Enyi Wanasiasa 'mnapoichokoza' Dodoma kisha 'kisirisiri' kutaka 'kukimbilia' Berlin au Brussels na Nairobi huwa mnatarajia nini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,533
2,000
Na 'Uchungu' zaidi unakuja pale ambapo GENTAMYCINE naweza Kuingia Kenya kwa njia za Panya na nikakaa huko bila 'Kukamatwa' lakini wengine 24/7 huwa 'wanatuaminisha' kuwa ni Wanasiasa 'Wajanja' lakini wakiingia mitaa ya 'Kaijia Dodo' wanakamatwa kama 'Kuku' na kurudishwa walikokumbilia baada ya Kukuchokoza.

Bora ya hata Wanasiasa wengine wao 'wakiichokoza' tu Dodoma wana uhakika wa Kupokelewa na hata Kulala Ofisi za Kuhifadhia 'Pasipoti' za kwenda Jiji la Berlin na kutokea hapo Berlin basi uwezekano wa kwenda Jijini Brussels unakuwa rahisi. Ila Watu wa Dodoma wanajua kweli 'Kuwanyoosha' wanaotaka kusafiri 'Kiuwoga' kwenda Berlin na Nairobi au hata 'Kaijia Dodo' tu hapo.
 

std7

JF-Expert Member
May 6, 2011
695
1,000
Kuna mambo yanayotokea kwenye nchi yetu tunayadharau na kusema hayatuhusu. Azori katoweka hayatuhusu, Lissu kapigwa risasi hayatuhusu, Lema kakimbilia kenya hayatuhusu, matokeo ya uchaguzi yana utata hayatuhusu, uhuru wa vyombo vya habari umeminywa hayatuhusu, mwishoni itakuwa kama ile hadithi ya panya.

Ng'ombe na mbuzi wanachinjwa kisa walidharau taharifa ya panya kuwa kuna nyoka aliyeko uvunguni mwa kitanda.

Kinapokuja kibano kinatuhusu wote bila kujali chama, dini, kabila mf kufungiwa intanet ilituhusu wote.
 

Ryaro wa Ryaro1233

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
353
1,000
Uchaguzi Umeisha, tuombane misamaha, tuijenge nchi usiwe muda wa kuwindana tena. Aliyeshinda ajenge upendo na vile vile walioshindwa watulie maisha yanaendelea regardless na nature ya ushindi...Tusiwindane hii italeta shida tukiona kwa sasa ni nzuri..
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,733
2,000
Na 'Uchungu' zaidi unakuja pale ambapo GENTAMYCINE naweza Kuingia Kenya kwa njia za Panya na nikakaa huko bila 'Kukamatwa' lakini wengine 24/7 huwa 'wanatuaminisha' kuwa ni Wanasiasa 'Wajanja' lakini wakiingia mitaa ya 'Kaijia Dodo'...
Siku yakukute ndio utajua kuwa hujui lolote!

Siyo busara kushangilia madhila na manyanyaso ya jirani au ndugu yako kwani siku yakikufika utajuta!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom