Endapo UKAWA wakishinda October, wataunda Serikali ya mseto?

Endapo UKAWA wakishinda October, wataunda Serikali ya mseto?

ukawa yenyewe ni mseto sasa sijui unauliza nini mkuu
 
Nawaza tu kwa mfano Lowassa ndiyo anashinda uchaguzi. Haya sasa kwenye kuunda serikali Chadema itapata wapi watu. Kuna mawaziri, manaibu, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wakuu, wakurugenzi, makatibu tawala, wakuu wa taasisi. Hao watu watatoka wapi jamani? Chadema yenyewe naona watu walewale kila siku.
 
Nani kakwambia watendaji watastaafishwa?Kitakachotokea ni kubadili mindset watu wanaendelea kupiga mzigo mkuu
 
Kwahiyo Makonda naye ataendelea?

Wakuu wa wilaya na mikoa hao ni makada wa chama hata kama wanafanya kazi za serikali kwa hiyo lazima waondoke na chama chao.
Watendaji wengine ni watumishi wa umma wanachapa kazi tuu tena kwa ufanisi zaidi.
 
INNOCENT CHACHA mura acha kifikiria utendaji wa serikali ya CHADEMA/UKAWA kwa akili ya KICCM.

Nia ya ukawa ni kubadirisha mfumo mzima wa kuongoza nchi; rejea Katiba ya CHADEMA.

Lakini hata kama UKAWA wakiamua kutumia mfumo huu uliopo wa kuongoza nchi tafuta ile picha ya mkutano mkuu wa CHADEMA tarehe 04/08/2015 ndo utajua kama wana watu wa kuongoza nchi au la!!
 
Back
Top Bottom