Elimu ya foundation ya chuo kikuu huria inatosheleza kumpeleka mtu chuo kikuu?

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,568
2,910
Nimekuwa mdau wa Elimu muda wote
Hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia matamko na maelezo mengi tu kutoka kwa wadau mbalimbali wa elimu.
Leo hoja yangu ni kuwa je Elimu ya FOUNDATION inatosha kumpeleke mtu kusoma degree?

1. Foundation hutolewa kwa muda wa mwaka mmoja
2. ili uqualify ibaidi uwe una walau D 5 na umesoma course ya ngazi ya cheti walau mwaka mmoja au zaidi
3. ukishasoma na kufanya mitihani kulimgana na field yako ukipata wastani wa 50% basi hapo waweza kusoma degree.
4. kuna ushahidi wengi tu wamepitia njia hiyo na saa wanasoma masters na hata PhD.
Lakini waziri ndalichako amepiga fullstop!! anataka lazima ufiuke form VI
5. Chuo kikuu huria sasa hivi wana matawi karibu nchi nzima na nchi za nje na zaidi ya 60% ya wanafunzi wao wanasoma foundation ama wametokea foundation.

Maswali yangu mdadavue
1. je uamuzi wa waziri uko sahihi au la, maana kila chuo kikuu kina senate na council
2. je ubora wa Foundation ni questionable?
3. nini unaona kifanyike , maana wengi watakosa hizo fursa.
4. Je ni lazima kila mtu apitie form VI ndiyo afike chuo kikuu - vipi wale wa mature entry? nao watafutwa?
KARIBUNI.
Mdau
 
jamani mpo hizi ni habri tete na zina mustakabaliwa wadau wengi, najua hapa kuna vichwa nasubiri madavue na umma uweze kuelewa nini hasa kinanendelea.
 
Tatizo sio rahisi kupata jibu maana wengi wamepitia huko..na wote waliopita huko wanautetea hupo mfumo..na wale ambao hawakupita huko wanauponda bila sababu ya msingi..
 
Acha tucheze madrafti na bao tyu! Mtu nipo kazini mda wa jioni unaamua kujiendeleza kielimu! Waziri hataki.
Inaonekana hajui kuwa elimu in knowledge na sio vyeti
 
jamani mpo hizi ni habri tete na zina mustakabaliwa wadau wengi, najua hapa kuna vichwa nasubiri madavue na umma uweze kuelewa nini hasa kinanendelea.
Wewe ndo hauko updated
Wizara ilifafanua kupitia Naibu waziri Eng. Manyanya
Alisema waziri hajazuia watu wenye diploma kujiunga chuo kikuu, hajasema kwamba ili ufike chuo kikuu ni lazima upitie form six.
Alichosema ni kwamba endapo mtu umemaliza kozi flani na unataka kuendelea na kozi nyingine ni lazima uwe na sifa, mfano ukimaliza diploma na unataka kujiunga degree ni lazima uwe na GPA inayokuruhusu kujiunga na degree sio uwe huna GPA inayohitajika ukimbilie kusoma Foundation course ukidhani itakuongezea sifa,
Akaongeza kwamba lengo la foundation course ni kumkumbusha mtu au kum-brash mtu ambaye alikua nje ya mambo ya shule kwa kipindi kirefu hivyo anajikumbushia kabla ya kuanza degree yake rasmi.
Akatolea mfano mtu akimaliza darasa la 7 anasoma pre form 1 lakini endapo hakufaulu kwenye matokeo ya darasa la 7 basi pre form 1 yake haimfanyi awe na sifa za kujiunga na kidato cha kwanza.
Mfano mwingine ni mtu anayesoma pre form 5,huyu nae ili ajiunge form 5 ni lazima awe amefaulu mtihani wa kidato cha 4.
Kwa mantiki hiyo pre form 1 na pre form 5 zote ni mifano halisi ya foundation course.

Narudi kwa waliosoma degree zao Open university of Tanzania (OUT) au chuo chochote ilihali hawakua na sifa ndo wakafanya ujanja ujanja wakasoma foundation course, hawa imeelezwa kua degree zao sio halali na wanatakiwa kufutiwa hata kama itakua imepita miaka 40.

Pia kwa waliosoma diploma na cheti endapo walikua na sifa stahiki za kujiunga na ngazi zingine za elimu kama vile degree basi degree zao ni halali lakini kama walichakachua kwa ujanja wa foundation course nao wajiandae.

Akaongeza kua endapo ulimaliza form six na points za kujiunga chuo kikuu zilikua ni principle passes "E" mbili na baada ya muda principle zikapandishwa na kuwa "D" mbili utakua salama kwa sababu kwa wakati huo wewe unasoma chuo "E" mbili ndo zilikua zinatakiwa ili kujiunga chuo kikuu hivyo uko salama salimini.

Kama hujaelewa uliza au ingia YouTube kuna videos kibao wizara inaeleza kila kitu kuhusu hili.
 
naona mjadala unaenda vema , weel done guys. maan tukidadavua from both angles hopefully wengi tutaelewa, maaan kila mtu aamka na lake
 
ila eng manaynya aliweka sawa , swali je wa;e walioingia kazini wakiwa wamefauli degree ila waliingi akw aukanjanja na wengine leo wana mpka PhD UTAWATOA KWELI kuna tija? kama kweli audit ikifanyika watabakia wangapi clean?
 
Kitu cha kwanza cha kujiuliza ni nadharia ya OPEN UNIVERSITY au CHUO KIKUU HURIA ina maana gani au inataka nini kwa upande wa udahili. Tuingie kwenye mtandao tuangalie OPEN UNIVERSITIES nguli hufanyaje (UK, Netherlands na India kwa mfano). Kuna lengo kubwa moja: kupeleka elimu ya chuo kikuu kwa matabaka yote ya jamii kwa wale wenye uwezo wa kupata hiyo elimu. Ili kutimiza lengo hili vyuo hivi vinakuwa na "OPEN ENTRY POLICY" na "UINGIAJI HURUA" na ndio sababu vinaitwa OPEN UNIVERSITY au CHUO KIKUU HURIA. Kwa mantiki hii OPEN UNIVERSITY UK wao wanasema qualification wanayo itilia mkazo na yenye tija siyo ile ya kudahiliwa kwako bali ile unayotoka nayo. Ukiacha program chache huwa hawana entry qualifications bora waone una utayari wa kusoma.

Kama ni hivyo inabidi unapojiunga uanze na level stahili-mwenye ufaulu wa form6 au equivalent anaanza moja kwa moja masomo ya degree. Kama huna wanakuchukua na utafanya masomo ya msingi (yanaweza yakawa ni masomo yasiyo sehemu ya degree lakini ukiyafaulu unaunganisha au yakawa sehemu ya degree). Kwa hiyo unachukuliwa unaingia level tofauti kutokana na utayari wako.

Kwa OUT yetu wao sio huria kama hizo nyingine za wenzetu, ili ujiunge nao qualification za chini ndio hizo walizoweka na unapitia FOUNDATION Program, ukifaulu unaanza degree. Ukiwa na F6 au Equivalent unaingia degree level moja kwa moja.

Kama chuo hiki kitakuwa sawa na UDSM, SUA, etc kwenye vigezo vya udahili kama vilivyowekwa na TCU na vyuo vyenyewe ni wazi dhana ya openness au uhuria itakuwa haipo. Kama ni huvyo hakuna sababu ya kimantiki ya kuita chuo hicho OPEN UNIVERSITY maana siyo open au huria. Chuo kama hicho hakikidhi malengo ya chu kikuu huria. Ikiwa ndio nchi inavyotaka kuwa udahili wa OUT uwe sawa na vyuo vingine basi TUBADILI JINA.

Tukitaka iwe open university tunaweza kuwa na mdahalo uhuria wake uwepo kiasi gani kutokana na mazingira yetu lakini bila uhuria basi si chuo kikuu huria. Kwangu mimi naona umuhimu wa foundation program kwa OPEN UNIVERSITY (kuhusu vyuo vingine hilo ni jabo lingine). Foundation program inapanua wigo wa kupata elimu ya chuo kikuu. Tukumbuke elimu ni haki ya kila mtanzania, mwenye uwezo na mwenye nia apatiwe elimu ya chuo kikuu na akifaulu apewe shahada yake. Kama kuna matatizo na jinsi Foundation program ilivyo dawa ni kuiboresha ili lengo la elimu huria litimizwe na si kufuta foundation program. Hatuwezi wote tukapitia form5/6, certificate/diploma kwenda chuo au RPL. Kwa open university Foundation Program ni muhimu na ndio maana VC alomba wao waruhusiwe.

Kutokana na hayo niliyoandika mimi siamini kama uamuzi wa waziri ni sawa kwa upande wa OPEN UNIVERSITY-tumuombe aurejee tena au tufute OPEN UNIVERSITY na tuipe jina lingine. Tukumbuke kinachotambulisha CHUO KIKUU HURIA ni filosofia yake ya nani apate elimu na siyo mfumo wake wa kufundishia hivyo tunaweza kubadili filosofia ya uhuria na kikawa chuo kama vyuo vingine kwenye udahili hata kama wataendelea na mifumo ya sasa ya kufundishia.
 
Masiya umeeleza mambo mengi lakini nakujibu in short nadhani utaelewa
Chuo kikuu huria lengo lake sio kudahili watu wasio na sifa, na kutendo cha kudahili watu kwa kigezo cha foundation course ni makosa kabisa.
Lengo la chuo kikuu huria ni kuhakikisha watu wengi wanafikiwa regardless wako sehemu gani ndo maana wanakua connected kwenye e-learning
Pia lengo lao open university ni kutoa nafasi kwa watu waliokazini/watu wazima waweze kusoma bila kuhudhuria full time learning kwa maana ya kutokuathiri ratiba ya kazi zao kwa kiasi kikubwa.

Ndo maana watumishi wa serikali kwa sasa wanahimizwa kusoma kwa mfumo wa chuo kikuu huria
 
so swali la msingi ni
1. sifa za kuingia? Foundation ya Open inatofautianaje na ACCESS course to higher learning ya UK?
2. Vyuo vikuu vingi Huria vina incubators za kuzalisha wadahiliwa wa degree mbali na wale wa TCU form VI
3. OUT nayo ni sharti iwekewe mashart the same na TCU au wawe na TCU YAO?

another issues ni process zao
OUT hakuna kudisco ! mtu waweza soma weeeeee mpaka mika hata 8 wengine wana 10 sasa - tofauti na convetional je kuwawekea OUT mashart sawa na conventional ni sawa?

at the end tunapima 1. sifa za kuingia?, 2. process za kufundisha au 3 . product?
Je product za OUT zilizoanzia huko foundation wanaperform vipi kwenye market? - kazini? ili saa serikali ifikie kuona Foundation ni kero? au labda waboreshe ?

JE Phylosopphy OPEN learning ni nini? tunailewa sawa?
 
Masiya umeeleza mambo mengi lakini nakujibu in short nadhani utaelewa
Chuo kikuu huria lengo lake sio kudahili watu wasio na sifa, na kutendo cha kudahili watu kwa kigezo cha foundation course ni makosa kabisa.
Lengo la chuo kikuu huria ni kuhakikisha watu wengi wanafikiwa regardless wako sehemu gani ndo maana wanakua connected kwenye e-learning
Pia lengo lao open university ni kutoa nafasi kwa watu waliokazini/watu wazima waweze kusoma bila kuhudhuria full time learning kwa maana ya kutokuathiri ratiba ya kazi zao kwa kiasi kikubwa.

Ndo maana watumishi wa serikali kwa sasa wanahimizwa kusoma kwa mfumo wa chuo kikuu huria
Mkuu distance education ni mfumo wa kufundishia ambao unaweza kukidhi hicho ulicho andika hapo. OPEN university by definition inatakiwa kuwa na milango wazi-short of that sio OPEN UNIVERSITY. Tafadhali angalia vyuo vilivyo bobea vinavyojinasibu kuwa ni open universities. Hivyo kama hatutaki open entry (admission) policy na foundation programs kwa OUT-tuibadilishe jina, na itaendelea kutufikia kupitia distance education. Nakazia kuna tofauti kati ya distance education kama mfumo wa kufundishia na nadharia ya chuo huria kama nilivyo eleza hapo juu. Kama tunachotaka ni Distance education mimi sinatatizo weka vigezo vyako vikali vya kudahili-lakini kama tunachotaka ni CHUO HURIA lazima tuwe na milango wazi. Nivumilie nadhani utanipata.
 
Nafikiri wengi hatuelewi maana ya Open university. Tofauti ya Open na vyuo vingine ni mfumo wa elimu ili kufikia watu wengi ambao kwasababu mbalimbali hawana muda wa kusoma full time hivyo kuwezeshwa kufikiwa na elimu kwa mtindo tofauti na vyuo vingine. Lengo la mfumo wa Open si kudahili wasio na sifa then kuwatafutia mlango wa kupata elimu ya juu. Swala la watu wasio na sifa wanasaidiwaje nje ya mfumo rasmi kila chuo kinaweza kuwa na utaratibu wake na si kazi ya Open tu. Unakuta mtu anayo Diploma ya Accounts na uzoefu wa kazi wa miaka 3 ktk uhasibu...kwanini kusiwe na utaratibu wa kudahili watu kama hawa? Upo umuhimu wa wizara kubaki na kazi ya sera na miongozo yenye option nzuri kwa makundi yote then vyuo viweke standard zao.
 
Pia tusibebe definition za open universities bila kujua kama kwa Tanzania lengo lilikuwa nini. Ndio maana kwa Tanzania Open wanapelekwa wanafunzi wenye sifa za kusoma chuo kikuu while wengine wana define kama sehemu za "vilaza".
 
Wewe ndo hauko updated
Wizara ilifafanua kupitia Naibu waziri Eng. Manyanya
Alisema waziri hajazuia watu wenye diploma kujiunga chuo kikuu, hajasema kwamba ili ufike chuo kikuu ni lazima upitie form six.
Alichosema ni kwamba endapo mtu umemaliza kozi flani na unataka kuendelea na kozi nyingine ni lazima uwe na sifa, mfano ukimaliza diploma na unataka kujiunga degree ni lazima uwe na GPA inayokuruhusu kujiunga na degree sio uwe huna GPA inayohitajika ukimbilie kusoma Foundation course ukidhani itakuongezea sifa,
Akaongeza kwamba lengo la foundation course ni kumkumbusha mtu au kum-brash mtu ambaye alikua nje ya mambo ya shule kwa kipindi kirefu hivyo anajikumbushia kabla ya kuanza degree yake rasmi.
Akatolea mfano mtu akimaliza darasa la 7 anasoma pre form 1 lakini endapo hakufaulu kwenye matokeo ya darasa la 7 basi pre form 1 yake haimfanyi awe na sifa za kujiunga na kidato cha kwanza.
Mfano mwingine ni mtu anayesoma pre form 5,huyu nae ili ajiunge form 5 ni lazima awe amefaulu mtihani wa kidato cha 4.
Kwa mantiki hiyo pre form 1 na pre form 5 zote ni mifano halisi ya foundation course.

Narudi kwa waliosoma degree zao Open university of Tanzania (OUT) au chuo chochote ilihali hawakua na sifa ndo wakafanya ujanja ujanja wakasoma foundation course, hawa imeelezwa kua degree zao sio halali na wanatakiwa kufutiwa hata kama itakua imepita miaka 40.

Pia kwa waliosoma diploma na cheti endapo walikua na sifa stahiki za kujiunga na ngazi zingine za elimu kama vile degree basi degree zao ni halali lakini kama walichakachua kwa ujanja wa foundation course nao wajiandae.

Akaongeza kua endapo ulimaliza form six na points za kujiunga chuo kikuu zilikua ni principle passes "E" mbili na baada ya muda principle zikapandishwa na kuwa "D" mbili utakua salama kwa sababu kwa wakati huo wewe unasoma chuo "E" mbili ndo zilikua zinatakiwa ili kujiunga chuo kikuu hivyo uko salama salimini.

Kama hujaelewa uliza au ingia YouTube kuna videos kibao wizara inaeleza kila kitu kuhusu hili.
Nimependa ufafanuzi wako..nimekuelewa vizuri sana.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom