Smith Rowe
JF-Expert Member
- Sep 18, 2018
- 4,513
- 9,553
Wasalamu wana JF
Hivi hii nchi imekuja kuwaje tena
Mbona kila sekta hakuna ajira
Ngoja nirudi kwenye mada
Nina kaka yangu mmoja hivi ana gamba la masters ya Public Administration from Mzumbe university mwaka wa tatu kama sio wa nne huu toka amalize lakini hajawahi kubahatika kupata ajira kabisa.
Ame zunguka na bahasha ya kaki mkononi na amepigwa na jua vya kutosha, akaona ajiajiri lakini bado akatoka kapa biashara aiendi wala nini maji yakamfika shingoni.
Naona sahivi amerudisha majeshi nyumbani kweli Dar kugumu
Sasa juzi juzi hapa kaitwa kwenye interview moja lakini hiyo kazi daaah kwa akili ya kawaida tuu take home haizidi 350k
Nikiwa sijakaa sawa ndugu yangu wa mbali amesoma afya hana ajira kila siku ananiomba buku ya vocha hivi haya maisha yamekuja kuwaje
(MAGU MUNGU ANAKUONA)
Nikiwa sijajisahau ninavyo piga msuli wa PCB kwa nguvu zote hizi nikaja kukosa ajira itakuwaje ?
Ngoja nianze kuchanga hizi buku buku na pocket money nikimalizana na elimu nifuge hata kware.