Issue ya Jerry, ni Kova amehamanika tuu, elimu yake fresh tuu. Nakumbuka nilimuona kamanda Zombe siku alipokaimu nafasi ya Tibaigana, wakati akitangaza zile habari za polisi kufanikiwa kuwauwa wale majambaz wanne msitu wa Pande, baada ya kujibizana risasi na polisi, alitangaza kwa masifa sana, na kuita waandishi kushuhudia polisi wakipongezwa, kilichofuatia sote tunakijua.
Ukimuona kamanda Kova anavyoongea, ni wazi, anaongea kwa masifa na mapozi ya kusmile mbele ya camera. Kamanda Tibaigana pia alikuwa akiongea na waandishi daily ila was serious.
Pamoja na elimu zao zote, pia ni kweli na kuna uthibitisho, debe tupu hupiga kelele!. Si unaonaga mwenyewe hata baadhi ya magreat thinkers miongoni mwetu humu JF yunavyopigaga kelele za kidebe tupu?.