jamani mpo hizi ni habri tete na zina mustakabaliwa wadau wengi, najua hapa kuna vichwa nasubiri madavue na umma uweze kuelewa nini hasa kinanendelea.
Wewe ndo hauko updated
Wizara ilifafanua kupitia Naibu waziri Eng. Manyanya
Alisema waziri hajazuia watu wenye diploma kujiunga chuo kikuu, hajasema kwamba ili ufike chuo kikuu ni lazima upitie form six.
Alichosema ni kwamba endapo mtu umemaliza kozi flani na unataka kuendelea na kozi nyingine ni lazima uwe na sifa, mfano ukimaliza diploma na unataka kujiunga degree ni lazima uwe na GPA inayokuruhusu kujiunga na degree sio uwe huna GPA inayohitajika ukimbilie kusoma Foundation course ukidhani itakuongezea sifa,
Akaongeza kwamba lengo la foundation course ni kumkumbusha mtu au kum-brash mtu ambaye alikua nje ya mambo ya shule kwa kipindi kirefu hivyo anajikumbushia kabla ya kuanza degree yake rasmi.
Akatolea mfano mtu akimaliza darasa la 7 anasoma pre form 1 lakini endapo hakufaulu kwenye matokeo ya darasa la 7 basi pre form 1 yake haimfanyi awe na sifa za kujiunga na kidato cha kwanza.
Mfano mwingine ni mtu anayesoma pre form 5,huyu nae ili ajiunge form 5 ni lazima awe amefaulu mtihani wa kidato cha 4.
Kwa mantiki hiyo pre form 1 na pre form 5 zote ni mifano halisi ya foundation course.
Narudi kwa waliosoma degree zao Open university of Tanzania (OUT) au chuo chochote ilihali hawakua na sifa ndo wakafanya ujanja ujanja wakasoma foundation course, hawa imeelezwa kua degree zao sio halali na wanatakiwa kufutiwa hata kama itakua imepita miaka 40.
Pia kwa waliosoma diploma na cheti endapo walikua na sifa stahiki za kujiunga na ngazi zingine za elimu kama vile degree basi degree zao ni halali lakini kama walichakachua kwa ujanja wa foundation course nao wajiandae.
Akaongeza kua endapo ulimaliza form six na points za kujiunga chuo kikuu zilikua ni principle passes "E" mbili na baada ya muda principle zikapandishwa na kuwa "D" mbili utakua salama kwa sababu kwa wakati huo wewe unasoma chuo "E" mbili ndo zilikua zinatakiwa ili kujiunga chuo kikuu hivyo uko salama salimini.
Kama hujaelewa uliza au ingia YouTube kuna videos kibao wizara inaeleza kila kitu kuhusu hili.