Elimu yetu inaenda wapi?

GedsellianTz

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
1,348
1,803
Siku hizi kuna vyuo vingi sana Tanzania na kuna wa wanavyuo wengi sana Tanzania ila tatizo lipo kwenye fikra na matendo ya wanavyuo sababu kuna wanavyuo wengi wajuaji na idadi ndogo ya wana vyuo waerevu.

Wanavyuo wengi wamesoma ila wengi hawajaelimika , wanavyuo wengi wanapenda kusoma ila masomo hayawapendi na ndio maana kwa sasa vyuoni kuna wasagaji,mashoga ,Team Diamond,Team KIba ,Team Wema Sepetu na wote ni wanavyuo.

Ni kazi rahisi sana kupata degree siku hizi ila ni kazi ngumu sana kuitetea degree yako kwa utashi wa fikra,ubora wa matendo na nidhamu ya kuzungumza kwa jamii husika na kwa watu wanao kuzunguka ,sasa hivi vyuoni kuna a.k.a nyingi kuliko mtaani.

Ningekuwa Hr ningetengeneza mfumo wa kushort list watu wote wanaomba ajira kisha na kuwaomba wanipe majina yao ambayo wanatumia kwenye social networks zote kuanzia ,Instagram,Twitter na Facebook ili kuweza jua ubora wa maarifa na utashi wao.

Mwanachuo anafukuzwa Tution fees ya 350,000/- anarudi nyumbani kumuomba mama/baba yake pesa ya Tution fees wakati yeye ana simu yenye thamani ya Tsh 1,500,000/- hapa ndio utajua degree wakati mwingine haina thamani .

Mwanachuo anayewasaida wazazi wake majukumu ya kujisomesha huwa na baraka mara 10 kwa Mungu na wazazi wake kuliko yule bingwa wa kuhonga wanawake na kununulia smart phone kwa pesa za wazazi wake ,ni vyema ukajijenga kwa fikra na kujitegemea hata kama wazazi wako wana uwezo.

Usijiite mwana chuo kama una bikira ya mawazo na ushamba wa fikra sababu unawazalilisha wanachuo wanao jitambua na wenye upeo mkubwa . What we become depends on what we read after all of the professors have finished with us. The greatest university of all is a collection of books .#TeamConscious
 
Mi huwa sion kazi ya TCU kabsa...alafu kuna elfu ishirin huwa wanakata wanafunz kila mwaka..cjui za nin...siku hizi GPA hazizingatii uwezo wako...cku hiz kupata 5 ni easy tu
 
Kwanza ata mitaala yenyewe ya vyuo haieleweki... Yaan watu wanasoma course moja..vyuo viwil tofaut af wanakuwa na mitaala tofaut kabsa...inatakiwa waandae basic things ambazo kila mwanafunz wa koz husika anatakiwa ajue kabla ya kuwaachia wamiliki kuunda yao
 
Ni kweli mkuu,Gedsellian Tz!!

Tatizo la elimu yetu nadhani ni katika msingi wa kumjenga mtu kifikira.Laiti kama tungekuwa tunajengwa katika mfumo wa kufikiri,kuhoji,kusaili,kudodosa nk tungekuwa tunafikiri vyema na kuondokana na huu u-bikira wa mawazo kama ulivyousema hapo juu ila tatizo sasa ni huu mfumo Uchwara wa kukaririshwa mambo.
Jaribu kuwatizama waalimu wetu wanavyofundisha,wanavyovaa,wanavyotembea,wanavyowaza nk.Utakuja kugundua mwisho wa siku kuwa kitakachozaliwa (Mwanafunzi) naye atakuwa kama mwalimu wake alivyo.Wanaoitwa wasomi leo hii ndio hawa ambao muda wote wako katika mapozi ya kupiga picha almaarufu (Selfie),Wanavaa nguo zinazoachia sehemu zao kubwa za miili wazi,Wananyoa viduku,wanaume wanavaa nguo zinazowabana nk,Sasa mwisho wa siku unakuja kujiuliza kama ifuatavyo-
>Huyu msomi,kavaa nusu uchi na kajipaka uchafu mdomoni pamoja na mikucha mirefu.
>Huyu mbumbumbu mzungu wa reli kama mimi,kavaa suruali inambana yaani hadi kuvua lazima kwanza ajilowanishe.
>Huyu mwingine kavaa suruali katikati ya makalio na simu kuubwa utadhani anafanya kazi Barclays

Waweke hawa pamoja halafu jiulize wanawaza nini vichwani mwao?,Mimi nadhani tutengeneze mazingira kwanza ya kumjenga mtu kifikra,Kuanzia Mama na Baba nyumbani,Dada na kaka,Mwanafunzi na mwalimu shuleni nk ambapo ni pamoja na kuwa na nidhamu nzuri,kuvaa vizuri,kuzungumza kwa ufasaha na utashi,kusali/kuswali katika kweli pamoja na UTAMADUNI WA KUSOMA VITABU mbalimbali vya kifasihi,Kitaaluma,kiafya,kielimu,kitamaduni,kisiasa,kiimani nk na tukishafaulu hapa ndipo matokeo ya mtu kuwaza vyema kutakapofuata baadaye.
Mkusanyiko wa maudhui yapatikanayo katika vitabu vya kifasihi kama Tamthilia,Riwaya pamoja na ushairi vinauwezo mkubwa sana wa kumfanya mtu yeyote yule kuwaza katika namna bora na kuwa mtu mwenye kuhitajika katika jamii inayomzunguka.
Nathubutu kusema kuwa kwa kufanya hivi,tutazalisha Taifa la watu wa maana kuliko vilaza (kama Rais wetu anavyowaita).

Ahsante.
 
Elimu iliyopo ni ya magumashi ndio maana unaona Sheria za ajabu ajabu zinapitishwa kwa kutokujua maana ya kitu mfano mdogo watunga sheria hawajui maana ya VAT(Value Added Taxation) nani wakuchajiwa hiyo kodi hakuna anaejua toka ilipoanzishwa 2005...Vat ilipwa kwa bidhaa zinazotoka nje ya Nchi au Transit?
 
Back
Top Bottom