Encipher Inye: Tablet ya Afrika

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159

​


Mnigeria Saheed Adepoju, mwanzilishi na CEO wa kampuni ya Encipher Group anatekeleza ndoto ya kuinyanyua Afrika katika Teknolojia kwa kuzalisha kompyuta aina ya tablet, tablet hiyo si miongoni mwa tablet ambazo zinaweza kushindana na iPad, Nexus au Galaxy Tab lakini ni tablet iliyobuniwa Afrika na kutengenezwa na Waafrika, katika kundi (batch) la mwanzo la uzalishaji kampuni ya Encipher Group imezalisha na kuuza Inye 100, sasa Kampuni hiyo inalenga kutoa tablet yao ya toleo la pili ambayo tayari wameishaitangaza.


Inye ina maana ya namba moja kuwa lugha ya kienyeji huko Nigeria inayojulikana kama Igala. Tablet hiyo ya Android ina disk ya ukubwa wa 16GB na RAM 512mb, pia ina betri yenye 2600 mAh. Vile vile Encipher Inye ina Wi Fi na 3G, na mambo yote ya msingi ambayo yanatarajiwa kwenye tablet yoyote ile kama vile sehemu ya kuwekea kadi aina ya MicroSD, tundu ya headphone na spika.

Kwa specs za tablet mpya ya Encipher Inye 2, fuata link ya chini usome makala hii kwa ukamilifu:
Gajetek - Gajet na Teknolojia: Encipher Inye Tablet ya Afrika
 
Wazungu wanatumia kigezo cha uafrika kuzolea soko tu, hapo hamna cha tablet ya afrika wala nini, hawa wazungu wametugeuza kuwa matahira sasa
 
Wazungu wanatumia kigezo cha uafrika kuzolea soko tu, hapo hamna cha tablet ya afrika wala nini, hawa wazungu wametugeuza kuwa matahira sasa

kuna kampuni ya kichina jina meisahau inatengeneza hizo tablet then unaeka logo yako. Unatoa order labda nataka tablet 1000 then unapewa. Zipo nyingi tu hizo tablet ndo zile zile za jamaa wa congo.

Watu ukiwaambia hawaamini ngoja nkipata zali la kwenda china ntarudi na tablet inaitwa jamiiforum ndo watu wataamini
 
Fuatilia kwenye Mtandao story ya kampunimya Incipher Group. Hii ni tofauti.
 
Wazungu wanatumia kigezo cha uafrika kuzolea soko tu, hapo hamna cha tablet ya afrika wala nini, hawa wazungu wametugeuza kuwa matahira sasa

Incipher sio kampuni ya Wazungu, inamilikiwa na Mnigeria na inafanya uzalishaji Nigeria. CEO wake anaitwa Saheed Adepoju.
 
Inakua ngumu kuamini. Inye?
Duh!
Kama kweli then big up sana kwa Nigeria



Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
mkuu hawa ni wale wale inye na tushawaongelea sana humu na wenyewe hawafichi hii tablet inaitwa inye 2
 
Incipher sio kampuni ya Wazungu, inamilikiwa na Mnigeria na inafanya uzalishaji Nigeria. CEO wake anaitwa Saheed Adepoju.
Mkuu hata usemeje hiki kichwa changu hutakaa ukiaminishe kwa sentensi rahisi kama hii. Kukua kwa tekinolojia kumesababisha ushindani mkubwa sana kwa vifaa vya electronics hasa kwa wenzetu huko ughaibuni, wingi wa vifaa hivi na ubora wake umesababisha baadhi ya kampuni kutopata wateja wa vifaa hivyo na kusababisha kuvibatiza majina yanayovutia wateja hasa sehemu ambapo tekinolojia ni ndogo ili nao wajione wana kitu cha kujivunia na kutoa ushawishi wa kununuliwa kwa wingi vifaa hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…