe mlinde,
  18. Waheshimu wazazi wake na kuwa na moyo wa upole kwa ndugu zake,
  19. Usiache kumuambia ni jinsi gani unampenda kila siku ya maisha yake, mwanamke hachoki kusikia hilo na hatachoka kamwe,


    Mwanaume kua katika njia ya mwenyezi Mungu, ndicho kitu kitakacho kufanya uwe mume bora na mwenye hofu ya Mungu.

cc: Miss Natafuta
 
fanya yote hayo ila usijiaminishe kuwa hutosalitiwa
 
Weka na “enyi wanawake mlio ndoani au mnaotarajia kuolewa”
Wengi hawajui wajibu wao.
Ata wanaume yunahitaji matunzo zaidi
 
Usiwaweke ndugu zako kabla yake, yeye ni mke wako ndiye anaekaa na wew, lazma umpe kipaombele kabla ya ndugu zako,

Kivipi...yeye c tumekutana ukubwani?
Mbona wao wanaweka ndugu zao mbele?
Ukizingatia hii utaumia sanaaa!!
 
tatizo LA wanawake wengi hawajielewagi.Ndio maana wanapewa mimba tu na kuachwa.
 
Back
Top Bottom