Elimu ya anga

Elimu ya anga

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,014
Reaction score
828,772
Je, ushawahi kujiuliza tofauti kati ya AIRPLANE or AEROPLANE?
Au AIRCRAFT na FLIGHT?

Ingawa maneno haya yote kwa Lugha ya kiswahili yanaweza kumaanisha Ndege, lakini hizi ndiyo tofauti zake;

Airplane:
✅ Neno hili hutumika sana katika Kiingereza cha Marekani, likimaanisha chombo cha usafiri wa anga chenye mabawa tulivu (Fixed wing)

Aeroplane:
✅ Neno hili hutumika katika Kiingereza cha Uingereza na lina maana sawa na 'Airplane' tofauti ni matamshi kati ya Nchi na Nchi.

Aircraft:
✅ Hili ni Neno pana zaidi likimaanisha ndege zote au mashine yoyote yenye uwezo wa kuruka angani.
Inajumuisha Ndege za kawaida, Helikopta, Glider, Drones, Puto, Tiara n.k.

Flight:
✅ Neno hili linamaanisha safari au kitendo cha ndege kuruka.
Linaweza kumaanisha safari ya anga iliyoratibiwa mfano 'Flight EK 200' au tukio halisi la kuruka kwa ndege yeyote.
1749970049563.jpg
 
Back
Top Bottom