Nilishawahi fuatilia kwa kipindi cha nyuma kidogo, mahitaji ilikuwa unatakiwa kudeposit kiasi fulani kwenye account yako ambayo wao watakuwa na uwezo wa kuifikia pia. Hii ni kuonesha kwamba utakapoanza kazi basi nao watakua salama na pesa yao,ambayo wewe utakuwa unaikusanya. Kila wiki utakuwa unapeleka report ya pesa ulizokusanya na kubanki kwenye akaunti ya bima husika kwa kuwasilisha slipu za benki kwa msimamizi wako watakayekuwa wamekupatia. Hayo ndo matakwa walikuwa wakiyahitaji BIMA.
Mahitaji yako binafsi ambayo unatakiwa kujiandaa nayo ni uwe na ofisi , meza na viti kwa ajili ya kuhudumia wateja bila kusahau komputa. Japo kwa kipindi kile nafuatilia mimi nilikuwa nimeahidiwa kupangingishiwa ofisi na BIMA husika na samani zake ,ambayo kwa sasa sijajua kama unaweza pewa vitu hivyo. Hayo ndiyo machache ninayoyafahamu