Email yangu wanaipataje?

Email yangu wanaipataje?

Ozzie

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2007
Posts
3,217
Reaction score
1,274
Nina private emails kadhaa, ambazo zinatumia majina yangu binafsi ambazo haziko katika mfumo wa yahoo.com au gmail.com (katika mfumo wa Ozzie.com). Kwa muda mrefu nimekuwa nikipata emails zenye matangazo toka kwa kampuni au watu ambao sitarajii wawe na contacts zangu. Watu wanaonitumia sana emails zenye matangazo ni kama Engen Ubungo, Winglink Travel Limited, Petsville, Jumbo Travel, Excel Management, Budget Electronics na wengine ambao wote wako Tanzania. Emails zangu ninawasiliana na watu walioko nje ya bara la Africa, sikumbuki kama nimeshawahi wasiliana na mtu yeyote, ndani ya nchi yetu. Mawasiliano yote kupitia hii email ninatumia internet ya Airtel. Pia sija zi list au kuzi register mahala popote kwenye mitandao. Sasa najiuliza wanaogawa emails zangu kwa watu wa namna hii ni watumishi wa ISP (hapa Airtel) au nani? Ninaboreka sana.
 
Back
Top Bottom