Una mtaji wa kiasi gani? Vinywaji na Vyakula vinauzika eneo lolote kwa kuwa kila mahali kuna wanywaji na walaji. Biashara ya Baa siku hizi kwa wenye kauwezo wanaziboresha kidigitali zaidi kwa kuweka muonekano mzuri, vitendea kazi vya kisasa na huduma VIP ili kuweza kuvutia zaidi, mfano unaweza kukodi au kununua nyumba kisha ukafanya ukarabati na maboresho na kuwewa eneo la jiko, kaunta ya nje eneo la kukaa watu nje na ukatenga space ya kuweka VIP Lounge au Night Club ya kisasa, kwa maeneo mengi ya Sinza na Kinondoni siku hizi kuna Baa za aina hii jaribu kutembelea uone. Ndo maana nikakuuliza una mtaji wa kiasi gani ili tujue namna ya kukushauri pa kutafuta eneo na mambo mengine. Biashara ya Baa ni JIKO ZURI, HUDUMA NZURI, MANDHARI NZURI na UONGOZI BORA mengine ni ziada.