GE2025 Emil Magige Nyerere achukua fomu ya ubunge jimbo la Kawe

GE2025 Emil Magige Nyerere achukua fomu ya ubunge jimbo la Kawe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Gagnija

Platinum Member
Joined
Apr 28, 2006
Posts
13,388
Reaction score
13,793
Mtoto wa baba wa taifa Emil Magige amechukua fomu ya kuomba kugombea ubunge jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM.

Emil, mhandisi kwa taaluma aliwahi kuwa mwenyekiti wa ccm Musoma vijijini miaka ya nyuma.
 
Emil Magige,mtoto wa tatu wa Mwalimu Nyerere amechukua na kurudisha fomu ya ubunge jana.

Magige ameniambia anataka kuwa mbunge wa Kawe.

Hili ndilo Jimbo la Gwajima.
Kawe naunga mkono tumpe tuu Magige kwa kumuenzi tuu Baba yake Mwalimu Nyerere!, kama Amani alivyopewa kumuenzi Abedi, Dr. Hussein kumuenzi, Ali Hassan, Riz1 kmuenzi Jakaya, lakini ni kweli kwenye miti mara nyingi huwa hakuna wajenzi!, Mwalimu hana mtoto hata mmoja wa kuvaa viatu vyake, vikamfiti na ukimuondoa msanii Brother Mako, hakuna mtoto mweingine yoyote wa Mwalimu ni mwanasiasa!, hata hao watoto wa wanasiasa, wengi sio wanasiasa bali wanabebwa na majina ya ubini!.

P
 
Kawe naunga mkono tumpe Magige kwa kumuenzi tuu Mwalimu!, lakini ni kweli kwenye miti hakuna wajenzi, Mwalimu hana mtoto hata mmoja wa kuvaa viatu vyake, na ukimuondoa msanii Brother Mako, hakuna mtoto mweingine yoyote wa Mwalimu ni mwanasiasa!.

P
What's your point! Hakuna mtoto wa mwalimu wa kufikia viwango vya intellect ya kina Samia!

I know you're not serious
 
Pascal ana delusions of grandeur. Anataka kushindana na Madame Spika.

Einstein alikuwa anaongea kuhusu Unified Field Theory.
Kwa nini hapa tunashindwa kusema kitu definitive.

Kwamba Uchaguzi itakuwa hivi na hivi,na hawa Chadema labda watashiriki au labda hawatashiriki.
 
Kawe naunga mkono tumpe Magige kwa kumuenzi tuu Mwalimu!, lakini ni kweli kwenye miti hakuna wajenzi, Mwalimu hana mtoto hata mmoja wa kuvaa viatu vyake, na ukimuondoa msanii Brother Mako, hakuna mtoto mweingine yoyote wa Mwalimu ni mwanasiasa!.

P
Na wasiwasi na upeo wako, yaani unachagua kiongozi kwa kigezo cha kuenzi mema ya baba yake? Vipi endapo yupo mwingine mwenye uwezo na maono zaidi yake?
 
Siyo mlevi kama wale ndugu zake?
 
Siyo mlevi kama wale ndugu zake?
Hatumii kilevi. Baba yake akiwa rais, yeye alikuwa meneja wa karakana ya Kijiji cha Butiama.

Kaishi maisha ya ujana wake na utu uzima kijijini Butiama hadi Butiama ilipopewa hadhi ya mji wa makao makuu ya wilaya.
 
Kawe naunga mkono tumpe Magige kwa kumuenzi tuu Mwalimu!, lakini ni kweli kwenye miti hakuna wajenzi, Mwalimu hana mtoto hata mmoja wa kuvaa viatu vyake, na ukimuondoa msanii Brother Mako, hakuna mtoto mweingine yoyote wa Mwalimu ni mwanasiasa!.

P

Braza kwani ni lazima kuvaa viatu vya mwalimu?

Je, kwenye siasa za Tanzania hadi leo hii kuna mwanasiasa yeyote aliyeweza kuvaa viatu vya mwalimu?
 
Back
Top Bottom