Elimu yako imekusaidia kwenye ndoa yako?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu yako imekusaidia kwenye ndoa yako??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jun 17, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,181
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  [h=3]Je, Utakubali?[/h]

  [​IMG]
  Fikiria wewe ni binti (au mzazi wa binti) ambaye unataka kuolewa na mwanaume ambaye hajasoma (illiterate) utakubali?

  Ni kweli elimu ni kitu kizuri hata hivyo elimu si kigezo cha upendo.
  Naamini kitu cha msingi kwa mahusiano yoyote ni upendo wa kweli, kujali, kufanana na kuelewana.
  Ukweli binafsi nitakubali kuolewa na mwanaume illiterate kwani inawezekana ana sababu za msingi za yeye kutokwenda shule na baada ya kuoana tunaweza kushauriana ajiendeleakimasomo.
  Joyce M.

  Ukweli nitaolewa na yule nimeamua na nimempenda na angalau awe ameelimika.
  Sidhani kama nitaweza kukubali ombi la mwanaume yeyote kunioa wakati hana elimu yoyote na hajaelimika, je itakuwaje kwa watoto tutakao wazaa? Je anaweza kupata kazi nzuri kwa ajili ya kuleta kipato cha familia huku hajasoma?
  Pia kwa kuwa mimi mwanamke nimesoma na yeye hajasoma maana yake hatufanani na kutokuwa na gap kubwa sana katika uelewa wa mambo kitu ambacho sikipendi.
  Margaret S.

  Nimeona mfano halisi wa dada ambaye alikuwa na elimu ya kidato cha sita na akaoewa na kaka mwendesha pikipiki ambaye alikuwa hana shule na hajaelimika kwa lolote.
  Baada ya dada kuolewa kilichofuata ni kulea mtoto mmoja baada ya mwingine hadi ndoto zake za kuwa lawyer zikafutika.
  Pia huyu mwanaume illiterate huwa hana shukurani kwa namna yule dada anavyojitahidi kuhakikisha anaanya kila analoweza familia iwe na mkate wa kila siku na kusomesha watoto.
  Sitakubali binti yangu ajiingize kwenye ujinga kama huo hata siku moja na pia nitajitahidi kuelimisha mabinti wasije ingia katika matatizo kama hayo.
  Mrs Christina B.


  Kama kuna upendo na kuna kufahamiana na kuelewana na kama ni kweli huyu mwanaume ana sifa ninazohitaji Ukweli nitakubali tuoane na nitaomba Mungu aniongoze.
  Julieth M.

  Kwangu kuwa illiterate si kizuizi hasa linapokuja suala la mahusiano pale tu kukiwa na kuelewana kati yangu mimi binti na huyo mwaname na kama ana sifa zile niahitaji. Najua kuna matatizo na watu watasema sana kwa kumkubali huyo kaka ambaye hana shule kabisa hata hivyo kama kuna kujitoa na kumuomba Mungu hakuna lisilowezekana.
  Esther L.

  Binafsi siwezi kujiingiza kwenye jaribu la kijinga kama hilo na kuona na mwanaume ambaye hajaenda shule.
  Anne K.
  Na Je, wewe msomaji ungekubali? Au unasemaje ?


   
 2. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,809
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  mke wangu ana masters leo nimemfumania na kaka yangu ambaye ni form 4 leaver.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,181
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Yesuuuuuuuuuuuuuu wangu samahani nilikuwanapita tu!!
  Kiikio mbora
   
 4. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,583
  Likes Received: 762
  Trophy Points: 280
  Aisee; kumbe it is serious! She was not worthy ur love! Achana naye; Mungu atakupa mke mwema. Tulia na you have done the best thing to share in here, we are here for you, don't drink or do anything u might regret later! Watu wengi humu watakusikiliza, share ur pain n kukuencourage. Loosing one stupid woman is not the end of the world, after all it is her loss, atajuta one of these days!
   
 5. k

  kisukari JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,562
  Likes Received: 798
  Trophy Points: 280
  ki ukweli nilidhani unatania,maana jf utani mwingi.pole sana,ipo siku maumivu uliokuwa nayo,yatapona.maana hapo ni kusambaratisha undugu.kuamua wote kuvunja amri ya 6 kwa mdogo wako.pole sana
   
 6. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,085
  Likes Received: 2,961
  Trophy Points: 280
  Unapogundua kuwa ulikuwa unaishi na nyoka ndani ni bora ukamshukuru Mungu!Utamtoa kisha kuishi kwa amani zaidi!
   
 7. Patty B

  Patty B Member

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Asili ya mtu huwa haifichiki hata siku moja...huyo si mtulivu hatakidogo na mlafi wa ngono..atakuletea matatizo hasa kugombana na ndugu zako, kama vipi we mpge chini uangalie mambo mengine..!
   
 8. M

  Maswa Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadua wa JF ni vizuri sana kutofautisha elimu na maisha ya kwaida ambayo watu tunaishi, kwa upande wangu naweza kusema elimu ni sehemu ndogo ambayo inamwezesha mtu kujitambua na kutambua mazingira anayokuwemo. Ndoa ni mfungamano wa watu wawili walioamua kuishi kwa mujibu wa sheria, tabia ya mtu inabakia pale pale isipokuwa inahitaji kubadilika ndiyo maana kuna masomo ya Ki-saikologia yanayohusu "Behavioural Changes" the only thing important in life that I could advice is Analyze the past, consider the present and visualise the future.
  Asanteni kwa somo...Ila tukumbuke pia kwamba vifo vingi vinavyotokea hasa kwa watu ambao wako kwenye ndoa %kubwa inatokana na matatizo ambayo yanatokana na aidha mme au mke kutokuelewana nani ya ndoa, kwa lugha nyepesi ni msongo unaosababishwa na mafarakano ndani ya ndoa. Zaidi hekima na uvumilivu utumike! Kama mtu ataweza kutumia huu msomo kwamba uvumilivu unalipa ataishi maisha mazuri ktk ndoa na hata na jamii yake inayomzunguka. ie. Passions Pays...........................................................................................................................................
   
 9. wahida

  wahida JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna watu wana elimu lakin is nothing, japo elimu n muhimu lakin haihusiani na ndoa ,wengi wao wankosa kujua nini wafanye , wako watu ambao mimi nimewaona kabisa,akina dada ana elimu ya degree tu ana somesha dodoma, a naolewa tu na kuachwa ,kama elimu ni kisaidizi cha ndoa mbona yeye ameshindwa, kwa hiyo usiangalie elimu angalia mtu tabia zake.na upendo wake that it,
   
 10. m

  muhanga JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  does love have anything to do with education level????? love doesnt ask why! na hapo ndio wengi tunakosea, kulinganisha penzi na kisomo. kila kimoja kina manufaa yake mahali pake, si kila mahali kisomo kinaweza kuwa na msaada sana. kwenye penzi hata watu ambao hawajui hata kushika kalamu tumeshuhudia wakiwa kwenye mapenzi mazito na wakaishi wakiwa wapenzi kwa muda mrefu bila kuwa na elimu. na tumeshuhudia ndoa nyingi sana za wanaojiita wasomi zikivunjika kwa muda mrupi sana, hii ni kwasababu wanachanganya mapenzi na elimu! na huyo mkeo mwenye masters ya hicho alichosomea, kampata kakako ana PhD katika mapenzi ndio maana umemfuma nae, yawezekana wewe katika fani ya mapenzi tungesema ndio kwanza umemaliza darasa la saba!
   
 11. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,564
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ndio imanisaidia, maisha nilivokuwa nayachukulia before sijasoma na sasa ni tofauti, napanga , nakuwa na malengo na namna ya ku achieve my goals, nimekuwa mwelewa kwenye mahusiano, sikurupukii vitu, nina budget vizuri pesa
   
Loading...