Elimu ya Sheria: Mgawanyo wa Mali kwa Wanandoa wanaotalikiana

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Tunapoongelea Wanandoa kugawana mali tunaongelea Talaka. Hakuna Mgawanyo wa Mali zilizotokana na Ndoa bila ya kuwepo talaka.

Kisheria Talaka inapotoka, hatua inayofuata ni mgawanyo wa Mali na Mustakabali wa Watoto kama wapo ikiwa ni pamoja na Matunzo yao.

Mali siyo lazima magari na nyumba lakini pia hata vyombo vya ndani vikiwemo Vitanda, Makabati na Samani navyo ni mali kwa mujibu wa Sheria.

Linapokuja suala la kugawana mali wengi hudhani mtindo unaotumika ni ule wa nusu kwa nusu, (50 kwa 50). Hakika huo si mtazamo wa Sheria ya Ndoa, 1971 Sura ya 29 iliyofanyiwa marekebisho, mwaka 2002 bali ni Mtazamo wa Mitaani .

Sheria tajwa, imeweka Msingi Mkuu wa Mgawanyo wa Mali ambao ndiyo hutumika katika Mahakama kutoa maagizo ya kugawa mali baina ya Wanandoa. Kifungu cha 58, 60 (a) na 61vyote vya Sheria husika vimeelekeza jambo hilo.

Msingi uliowekwa na Sheria tajwa hapo juu ni kiwango cha mchango wa Mwanandoa katika kupatikana kwa Mali bishaniwa. Katika suala hilo kiwango alichochangia Mwanandoa katika kupatikana kwa mali ndicho kitakachokadiriwa kuwa ndicho anakachostahili kupata. Mfano; Kama ni nyumba ya vyumba 6 mmoja anaweza kupata 1 na mwingine 5 kutegemea na mchango wa kila mmoja.

Aidha, mchango siyo lazima iwe leta ni lete au Shilingi kwa Shilingi bali hata kazi za nyumbani anazofanya Mama/Mke au Baba/Mume wa nyumbani ambaye hana kipato zenyewe nazo huhesabika kama mchango katika kupatikana kwa Mali husika.

Shauri Maarufu la Hawa Mohamed dhidi ya Ally Sefu la Mwaka 1983 T.L.R Na. 32 (CA) linahibitisha utaratibu huo.

Katika kutenganisha mali za Wanandoa, Mali hizo huwekwa kwenye Makundi Makuu Matatu:

KUNDI LA KWANZA:

Mali ambazo mmoja kati ya Wanandoa alikuwa nayo kabla ya kuoana au alikuja nayo wakati anaingia kwenye Ndoa. Mfano: Mwanamke au Mwanaume ameolewa au kuoa akamkuta mwenzake tayari ana nyumba yake basi hiyo haitachukuliwa kuwa ni Mali ya Ndoa.

KUNDI LA PILI:

Mali ambazo zimepatikama wakati wawili hao wakiwa tayari, ndani ya ndoa. Mfano: Ndoa imefungwa wawili wakaanza kuishi pamoja kwa taratibu wakaanza kujenga nyumba na kuikamilisha. Vifungu vya 59 na 60 (b) vya Sheria ya Ndoa, vinahusika.

KUNDI LA TATU:

Mali ambazo zimepatikana kwenye ndoa lakini hazina uhusiano wa kindoa. Mfano: Mmoja wa wahusika kurithi au kuzawadiwa mali fulani. Kifungu cha 61cha Sheria ya Ndoa kinaelezea.

KABLA NA BAADA YA NDOA:

Mali iliyopatikana kabla ya ndoa na ikaendelea kuwapo kipindi cha ndoa inaendelea kuwa ya huyo mmliki, bila ushirika wa mwenza wake, kwa mujibu wa kifungu cha 58 cha Sheria ya Ndoa.
Kama ni nyumba mwanamke alikuwa nayo kabla ya kuolewa au ni mwanaume alikuwa anamiliki basi inaendelea kuwa ya kwake peke yake na haihusiki katika mgao pindi itakapohitajika kufanya hivyo.

Hata hivyo, Mali husika inaweza kuingizwa katika mgao ikiwa kuna mchango wowote wa kuiendeleza uliotolewa na mwenza (Mke au Mume) au kwa mhusika kuamua yeye mwenyewe bila kulazimishwa, mali ihusishwe kama mali ya familia au Mali ya Ndoa.

Mfano: Kabla ya ndoa vyumba ilikuwa na vyumba viwili lakini katika kipindi cha ndoa imeboreshwa na kufikia vyumba vitano (5) au ilikuwa haina uzio, au madirisha kabla ya ndoa lakini baadaye vitu hivi vikawepo.

Katika hali kama hiyo itatakiwa iingizwe katika mgao na kutazama kiwango cha mchango wa kila mmoja katika uendelezaji huo. Ni hapo ambapo mchanganuo utafanyika ili kila mmoja apate haki kutokana na kiwango cha mchango wake. Ikiwa hakuna uendelezaji wowote nyumba inabaki kuwa ya Mwanandoa mmoja pekee ambaye ndiye mmiliki wa tangu awali.

Mambo ni hivyo hivyo, hata kwa mali ambayo imepatikana katika Ndoa lakini ikiwa haina uhusiano na kipato cha wanandoa. Mfano: Mali ya urithi au zawadi. Kifungu cha 61 cha Sheria ya Ndoa kinahusika.

Endapo Mali husika itaendelezwa basi mchango wa uendelezaji utatathiminiwa na ikiwa haitaendelezwa itabaki Mali ya mrithi au mpewa zawadi pekee na haitahusika katika mgao.

Jambo muhimu kwa sehemu kubwa ya jamii kulifahamu hapa ni suala la kuwa na mchango hasi katika ustawi wa familia. Mfano: Matumizi mabaya ya fedha za Miradi, Biashara, Uenzi wa Nyumba na hata Usababishaji wa Ndoa Kuvunjika unaweza kusababisha Mke au Mume kujipunguzia kiwango cha mgao au hata kukosa kabisa.
 
Aisee!
Elimu kuntu
 
kuna watu wanadai hata kama mwanandoa alimkuta mwenzie akiwa na mali mathalani nyumba, akinunua hata bulb tu basi naye atapata gawio murua kabisa. ikoje hii?
 
Hapo hakuna mgao atatakiwa aondoke na bulb yake na kama ameweka mlango atatakiwa aondoke na milango yake .
Jinsi ndoa za sikuhizi zinavyoangukia pua kila kukicha nashauri kama mtu anamali aliyoipata kabla ya ndoa ajitahidi kuiendeleza mwenyewe especially nyumba
 
Unatufundisha vizuri nitaweka hapo Chini MAAMUZI ya Mahakama ya Upeo ya Kenya vipi Kwa Tanzania huoni kama itakuwa na tija kama tukifuata misimamo huo?
Umesema mgawanyo wa Mali ya Ndoa unatolewa baada ya TALAKA je,Kwa Wale wanaofahamika kwa dhana ya Ndoa ni utaratibu gani hutumika KUGAWA Mali wakati hawapewi TALAKA?
Dhana ya Ndoa inakuwaje inakuwa Ndoa?

"KANUNI YA KUGAWA MALI 50-50 BAADA YA TALAKA HAITATUMIKA TENA! MAHAKAMA YA UPEO

Katika kesi ya talaka, kila mhusika anapaswa kuacha ndoa na mali aliyoipata wakati wa muungano" - Mahakama.
Muhtasari
• Majaji wakuu waliamua kwamba masharti ya Ibara ya 45(3) ya Katiba kuhusu usawa katika ndoa hayaruhusu mahakama yoyote kubadilisha haki za umiliki zilizopo za wahusika.

Wenzi wa ndoa hawana haki ya moja kwa moja ya asilimia 50 ya sehemu ya mali ya ndoa baada ya talaka, Mahakama ya Juu imeamua kusuluhisha mojawapo ya masuala yenye utata katika Sheria ya Familia.

Ikitangaza kuwa kanuni ya 50:50 haitumiki kabisa, mahakama ya juu ilisema kwamba katika kesi ya talaka, kila mhusika anapaswa kuacha ndoa na mali aliyoipata wakati wa muungano ingawa mwenzi anaweza kupata zaidi kulingana na mchango wake katika ndoa na upatikanaji wa mali ya ndoa.

Mahakama ya majaji watano ikiongozwa na naibu jaji mkuu Philomena Mwilu pia ilishikilia kuwa kila mwenzi katika ndoa lazima athibitishe mchango wake katika utajiri wa familia ili kuwezesha mahakama kuamua asilimia inayopatikana kwake katika ugawaji wa mali ya ndoa.

Mahakama ilisema kuwa mtihani wa kuamua kiwango cha mchango wa mhusika ni mojawapo ya msingi wa kesi.

Uamuzi huo unatarajiwa kutoa sura ya ugomvi wa kisheria kati ya waume zao wa zamani na wake wa zamani kuhusu kugawana mali baada ya ndoa zao kusambaratika.

Majaji wakuu waliamua kwamba masharti ya Ibara ya 45(3) ya Katiba kuhusu usawa katika ndoa hayaruhusu mahakama yoyote kubadilisha haki za umiliki zilizopo za wahusika.

Masharti hayo yaliyotajwa kufanya kazi tu kama njia ya kutoa usawa wakati wa kuvunjika kwa ndoa huku kila mhusika akiwa na haki ya kupata mgao wao wa haki wa mali ya ndoa, ilisema mahakama."
 
Ndoa isipoheshimiwa na watu wote, matokeo yake ndio hayo
 
Tunapoongelea Wanandoa kugawana mali tunaongelea Talaka. Hakuna Mgawanyo wa Mali zilizotokana na Ndoa bila ya kuwepo talaka.

Kisheria Talaka inapotoka, hatua inayofuata ni mgawanyo wa Mali na Mustakabali wa Watoto kama wapo ikiwa ni pamoja na Matunzo yao.

Mali siyo lazima magari na nyumba lakini pia hata vyombo vya ndani vikiwemo Vitanda, Makabati na Samani navyo ni mali kwa mujibu wa Sheria.

Linapokuja suala la kugawana mali wengi hudhani mtindo unaotumika ni ule wa nusu kwa nusu, (50 kwa 50). Hakika huo si mtazamo wa Sheria ya Ndoa, 1971 Sura ya 29 iliyofanyiwa marekebisho, mwaka 2002 bali ni Mtazamo wa Mitaani .

Sheria tajwa, imeweka Msingi Mkuu wa Mgawanyo wa Mali ambao ndiyo hutumika katika Mahakama kutoa maagizo ya kugawa mali baina ya Wanandoa. Kifungu cha 58, 60 (a) na 61vyote vya Sheria husika vimeelekeza jambo hilo.

Msingi uliowekwa na Sheria tajwa hapo juu ni kiwango cha mchango wa Mwanandoa katika kupatikana kwa Mali bishaniwa. Katika suala hilo kiwango alichochangia Mwanandoa katika kupatikana kwa mali ndicho kitakachokadiriwa kuwa ndicho anakachostahili kupata. Mfano; Kama ni nyumba ya vyumba 6 mmoja anaweza kupata 1 na mwingine 5 kutegemea na mchango wa kila mmoja.

Aidha, mchango siyo lazima iwe leta ni lete au Shilingi kwa Shilingi bali hata kazi za nyumbani anazofanya Mama/Mke au Baba/Mume wa nyumbani ambaye hana kipato zenyewe nazo huhesabika kama mchango katika kupatikana kwa Mali husika.

Shauri Maarufu la Hawa Mohamed dhidi ya Ally Sefu la Mwaka 1983 T.L.R Na. 32 (CA) linahibitisha utaratibu huo.

Katika kutenganisha mali za Wanandoa, Mali hizo huwekwa kwenye Makundi Makuu Matatu:

KUNDI LA KWANZA:

Mali ambazo mmoja kati ya Wanandoa alikuwa nayo kabla ya kuoana au alikuja nayo wakati anaingia kwenye Ndoa. Mfano: Mwanamke au Mwanaume ameolewa au kuoa akamkuta mwenzake tayari ana nyumba yake basi hiyo haitachukuliwa kuwa ni Mali ya Ndoa.

KUNDI LA PILI:

Mali ambazo zimepatikama wakati wawili hao wakiwa tayari, ndani ya ndoa. Mfano: Ndoa imefungwa wawili wakaanza kuishi pamoja kwa taratibu wakaanza kujenga nyumba na kuikamilisha. Vifungu vya 59 na 60 (b) vya Sheria ya Ndoa, vinahusika.

KUNDI LA TATU:

Mali ambazo zimepatikana kwenye ndoa lakini hazina uhusiano wa kindoa. Mfano: Mmoja wa wahusika kurithi au kuzawadiwa mali fulani. Kifungu cha 61cha Sheria ya Ndoa kinaelezea.

KABLA NA BAADA YA NDOA:

Mali iliyopatikana kabla ya ndoa na ikaendelea kuwapo kipindi cha ndoa inaendelea kuwa ya huyo mmliki, bila ushirika wa mwenza wake, kwa mujibu wa kifungu cha 58 cha Sheria ya Ndoa.
Kama ni nyumba mwanamke alikuwa nayo kabla ya kuolewa au ni mwanaume alikuwa anamiliki basi inaendelea kuwa ya kwake peke yake na haihusiki katika mgao pindi itakapohitajika kufanya hivyo.

Hata hivyo, Mali husika inaweza kuingizwa katika mgao ikiwa kuna mchango wowote wa kuiendeleza uliotolewa na mwenza (Mke au Mume) au kwa mhusika kuamua yeye mwenyewe bila kulazimishwa, mali ihusishwe kama mali ya familia au Mali ya Ndoa.

Mfano: Kabla ya ndoa vyumba ilikuwa na vyumba viwili lakini katika kipindi cha ndoa imeboreshwa na kufikia vyumba vitano (5) au ilikuwa haina uzio, au madirisha kabla ya ndoa lakini baadaye vitu hivi vikawepo.

Katika hali kama hiyo itatakiwa iingizwe katika mgao na kutazama kiwango cha mchango wa kila mmoja katika uendelezaji huo. Ni hapo ambapo mchanganuo utafanyika ili kila mmoja apate haki kutokana na kiwango cha mchango wake. Ikiwa hakuna uendelezaji wowote nyumba inabaki kuwa ya Mwanandoa mmoja pekee ambaye ndiye mmiliki wa tangu awali.

Mambo ni hivyo hivyo, hata kwa mali ambayo imepatikana katika Ndoa lakini ikiwa haina uhusiano na kipato cha wanandoa. Mfano: Mali ya urithi au zawadi. Kifungu cha 61 cha Sheria ya Ndoa kinahusika.

Endapo Mali husika itaendelezwa basi mchango wa uendelezaji utatathiminiwa na ikiwa haitaendelezwa itabaki Mali ya mrithi au mpewa zawadi pekee na haitahusika katika mgao.

Jambo muhimu kwa sehemu kubwa ya jamii kulifahamu hapa ni suala la kuwa na mchango hasi katika ustawi wa familia. Mfano: Matumizi mabaya ya fedha za Miradi, Biashara, Uenzi wa Nyumba na hata Usababishaji wa Ndoa Kuvunjika unaweza kusababisha Mke au Mume kujipunguzia kiwango cha mgao au hata kukosa kabisa.
.
 
Zinazogawanwa ni mali zote zile za mwanamke na zile za mwanaume ama za mwanaume tu?
 
Back
Top Bottom