Richard mtao
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 217
- 242
Hellow JF,
Kwa miaka ya hivi karibuni waajiri wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu utendaji kazi duni wa waajiriwa ukilinganisha na ufaulu wao unao onekana kwenye vyeti vyao vya kitaaluma.
Sitaki kupinga au kuelezea sana jambo hili kwakua sina taarifa za kutosha na hata tafiti sijafanya. Lakini naweza kusema machache kutokana na uzoefu wangu kipindi nipo chuo:-

- Wanafunzi wengi wa vyuo vya kati pamoja vyuo vikuu hawatumii muda wao vizuri katika masomo yao, wengi wanawekeza muda wao katika kufanya mambo ya kijinga yasiyo na manufaa ya muda mrefu katika masomo na hata maisha yao. Mfano, wengi wanawekeza muda katika kuaminisha watu wengine kwamba wao ni bora, wazuri, wajanja, sio maskini na wala hawajapitwa na nyakati.
- Wanafunzi wengi wanapenda shortcut, hawapendi kujishughulisha, pia ni wavivu sana. Hali hii inawafanya washindwe kutumia bongo zao na ndio maana wanakariri sana,wanakosa ubunifu, hawajiongezi na ndio maaana Wanapata GPA makubwa lakini hawawezi ku-apply katika utendaji.
- Mfumo unaotumika kupima uwezo na uelewa wa mwanafunzi bado upo chini sana, hali hii inasababisha wazalishwe wanafunzi wengi wenye GPA kubwa ambazo hazina uhalisia na uwezo wao.
- Wanafunzi wajitambue
- Vigezo vya kujiunga na vyuo vya kati/Vyuo vikuu viongezwe. Hii itasaidia kupunguza idadi ya wanafunzi wasio na uwezo kujiunga vyuo vikuu.
- Taasi z elimu ya juu zibadili mifumo yao ya kupima wanafunzi. Iwe knowledge and practices based education isiwe GPA based education.