Elimu ya bure kuhusu Deni la Taifa, Serikali iungwe mkono

Comrade Mushi

Member
Feb 25, 2023
5
7
Kuhusu deni la serikali muhimu zaidi ni Elimu kulihusu ili kutoa dhana kwamba serikali huwa inakopa ili kununua V8. Well Kimsingi kabisa deni la serikali hutokana na maeneo makuu 3 ambayo ni.

1. Serikali na idara zake kukopa/kudaiwa.
2. Serikali kudhamini (guarantor) sekta binafsi kukopa.
3. Serikali kuwakopa watu binafsi kwa mfumo wa hati fungani.

Madeni ya No. 1 hapo wakati mwingine huwa hayawezi kuepukika kwa sababu ya day-to-day operations za serikali ambazo wakati mwingine zinashindwa kugharamiwa kwa fedha za "Cash'' pekee, lakini pia madeni hayo yanaweza tokana na riba, matokeo ya mashauri ya serikali katika mahakama, adhabu etc.

Madeni yanayotokana na serikali kuwa mdhamini wa sekta binfasi (guarantor) ambayo kimsingi kwa data za sasa ni Tril 20 haya kimsingi ndio chachu na roho ya sekta binafsi kokote duniani.

Iko hivi, mwekezaji X kutoka Tanzania anaweza ona fursa ya kuwekeza nchi Y lakini akawa hana mtaji wala dhamana ya kutekeleza project yake lakini kwakuwa ni mwekezaji wa kuaminika Tanzania na anadhaminika basi nchi inamdhamini kuchukua mkopo mahala fulani ili atekeleze. Hii katika overall counts inahesabiwa kama deni la taifa.

Hii njia ya serikali kudhamini wafanyabiashara wake ndio hii ilitumikaga kututawala. Zile kampuni za kina Carl Peters zilipataga chance ya ku expand biashara yao kupitia hii njia, na hata sasa zipo kampuni kadha.

Njia ya tatu ni serikali kukopa watu wake kupitia vitu viaitwa hati fungani. Hizi zinakuwa za muda mfupi na muda mrefu (Treasury Bills/Bonds) ambapo pia njia hii hutumiwa na serikali kupunguza hela kutapakaa sana miongoni mwa raia, na kuna tetesi serikali recently imefanya udhamini wa Tril 20 zingine kwa sekata binafsi so ni likely kukawa na deni la jumla linalofikia 90.1 soon.

Hapa serikali inaitisha mnada wa hizi bonds watu wananunua kwa mashrti ya kurudishiwa hela zao baada ya muda Fulani (mara nyingi kuanzia 5 yrs+) then serikali inapata hela ya kutekelezea projects mbili tatu, na hii pia huwa part ya deni la serikali. Na kwa mujibu wa Data deni la sasa litokanalo na hati fungani ni Trilioni 26.

Sasa haya yote kwa ujumla wake ndio hufanya kitu kinaitwa deni la taifa na unakuta wakati mwingine ni kiasi kidogo sana ndio kinaingia katika matumizi ambayo wengi huwa tunadhani ndio sababu ya nchi kama zetu kukopa.
 
Back
Top Bottom