Elimu ya Bongo ni zaidi ya Komedi

Elimu ya Bongo ni zaidi ya Komedi

Wapendwa mm ni mgeni wa jf.kuna Uzi nilitaka tujadili kuhusu elimu yetu kwa sasa. Kwanza ni nchi gani kwasasa inaongosa east Africa. Kielimu? Je serikali ya tz walifikiria nn kuondoa drs la saba? Je tutarajie nini siku sijazo kwa secta ya elimu? Naombeni mtu moja awake vizuri kama Uzi Ahsanteni
 
Elimu haijawahi kwenda sawa kipindi chochote kila awamu zote ukitoa ya mwalimu tu.ndio mwisho wa elimu bora kutoka labda na mzee mwinyi lakn waliobakia wote hakuna kitu.zuga tu
 
Tunaweza sifu kitu wkt hawa wakina Ndalichako wameuza vyeti feki kibao tu enzi zao na ndio watu wanaojifanya wamesoma na kuponda ya sasa wkt hawa walinunua
 
Kama uliwaamini walikuzidi akili

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Hii elimu ya TZ hasa kwa kaya za vijijni ni shida sana, juzi nimetoka kwetu kusalimia nikaenda kumsalimia shangazi yangu kijiji jirani mwane kafaulu kwenda form one shule iko kijiji cha pili cha kuhuzunisha shule nzima form one mpaka four, kila kidato kina madarasa mawili, tangu shule ifunguliwa mwalimu ameingia darasani chini ya mara 10. Jamani huko kanda ya kati sijui kuan shida gani Ashatu Kijaji mbunge mpya aangalie hili jambo, watoto wana acha shule kwenda kulima na kuolewa. Sasa hapa mwnafunzi akishindwa kukutajia utakacho uta shangaa?
 
Dah! Yaani nafikiri hao vijana wamekushangaa kuliko ulivyowashangaa. Inawezekana walitoa majibu ya kijinga ili waone uelewa wako. Walivyokudanganya walitegemea critical response kutoka kwako badala yake ukawa unabaki kuwaangalia. Wakajisemea kwamba kumbe Tanzania bado Kuna watu watu wanadanganywa kama watoto na hawaoji. Kwanini wasishangae na wao?
 
Punguza jazba ndugu.
Sisi walimu tunakutana na wanafunzi 4m3 hajui kusoma vizur kiswahili na kuandika. Na pote alipopita kafaulu vizur tu.
Naanzakuamini haya makanisa yanayofanya miujiza maana yapo makubwa zaidi ya hayo.

Mwisho kabisa kijana wako akifika kidato cha nne hasa karibu na mtihani wa mwisho, akikuomba fedha kuanzia 30,000/= na kiendelea tambua tia maji tia maji imeenza....mwandalie nguo za kuingia kidato cha 5 hata kama hajui kusoma.
 
hivi jamani ni kweli tunataka kuwa na wasomi nchi hii au idadi tu ya watu ambao angalau wameenda shule? kuna vijana wawili nimekutana nao na nilipowauliza wakasema wote wapo kidato cha tano na karibuni wanaingia kidato cha sita. hivyo nikataka tu kujua kuwa wanachukua combinations zipi au gani ndipo nikashtuka kidogo kwa majibu yao kwani nilishajua kuwa hata wakienda chuo kikuu hawatakuwa na jipya kutokana na kwamba tangia huku chini hawakuwa na msingi mzuri wa hasa kujua wanataka kusomea nini au kuja kuwa nani hasa kitaaluma hapo baadae.

wa kwanza aliniambia anafanya kombi ya LDP akimaanisha Literature, Divinity na Physics.
wa pili akasema yeye anafanya kombi ya AKI akimaanisha Agriculture, Kiswahili na Islam.

najua humu kuna wasomi mliobobea na wajuzi wa mambo mbalibali yahusuyo elimu hivyo naomba michango yenu je hao vijana wako sahihi kwa hizo combinations zao wanazozifanya na kwamba zina tija au sisi wenye elimu zetu za zamani za kikoloni ndiyo tulipotea maboya?

karibuni tulifanyie uchambuzi hili suala.
Walikuwa wanatest kama wewe umefika advanced level
Kilichotokea umewaamini bil kuhoji hahahaha
 
Ulikuwa unawauliza maswali wana njaa wakaona wakuzuge
 
Back
Top Bottom