Elimu ya shule za kata na matokeo yake

fellali

Member
Aug 14, 2013
17
2
ELIMU YA SHULE ZA KATA NA MATOKEO YAKE
Kati ya mambo ambayo watanzania wanayaenzi katika kipindi cha utawala wa waziri Mkuu mstaafu aliyeachia kiti kwa kujiuzuru baada ya kutokea dosari ya kuingiza nchini kampuni ya kufua umeme ambayo haikuwa na vigezo vinavyohitajika na hivyo kuisababishia hasara nchi na kuiingiza Tanesco katika matratizo makubwa ambayo mzimu wake unaendelea kuitafuna Tanesco hadi leo ninapoandika makala hii. Ninamzungumzia Mh. Edward Lowasa. Ndiye kiongozi aliyekuja na wazo la kuanzisha shule hizi inawezekana wapo waliotangulia lakini kwa kumbukumbu zangu huyu ndiye aliyelisimmia. Naamini ya kwamba mawazo ya Mh. Lowasa yalikuwa sahihi kwa wakati huo kwani kwa tafsiri yangu naweza kusema alilenga haya ninayobainisha:-
Naweza sema lengo lake la kwanza ilikuwa ni kuwasadia watanzania wa kipato cha chini ambao hawakuwa na uwezo wa kuwapeleka watoto wao katika shule za gharama kubwa yaani za binafsi iwapo wangeshindwa kuchaguliwa kujiunga na shule za serikali baada ya kumaliza elimu yao ya shule ya msingi. Matokeo yake yalikuwa na yanaendelea kuwa chanya kwani wanafunzi wengi wamepata nafasi za kujiunga na shule hizi baada ya kuwa zimefunguliwa.
Lengo la pili inawezekana lilikuwa ni kuongeza idadi ya wanafunzi wanaofaulu mitihani ya darasa la saba na kujiunga katika elimu ya sekondari. Kwa kiasi kikubwa aliweza kufanikisha katika swala hili maana baada ya hapo tumekuwa tukishuhudia idadi wafaulu wa mitihani ya darasa la saba ikiongezeka mwaka hadi mwaka na hivyo kuwavutia hata wanafunzi wenyewe mbali ya kwamba asilimia kubwa ya wanafaulu hawa wamekuwa wakipangiwa shule zilezile za kata.
Lengo la tatu ilikuwa ni kuongeza idadi ya wasomi ndani ya nchi yetu kwa maana ya kwamba kila mtoto aliyejiunga na elimu ya msingi alihakikishiwa kuendelea na elimu ya sekondari kwa kujiunga katika shule hizi za kata. Hili nalo pia amelifanikisha.
Lengo la nne ilikuwa ni kuondoa tabaka la ujinga ndani ya nchi yetu yaani kwa kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa angejua kusoma na kuandika na kupata elimu angalau kidogo ya kumsaidia katika maisha yake ya mbele. Katika hili aliweka mazingira ya kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kujiunga na shule ya msingi anaenda shule. Kwa zoezi hili pia alifanikisha.
Lengo la tano ilikuwa ni kuondoa adha kubwa waliyokuwa wanapata wanafunzi ambao walikuwa wanatembea umbali mkubwa kwenda shule. Ki ukweli wanafunzi wa aina hii walikuwa wakiteseka sana kwani walikuwa wakitembea umbali mkubwa kwenda shuleni na hivyo kuwafanya wachoke sana hata kabla ya kuanza masomo. Kwa kiasi chake alipata kuwasadia wanafunzi hawa na wazazi wao pia.
Kwa mtazamo wangu hayo ni baadhi ya malengo Mh. Lowasa aliyokuwa nayo ndani ya fkra zake alipokuja na wazo lakuanzisha shule hizi za kata. Siwezi sema amelikosea kwa kuanzisha shule hizi ila niseme kwamba hakuangalia upande wa pili wa shilingi katika jambo hili. Lakini pia wazo lake lilianza kutumika serikalini kabla ya kuliangalia kwa undani zaidi.
Ni kweli shule hizi zinasaidia kwa wale waliopata bahati ya kujiunga nazo, lakini shule hizi pia zinawatesa sana wanafunzi hawa wanaosoma katika shule hizi. Hebu tufikilie hili “mwanafunzi anaenda kujiunga shule ya sekondari ankuta kuna mwalimu mmoja tu” unadhani hata molali wa kusoma utakuwemo ndani mwake? Hauwezi kwasababu anajua hakuna atakachokipata kwa muda wa miaka minne atakayokuwa aple shuleni.
Au anaenda kujiunga kwenye shule yenye darasa moja ambalo linatumika kama ofisi ya walimu lakini pia ndilo darasa la kusomea; hakuna vyoo, hakuna kisima cha maji, hakuna madarasa ya kusomea, hakuna maabara, hakuna maktaba ya kujisomea, hakuna walimu wa kutosha, hakuna vitabu vya kujisomea, hakuna kitku chochote, ni jengo tu moja basi! Hapa kweli kutakuwepo kusoma au itakuwa ni kudanganyana tu.
Kimsingi wazo la Mh. Lowasa lilikuwa thabiti ila tu kulikosekana mipango madhubuti ya kufanikisha wazo lake vizuri. Na mbali ya mipango madhubuti pia kulikosekana watendaji kazi stahiki. Nasema haya kwasababu hayakuandaliwa mazingira ya kuweza kufanikisha wazo lake. Mazingira ninayozungumzia hapa ni pamoja na mipango mikakati ya kuweza kufanikisha zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa mazingira ya shule za msingi kupata elimu iliyobora na sio bora elimu. Kwa mfano angehakikisha kwanza shule za msingi zinakuwa na madarasa ya kutosha na madawati na vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya kuendesha shule; lakini kinyume chake hakuna mazingira yaliyobadilishwa kwa mfano hadi leo hii kuna baadhi ya shule hazina hata madawati wanafunzi wanakaa chini kwenye vumbi.
Kwa mtazamo wangu ili kufanikisha wazo lake kwa umakini, kwanza angehimiza kujenga majengo katika kata zote na kuhakikisha kwamba majengo hayo yana vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya kuanzisha shule za sekondari. Kwa mfano:- kwanza angehakikisha kila kata inajenga madarasa yakutosha kwa ajili ya kuanzisha shule. Pili angehakikisha kunajengwa maabara kwa ajili ya masomo yanayohitaji majaribio kwa vitendo kama vile Kemia, fizikia, biolojia n.k., Tatu angehakikisha japo kunajengwa bweni mbili kwa kila shule inayojengwa, Jambo la nne na muhimu angehakikisha serikali inaandaa fungu la kutosha kwa ajili ya kuajili waalimu wa kutosha ambao watafndisha katika shule hizi ikiwa ni pamoja na kuwawekea mazingira ya mazuri ya kazi hii ni pamoja na kujenga nyumba za kukaa walimu hawa.
Kwa mtazamo wangu wazo hili lilikuwa sahihi lakini tulilikurupukia kwani wakati wake ulikuwa bado. Yalipaswa kuandaliwa mazingira na mikakati ya kufanikisha zoezi hili na baada ya hapo ndipo zingefunguliwa shule hizi na kuanza kutoa huduma; lakini siyo kama ilivyofanyika.
Sasa nini matokeo ya kukurupuka kwetu? Kwanza badala ya kupata elimu bora tutapata bora elimu yaani tutaanza kupata wasomi-wajinga ambao hawajui kusoma wala kuandika (hii ni mifano alisia inayotokea). Hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia vimbwanga vya wanafunzi kumaliza elimu ya sekondari lakini hawajui kusoma wala kuandika! Siyo makosa yao ila ni makosa ya mfumo “kurupuka” tuliouanzisha pasipo kuandaa mikakati ya kutosha katika kulifanikisha.
Lakini jambo la pili ni kwamba wasomi tutakaowapata ni wasomi wa vyeti na sio wasomi halisia. Na ikifikia hapo ni kwamba tutakuwa tunaliangamiza taifa na siyo kuliokoa kama yalivyokuwa malengo yetu.
Tatu nikwamba hapa tutapata wasomi wanaoenzi ukabila na sio wasomi wanaoenzi utaifa. Tufikirie mtu aliyezaliwa Lushoto-Tanga, akasoma elimu ya msingi Lushoto, akapata elimu ya sekondari (O-level) Lushoto, akapata elimu kidato cha tano na sita Lushoto, elimu ya juu (Chuo kikuu) Lushoto kulekule; hivi mtu huyu atakuwa na uelewa gani? Si utakuwa ki-Lushoto-Lushoto au Ki-Tanga-Tanga? Hivi utendaji kazi wake utakuwaje pia akikutana na mtu wa kabila tofauti? Je, kutakuwepo mabadiliko katika jamii zetu? Maana mtu huyu atakuwa anawaza Ki-Lushtoto na hatakuwa na uingizaji mwanga (exposure) mpya wowote ule maana mawazo yake yatakuwa ndani ya Lushoto tu au Tanga tu. Lakini pia utendaji kazi wa mtu huyu utakuwa ni wa kikabila maana hajatengenezewa mazingira ya kuishi na watu tofauti-tofauti (yaani kabila tofauti).
Shule hizi zitageuka maeneo ya kukuzia wanafunzi hawa na siyo kuwapa elimu stahiki suala ambalo litapelekea kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wnaobeba mimba ziszotalajiwa na vijana wengi wa vijiweni na sio wasomi.
Lakini kutokana na elimu inayopatikana katika shule hizi, mwisho wa siku taifa litajikuta halina wasomi wa kuliongoza labda tu wale watakao kuwa wamepata bahati ya kwenda shule binafsi ambayo kitakwimu wanayokpata nafasi hizo ni wachache sana na ni wale wenye uwezo.
Jambo lingine pia ni kwamba tutatengeneza mazingira ya utawala wa kifalme kwani wale watakaoweza kupata madaraka ni wale waliopata elimu bora na sio bora elimu! Ambao asilimia kubwa ni watoto wa vigogo na sio walalhoi kama sisi. Jambi hili likifikiwa, litaathiri hadi maendeleo ya nchi.
Wakati hayo yakitokea na matabaka yatazidi kuongezeka kati ya wenye nacho na wasio nacho kwa maana kwamba watoto wa walalahoi wataendelea kupata bora elimu na watoto wa vigogo watendelea kupata elimu bora.
Wakati mwingine huwa nafikiria kwamba shule hizi zilianzishwa kwa ajili ya kuwatenga wenye nacho na wasio nacho maana asilimia kubwa ya wanaosoma kwenye shule hizi ni watoto wa walalahio na siyo watoto wa vigogo. Hivi tujiulize kama shule hizi zimejengwa kwa ajili ya wote kwanini watoto wa vigogo hawasomei kwenye shule hizi? Tusidanganywe na maneno ya wanasiasa kwamba shule hizi zinasaidia wazazi wasio na uwezo ila tuijiulize tunafaidi nini kutoka kwenye shule hizi?
Inawezekana Mh. Lowasa alikuwa na malengo mazuri ila yakachakachuliwa na wanasiasa wenzake kwa maslahi binafsi labda hatujui tunahisi tu.
Mwaka mmoja tu uliopita tumeshuhudia manyanga katika tasnia ya elimu pale ambapo zaidi ya nusu ya waliofanya mtihani wa kidato cha nne walishindwa mtihani wao wa mwisho; sakata hili likahusishwa na mabo mengi likiwemo suala la kidini na hivyo kuwaandama viongozi wa baraza hilo kuwa ndio chanzo cha wanafunzi kushindwa mitihani yao, lakini ukweli ni kwamba hayo ni matokeo ya shule za kata ambazo hazina dira wala malengo katika uwepo wake. Na kwa mtazamo wangu, huo ni mwanzo tu maana tunakokwenda itafika hatua wanaomaliza kidato cha nne wote wanashindwa au ni robo tu wanashinda mtihani huo tena kwa kujikongoja.
Mrisho mpoto aliwahi kusema “kuanza upya siyo ujinga”; tusimtafute mchawi wakati tunajiloga wenyewe, tujipange upya kwa maana ya tuanze mkakati upya wa shule hizi za kata, tumalize amjengo kwanza, kisha miundo mbinu, tuhakikishe upatikanaji wa walimu baada ya hayo yote turuhusu wanafunzi kwa ajili ya usomaji. Hakuna atakaye tuuliza maamuzi yetu, wala kutuamrisha kitu gani cha kufanya kama tukiamua. Tukiafanaya hivyo tuaiokoa tasni ya elimu katika nchi yetu.

Imeandaliwa na Lugeiyamu Felix.
 
Pongezi xna kwa maoni yako mazuri,ila da muda ushaisha kwa kufanya hayo na kwa serikar ya CCM its never do that coz of budy lidership,corruption and so many problem to our lider of tz br!
 
Back
Top Bottom