Elimu ya Veta kuunganishwa na Elimu ya Sekondari

Elimu ya Veta kuunganishwa na Elimu ya Sekondari

said rutemba

New Member
Joined
Jan 27, 2015
Posts
1
Reaction score
1
Nimejaribu kuwaza kwa sauti tu....

Elimu/ujuzi wa veta imekua ni elimu ambayo wengi wanaifata baada ya kuwa wamefanya vibaya kimasomo na mara nyingi baada ya kufeli elimu ya secondari au wengine baada ya kufeli kabisa ki maisha ndio linakua kimbilio la mwisho.

Kwa nini Elimu hii ( Ya Veta ) isiwekwe pamoja na Elimu ya Sekondari yaani mfano haya Madarasa yanayo jengwa mapya kwa nini yasiwekwe hata madarasa mawili ya elimu ya veta ili mtu anapo maliza kidato cha nne au sita anakua ana ujuzi tayari na hata kama elimu ya sekondari anakua hajafanya vizuri tayari ujuzi unakuwepo na anaweza endelea kujiajiri badala ya kwenda veta kuanza upya.
 
Kwa nchi yetu hii hili suala ni gumu sana kutekelezeka. Japo kisiasa wanaoliona ni rahisi na ndio maana wamekuja na maono ya ELIMU YA AMALI (ambayo ndio unayoisema hapa) lakini kiuhalisia ni ngumu sana.

Mi naona ni bora waongeze vyuo vya technical na VETA na waviwezesha karakana na mashine/zana za kufundishia kwa vitendo kuliko kijidanganya kwa kwa hii inayoitwa ELIMU YA AMALI.

Vyuo vya Veta na vya ufundi (Technical colleges) + FDC hazina karakana na vifaa vya kutosha kufundishia kwa vitendo na hzi karakana na vifaa ni bei ghali sana. Huko hatujamaliza wanaibuka maprofesa wanamshauri Rais kuja na AMALI. Hii nchi haina vipaumbele hasa kwenye suala la elimu kwa kweli kila mtu anaibuka na cha kwake.

Walionzisha vyuo vya ufundi (Techical schools/college+VETA + FDCs) sio kwamba hawakuona umuhimu wa ku-integrate haya mafunzo na elimu ya kawaida kwa kila mwanafunzi. Naamini walijua sana kuhusu hilo ila kwa sababu ya ugumu wake katika utekelezaji ndio wakaona ni borq waanzishe vyuo au shule special tu kwa ajili ya wale wenye mahitaji hayo.
 
Back
Top Bottom