Wana JF,
Kwa mujibu wa habari tulizopata muda huu, ni kuwa hatimaye Mh. Emmanuel Nchimbi amefanikiwa kumaliza PHD yake aliyoianza mwaka 2004.
Katika PHD hiyo ambayo alikuwa akifanya utafiti wa uhusiano wa umasikini na mikopo midogo midogo katika mazingira ya wajasiliamali wa Tanzania wanaoukutana na vikwazo kadha wa kadha kama vile umeme, kushuka kwa thamani ya shilling, mzunguko mdogo wa hela na nguvu ya soko ya nje wanavyoweza kutoka kwenye lindi hioli la umasikini.
PHD paper yake ilipelekwa na kusahihishwa taasisi ya Development Studies ya UDSM kama external na walimpa alama ya A nilivyoambiwa.
Nakaribisha maoni yenu kama ifuatavyo: -
1. Mzumbe haina status,
2. Kaandikiwa ni kilaza,
3. Anajisafisha baada ya kuona anaandamwa,
4. Tuletewe tuipitie hapo jamvini (anaedai tena ni std 7),
5. Hatuitambui kabisa,
6. Huu ni uzushi,
7. Hata masters hana mbona,
8. Ni ya kisiasa hiyo,
9. Mimi hata sisomi hii thread
11. Huyu alietuma ni mpuuzi, mjinga, analeta utoto hapa,
12. Nae anataka urais,
13. Kumbe ni rahisi sana,
14. Tupe source ya taarifa,
15. Lini alipata muda wa kufanya huo utafiti,
16. Kapendelewa na walimu wa mzumbe na udsm pia
17. Nimeambiwa utafiti wenyewe ni shallow sana,
18. Mwalimu mmoja wa mzumbe kaniambia kuwa wameamua kumwachia tu,
19. Shule za bongo ni za ajabu kweli hivi mzumbe wanaweza kutoa PHD kweli,Mzumbe walimu wote wana PHD fake likewise na wanafunzi pia,
20. Nampongeza kama ni kweli.
Graduation itakuwa mwanzoni mwa December. Kama una maoni yafananayo na naapo juu yani namba 1-20 , changia kwa kuweka namba inayowiana namchango wako tu inatosha kama ni tofauti basi karibu.