Elimu ya Tanzania na Technology

Elimu ya Tanzania na Technology

mafikizoloo

Member
Joined
Oct 13, 2018
Posts
19
Reaction score
15
Ndugu wanajamvi kuna jambo linaniumiza kichwa sana inakuwaje kila siku vyuo vyetu watu wanagraduate na wimbi la ukosefu wa ajira likiongezeka huku tukishudia kila siku tunasema hatuna wataalamu na kushuhudia wataalamu wakitoka nje tunatengeneza ajira za wageni lkn sisi tukiishia kuwa vibarua kwao. Kwanini kama vyuo vyetu havikidhi ukuaji wa technology na kuwa suluhu kwa matatizo yetu ya kila siku kwanini visifungiwe vyote kuliko kuendelea kutoa unproductive product???
 
Jambo hili kweli linakuumiza kichwa au kodi ya pango imefika?
 
• Vyuo ni ‘kiwanda vinavyetengeneza’ watu ili wakaajiriwe ‘sehemu’. Mfumo wa chuo na ‘elimu shule’ umekaa kutengeneza watu ambao wanaenda kuajiriwa sehemu; havitengenezi waajiri. Sawa na kufyatua matofali ili yakajenge nyumba; inakuwa vipi wajenzi hawapo ama wachache ama wanajenga kwa mtindo mwingine?

• Vyuo vingi , wahitimu wengi (‘matofali mengi’); na waajiri wachache; USHINDANI umekuwa mkubwa. Ushindani hauletwi na wingi wa wahitimu tu, unaletwa na maendeleo na mageuzi ya teknolojia. Kwa mfano: wako wapi wasoma mita wa TANESCO, sidhani kama kitengo kile kipo– teknolojia (LUKU) imechukua nafasi yao na kinyume chake shirika, mwajiri, linapumua (mapato yameongezeka). Huo ni mfano wa wazi unaonekana.
Ikumbukwe waajiri wakuu ni Serikali na Sekta binafsi. Wote hawa wanataka kujiendesha kifaida na kiufanisi zaidi. Ukiwa na teknolojia inayofanya kazi za watu 100, maana yake ni faida na ufanisi upo juu, utahitaji watu wachache–kuhudumia nakuitunza teknolojia husika.

Ushindani unafanya waajiri wadengue, na kuanza kuweka machujio mbalimbali ili kuwapata watu wanaowataka pale wanapotangaza ajira. Kwa mfano: zimetangazwa nafasi 10 wanaomba watu 1000 au 2000 unafanyaje? Machujio yanaweza kuwa: Chuo ulichosoma (‘watu wanajiwekea tu vigezo mhitimu chuo ‘X’ anapewa kipaumbele kuliko chuo ‘Z’ kwa kozi ‘Y’), ufaulu, uzoefu n.k
Zama zimebadilika lakini mifumo haijabadilika.

• Ni wakati wa kuanza kutengeneza watu watakaoenda kuajiri; mfumo uliopo unatengeneza wengi wanaotaka kuajiriwa na wachache wa kwenda kujiajiri. Kama kila anatoka chuo kwanza anaweza kujiriwa matumaini yakiyeyuka anawaza kujiajiri; kuajiri ni suala la majaliwa– halipo kwenye mpango, inakuwa ngumu. Vyuo na mfumo elimu shule bado katika zama miaka ya 1970–, zama za viwanda. Miaka 8 iliyopita kwa mfano: walimu walikuwa hawaombi ajira, wanajikuta wapo sehemu fulani wanafanya kazi; sa’izi mambo ni tofauti. Cha ajabu watu wanahitimu latika ruwaza zilezile za fikra.

• Tujiajiri? Nani anasema hivo... wengi wanaoshauri hivo ni watu ambao wameajiriwa. Suala la ajira linahitaji kupewa jicho la tatu, serikali haitaweza kumaliza vijana wote mtaani, wale waliotumainishwa ukimaliza chuo kuna kazi.
Tufanye nini sasa? Tufunge vyuo? Basi elimu haina maana? HAPANA; kila mtu ajifunze kufanya kazi zake ndio uwe msingi wa kwanza, teknolojia inaturudisha huko. Kama ambavyo uvumbuzi wa motokaa uli badili nafasi ya farasi katika usafiri ndivyo ambavyo teknolojia leo hii (ya digitali) inabadili nafasi ya mtu.
Wanasiasa wanatuambia maneno ‘tunayotaka’ kusikia sio ‘tunayohitaji’ kusikia; tatizo la ajira ni kubwa mno na haliwezwi kumalizwa kwa mbinu za sasa. Vyuo vingi vinatembea wakati dunia inakimbia kwa kasi ya mwanga.
 
Wanasema wasomi wa hapa hawana exposure na Technolojia ya ulikwengu wa kwanza...
 
Ni kweli kabisa , unakuta mwajiri anataka mfanyakazi mwenye uzoefu wa miaka 2 sasa hawa wanaotoka mmoja kuwa mmoja chuoni itakuwaje?
 
Back
Top Bottom