Enterprises yaunganishwa orodha ya wadaiwa sugu kodi ya ardhi

Super Don

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,978
1,781
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na manispaa za Jiji la Dar e s Salaam imetoa notisi kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi, ambao ni pamoja na Kampuni ya Mohammed Enterprises.

Kampuni ya Mohammed Enterprises inatajwa kudaiwa shilingi milioni 73 na imewekwa katika kundi moja la wadaiwa sugu

Hayo yamebainika leo, Februari 3, 2017 wakati wizara ikiwa katika mwanzo wa oparesheni maalumu ya kukusanya kodi ya pango la ardhi kutoka kwa wadaiwa sugu iwe ni kampuni, mashirika ya kiserikali na watu binafsi.
Kampuni hiyo imepewa notisi ya siku 14 kulipa kodi hizo wanazodaiwa na endapo hawatalipa watafutiwa umiliki au mali zao kupigwa mnada ili kufidia gharama madeni hayo.

Operesheni hiyo imeanza kutekelezwa kwa mtindo wa aina yake ambapo wahusika hufuatwa kwenye ofisi zao. Operesheni hiyo inaendeshwa kwa kushirikisha kampuni ya udalali ya Msolopa Investment.
 
Back
Top Bottom