Energy drinks

Hivi hizi energy drinks za Mo na Azam zina nini!? Nisipozinywa nashinda kama nimechoka choka siku nzima, ila nikinywa tu nachangamka vizuri.
Umeshakua addicted tayari , punguza taratibu kutumia hayo madude, yana madhara kiafya , itafika kipindi huwezi Fanya chochote bila kutumia hizo energy drinks
Pia kuna Jamaa yangu alikua anapenda kutumia hizo vitu sasa hivi yupo anatafuta matibabu ya moyo , sio mazuri hayo achana nayo
 
Kwa maelezo yako mafupi inaonekana mwili wako umeshazizoea tayari japo si nzuri kwa kunywa kila siku.
Hizi energy zina kiungo cha kahawa ambacho ndicho kinakufanya uchangamke pale unapokunywa.
Kahawa iliyo ndani ya energy moja inaweza kukata usingizi hata kama ulikuwa na uchovu mwingi! Ni hatari sababu kipindi zimetoka tu nilidhani ni redbull nikawa nakunywa hadi tatu kwa siku ila kilichotokea baada ya miezi michache nikajikuta kuna wakati natetemeka kama mzee.
 
Hivi hizi energy drinks za Mo na Azam zina nini!? Nisipozinywa nashinda kama nimechoka choka siku nzima, ila nikinywa tu nachangamka vizuri.
Nmeona mateja pale mwananyamala wanaipenda sana na madereva boda boda cjajua ina kitu gani haswa kwa kweli
 
Kwa maelezo yako mafupi inaonekana mwili wako umeshazizoea tayari japo si nzuri kwa kunywa kila siku.
Hizi energy zina kiungo cha kahawa ambacho ndicho kinakufanya uchangamke pale unapokunywa.
Kahawa iliyo ndani ya energy moja inaweza kukata usingizi hata kama ulikuwa na uchovu mwingi! Ni hatari sababu kipindi zimetoka tu nilidhani ni redbull nikawa nakunywa hadi tatu kwa siku ila kilichotokea baada ya miezi michache nikajikuta kuna wakati natetemeka kama mzee.
Umepima Ngwengwe?
 
Hiyo Hali ya kutetemeka Ni dalili (advanced) ya ngwengwe

Mimi sitetemeki sasa, naamka nikiwa nimechoka na nisipokunywa hizo energy drinks kama mbili tatu+ fanta orange moja sijisikii poa kabisa, ila nikinywa nachangamka kabisa
 
Mimi nimekua addicted kabisa siweza kukaa na Jua hili la dar bila kunywa na siku nikisema leo sinywi najikuta naamka hata saa 5 usiku naanza kuzitafuta madukani kuna kipind nilienda kijiji kimoja hazikuwepo nilikaa kama week 3 bila kinywa

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Acha kutumia.

Fanya kujifunza kuacha usiwe tegemezi(Addicted).

Energy Drinks zina kiasi kikubwa cha caffeine ambacho kwenye mishipa ya fahamu ufanya kazi ya kuchangamsha akili na kuhisi mwili kuchangamka.
Mara oooh "Usinywe nusu saa kabla hujaenda kulala"

"Usinywe zaidi ya chupa 1 kwa siku"

"Marufuku kutumiwa na Ke mjamzito au Ke aliyejifungua"

Sasa hapo si ni sumu juu ya sumu tu au kuna kipi kingine kinachohitaji ushauri zaidi ya kuacha tu kuyanywa?

Sent from my ONEPLUS A3010 using JamiiForums mobile app
 
Hivi hizi energy drinks za Mo na Azam zina nini!? Nisipozinywa nashinda kama nimechoka choka siku nzima, ila nikinywa tu nachangamka vizuri.

Umeshakuwa teja mkuu unahitaji rehab,.ndiyo maana huwa nashauri uspendelee kunywa kinywaji aina moja wakati wote.mfano kuna mtu anapenda pepsi au coca kiasi akinywa soda nyingine hamu haishi.ukiona hivyo ujue tayari umeshakuwa teja
 
Back
Top Bottom