EMINEM na STAN wake

EMINEM na STAN wake

Kwanza niweke wazi kabisa, EMINEM ndiye mwanamuziki wa HIP HOP ninayemkubali kuliko mwanamuziki mwingine yeyote wa HIP HOP, yaani ninamkubali kiasi kwamba nikiona "list" yoyote inayohusu wanamuziki watatu (3) bora tangu muziki wa HIPHOP upate kuanzishwa, kwangu mimi hiyo "list" inakuwa ni batili kama jina la mkali EMINEM halipo katika hiyo "list". Naam kwangu mimi EMINEM ndio msanii bora kuwahi kutokea kwenye "game" ya HIP HOP (Mnisamehe sana mashabiki wa TUPAC na BIG, maana ni wazi kuwa nitakuwa nimewakera mno).
View attachment 1075251

Haya, niwarudishe kwenye lengo la "thread". Leo nikiwa natazama video mbalimbali za muziki nikakutana na video ya STAN kutoka kwa mkali wangu EMINEM akimshirikisha mwanamama DIDO kutoka Uingereza. Wimbo huu unamzungumzia mshikaji mmoja anayefahamika kama STAN (Stanley), huyo jamaa anamkubali vibaya mno msanii EMINEN, anamkubali EMINEM kiasi kwamba ilifikia hatua akawa anagombana na mke wake, jamaa alifikia hadi kubadilisha muonekano wake ili aweze kufanana na EMINEM.
Sehemu ya Video inaonesha STAN akimuandikia barua EMINEM kulalamika jinsi alivyokua akimpuuzia, STAN alikuwa anajitahidi kuhudhuria show za EMINEM ili EMINEM atambue jinsi anavyomkubali, juhudi za STAN ziligonga mwamba,kwasababu EMINEM hakuonesha kujali kabisa.
Baada ya kumaliza kuandika barua hiyo STAN anaamua kumchukua mke wake ambae alikua mjamzito na kumuingiza kwenye buti ya gari, kisha anaendesha gari mpaka darajani kisha analiingiza gari kwenye mto, hivyo kutokana kutoonesha kujali kwa EMINEM, STAN anaamua kujiua yeye pamoja na mke wake mjamzito, inashangaza eeenhe?
Kwangu mimi hii ndio video bora kuliko zote kutoka kwa mkali EMINEM.

Kutokana na huu wimbo neno "Stan" limeingizwa kwenye kamusi za lugha ya KIINGERZA likiwa na maana kama "USHABIKI ULIOPITILIZA KWA MTU MASHUHURI/MAARUFU"



Kwa wale mnaomkubali EMINEM kama mimi, taja wimbo unaokubamba kutoka kwa mkali huyu.

100%
 
Yupo poa...

Karibia nyimbo zote za Eminem ni nzuri...

Love the way you lie (ft Rihana)
Without me
Not Afraid
Killshot
Mockingbird
When am gone
My name is
Superman
Just loose it
Like Toy Soldiers (My favourite)
The way i am
Ass like that
Shake that ass
Remember me
Cleaning out my closet
8 miles
Stan
Kiss my ass (*** you too)



Cc: mahondaw
 
Asante sana chief,alafu nilikua sijui kama ugomvi wa Stan na mke wake ilikua pia ni sehemu ya Stan kumuiga Eminem..!
Hakika Stan alikua mwehu..!
Ila mkongwe,mashabiki aina ya Stan wapo kweli..?
Tupo asee,mm ni stan wa soka,namkubali sana rooney,ad nkaanzisha mahusiano na binti wa watu tukiwa machalii ili baadae tukitoboa tuwe tuna ka hstoria tumetoka mbali km WR10 na mkewe,ah ah ah hadi sasa mambo yako poa,rooney nimebaki alone,coleen wangu kaolewa na niliemkuzia
 
Yupo poa...
Karibia nyimbo zote za Eminem ni nzuri...
Love the way you lie (ft Rihana)
Without me
Not Afraid
Killshot
Mockingbird
When am gone
My name is
Superman
Just loose it
Like Toy Soldiers (My favourite)
The way i am
Ass like that
Shake that ass
Remember me
Cleaning out my closet
8 miles
Stan
Kiss my ass (**** you too)
Cc: mahondaw
Umetisha mzazi...
Nilivyoiona hiyo ngoma ya "My name is" ndio nimeamini kuwa unamfuatilia vyema huyu fundi wa michano...
 
Kwan hiyo Stan ni story ya kweli?
Mi nilimkubali zaid jamaa kwenye ile nyimbo yupo na jay z ya kuitwa Renegade,,
Beat tamu sana ile
Dah

Me ndo maana nimeshindwa kuweka list

Ntaweka upi niache upi? Renegade never being afraid to say abt anything

Nakumbuka nimebishana sana na wana Juu ya nan alimfunika mwenzie
 
Umetisha mzazi...
Nilivyoiona hiyo ngoma ya "My name is" ndio nimeamini kuwa unamfuatilia vyema huyu fundi wa michano...

Huyu jamaa najikutaga nanunua album zake kama...

1) Infinite ya 1996
2) The Slim Shady LP ya 1999
3) The Marshal Mothers LP ya 2000
4) The Eminem show ya 2002
5) Encore 2004
6) Straight from the vault ya 2011
7) The Marshal Mothers LP2 ya 2013

Zingine sikufanikiwa kununua... Album number 3 na 4 ni zilifunika mbaya...

Cc: mahondaw
 
Dah

Me ndo maana nimeshindwa kuweka list

Ntaweka upi niache upi? Renegade never being afraid to say abt anything

Nakumbuka nimebishana sana na wana Juu ya nan alimfunika mwenzie
Jay z aliachwa mbali sana hata jay mwenyew analijua hilo
 
Back
Top Bottom