Elimu yetu haisadii chochote ni masifa tu ya kuvaa majoho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu yetu haisadii chochote ni masifa tu ya kuvaa majoho

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Nakei, Oct 26, 2011.

 1. N

  Nakei Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wasomi wanatakiwa wawe wavumbuzi na wajenzi wa uchumi, kwa mfano ukisoma jinsi ndege ilivyovumbuliwa utashangaa, ilianza mwaka 1799-1913. Kila mvumbuzi alikuwa anajitahidi kufanya kitu, anakata tamaa lakini anaacha kijitabu cha theory zake. Kufikia mwaka 1913 wright brothers walipitia vitabu vyote na matokeo yake ni mafanikio ya binadamu kutumia usafiri wa anga. Elimu ya vitendo ndio matokea ya wenzetu kupiga hatua katika nyanja mbalimbali, silaha za kisasa za kivita, vyanzo vya umeme, haya magari ya kifahari tunayotamba nayo, yote ni matokeo ya wasomi waliotumia elimu yao katika vitendo.

  Sisi watanzania hatuna cha kujivunia kwa hawa wasomi wetu wanaoringa kwa kuvaa majoho, hatuoni impact yoyote kwenye jamii kutokana na usomi wao. Kwa mfano mtu amesota hapo UDSM amepata hadi PhD, huyu mtu atatafuta wahisani(donors) atafanya research ambayo haina faida kwa nchi yake bali kwa hao wahisani(kuganga njaa), ni hawa hawa wasomi ndio wamedidimiza mashirika yetu(hawana uzalendo hata kidogo, wamejaa ujinga wakujipatia hela kwa hila na uwizi). Angalia taasisi za serikali watu wamejazana mle, hakuna anaeweza kumkemea mwenzake, kwenye akili zao kumejaa michongo michongo, kutunga safari kwa ajili ya kujipatia perdiem. Kwao kipimo cha mafanikio ni kupata hela za ujanja ujanja, kwenye nyuso zao kumejaa usanii mtupu, ukiwa na bidii ya kazi wataku kejeli na hata kukufanyia hila. Kwenye kundi la hawa watu huruhusiwi kuboresha. Utaambiwa hujafuata utaratibu, subiri kwanza hadi tufanye kikao, na kama hujafanyiwa hila basi utaonewa huruma kwa kufanya kazi kwa bidii, wajisemea aaah huyu mbona anajitesa hivi.


  Hii ndio Tanzania yetu.
   
 2. Chenge

  Chenge JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 1,077
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Pole sana! Elimu inatusaidia kuiba kwa kutumia kalamu
   
 3. k

  kajembe JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45

  Point yako ni nini sasa? Watu waache kusoma? au watafute vyuo vya ulaya ndiyo wasome? Mzee hebu conlude basi vizuri ujumbe wako,maana inaonesha kwamba Elimu haina maana huo ndio ujumbe wako? ujumbe wako sio mbaya lakini umeshindwa ku conlude vizuri
   
 4. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,996
  Likes Received: 2,651
  Trophy Points: 280
  Anapoint nzuri sana kwa mtu mwenye akili timamu,tumejaza wasomi wa kila aina lakini cha ajabu usomi huo hauna faida yoyote kwa Taifa letu,usomi wa tanzania ni wa kugangia njaa tu na kutishia watu pamoja na kupinga mambo ya msingi,kama ulivyo post hapo juu hatuna hata kitu kimoja cha kujivunia kutoka kwa wanaojiita wasomi,labda CHIPS MAYAI ndio tunajivunia maana ndicho tulichovumbua.
   
 5. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kama huja-disco wewe katika moja ya vyuo sijui! Huna tofauti na wanasiasa wa Tanzania ambao kila wanachokifanya ni rule of thumb tu that exist! No evidence-based decisions! Ur thread is replete of unfounded and baseless arguments, so to speak!
   
 6. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hata Matonya na vichaa wana akili..... binadamu ana akili na kichaa... sema degree ya akili na ukichaa ndo unatofautina! Hv umejiuliza USOMI ni nn? Nchi zote zilizoendelea they invest alot kwenye Research and Development, huko ndio chimbuko la kitu ktk maendeleo. Tofautisha vipawa vya kuzaliwa na USOMI. Tanzania ndio mwaka juzi au jana nlimsikia JK akisema budget ya R & D ndio imepandishwa angalau kukidhi tafiti katika maeneo ya maendeleo. Jiulize 50 years of independence unawekeza kwenye R & D mwaka jana! Sasa hapo tatizo liko kwa wasomi wetu au serikali na mfumo wake?

  FYI, nchi nyingi za Africa hususani SSA, maamuzi yao mengi ya kimaendeleo hayana research back up. Na kwa budget ndogo zinafanyika na hazifanyiwi kazi. Niambie ni maamuzi gani yaliyofanywa yaliyo na research back up? MKUKUTA? KILIMO KWANZA? Just mention one?
   
 7. N

  Nakei Member

  #7
  Oct 26, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wewe endelea na evidence based. Hoja tunayojenga hapa ni je elimu ya Tanzania inaleta impact yoyote kwenye uchumi wetu? Kuna nini kwenye akili za wasomi wa tz? je wanaganga njaa au ni wazalendo wa kweli. Taasisi nyingi za serikali zinaongozwa na wasomi waliobobea Je utendaji wao unaridhisha?. Usidhani kila anayewaza nje ya boksi ame disco huo ni ufinyu wa upeo.
   
 8. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Speak the truth and leave imediately bwana watu hawataki ukweli kabisa.Wasomi wa Tanzania angalau bank teller,nurses na walimu wametufundisha a,e,i,o,u. My name is devil etc wengine ni kula mpunga tu.JAMII ILIYO LALA!
   
 9. K

  KVM JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Kuna ukweli fulani katika ujumbe wako.

  Labda mimi niseme tu kuwa kusoma hakuwezi kumfanya mtu kuacha kabisa kuwa mwizi, mwongo, fidhuli, jeuri, mpuuzi, kama alikuwa na tabia hizo. Kuna wakati vitu hivyo huongezeka baada ya kusoma. Vilevile mazingira ambayo msomi anafanyia kazi yanaweza kumfanya aonekane kama hakusoma kabisa kwani atakuwa anakumbana na vikwazo vingi ambavyo vitamkatisha tamaa kabisa. Anaishia kuwa kama wengine wote.

  Mimi nadhani tunachokosa Tanzania ni misingi ya utawala bora hasa ile inayozingatia sheria za nchi. Waliotufikisha hapa tulipo ni wanasiasa, toka enzi za Mwalimu mpaka leo hii. Wanasiasa na wakuu wengine wa nchi wamekuwa ni sheria - wao hawaulizwi. Kufanya kazi katika mazingira ambayo kuna watu (wakubwa) wapo juu ya sheria ni ngumu sana, na nchi haitafika popote pale.

  Wasomi wa Tanzania wanafanya mambo makubwa wanapokuwa nchi za nje. Nenda Botswana uone miji na barabara zilivyopangwa. Kazi hiyo imefanywa na Watanzania waliosoma Diploma pale Ardhi Institute na UDSM. Wale waliobakia Tanzania wengi wao wamekuwa ni wezi na waongo wakubwa. Wnashindwa hata kuipa majina mitaa ya Sinza, Mbezi Beach na kwingine kwingi. Utafikiri hawajui kusoma wala kuandika. Tofauti ya Botswana na Tanzania ni utawala wa sheria. Botswana sheria inafuatwa sana sana. Hakuna ubabe au kutumia ukubwa na mabavu. Ni raha sana, kwa kila mtu kuishi kwenye nchi kama hiyo.

  Sote tupiganie kuwa na nchi ambayo inafuata utawala wa sheria. Kila mtu awe na haki mbele ya sheria, si mkubwa wala mdogo. Na hizo sheira siyo zitungwe tu bali zifuatwe. Bila hilo Tanzania haitapiga hatua ya kwenda mbele. Tusijidanganye kwenye hilo. Mpaka leo sielewi kwa nini mtu akiiba mabilioni ya pesa au kuliingizia taifa hasara kubwa anasifiwa au sana sana atafungwa miaka mitano tu.
   
 10. Engager

  Engager JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  vijisenti!! Are you??
   
 11. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #11
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hujaelewa point yake? basi we ni zuzu!
   
 12. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  inawezekana wakawa wanaganga njaa lakin hujiuliz tumefikaje hapa?
   
 13. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,131
  Likes Received: 3,320
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo tusisome..nchi iwe na mimbumbumbu..tatizo ni system ya serikali ambayo inaongozwa kifisadi na utawala mbovu.
   
Loading...