Mimi niliwahi kua mtumishi wa altare since 2004-2015 ,, kwa experience niliokua nayo kuhusu mambo ya kanisa, pia nakumbuka padri mmoja aliwahi kutueleza haya mambo,, lakini kwa sasa bahati mbaya na yeye ni marehemu
'MSHUMAA, au moto huwakilisha uwepo wa Mungu inategemea na mahala husika, (nikimanisha sio kwa mfano mtu anawasha mshumaa au moto kwenye casino then tuseme Mungu yupo pale, ingawa kiimani Mungu yupo mahala pote) na shughuli husika, alitupa maelezo mengi sema nakumbuka machache
1.Mungu alimtokea Mussa katika umbo la moto, juu ya kichaka.
2.Roho mtakatifu aliwashukia mitume kwa njia za ndimi za moto.
3.Mtume Yohana aliwambia watu mimi na wabatiza kwa maji lakini yeye atawabatiza kwa moto na roho mtakatifu.
4. Kwa wasomaji wa bibilia watanisaidia kuna andiko ndani linasema Mungu ni moto ulao.
Mfano mwingine hai, wakatoliki tunaamini ekaristi ni mwili na damu ya Yesu kristu (sitaki kuzungumzia udini au dini ya mtu) lakini ni mfano rahisi kueleweka, ndio maana kwenye tebanakoa zinapohifadhiwa ekaristi takatifu masaa 24/7 ni lazima mishumaa itakua inawaka muda wote kama ishara ya kuonyesha uwepo wa Mungu mahala pale