Eyce,
Kutafuta best talents....ni mpaka hapo mshahara wa walimu uwe juu sawa na mahakimu,wahasibu etc..ndipo ualimu uta attract watu makini...lol..hili swala liko complicated kidogo.hata watu wenye best talents hawatumiki ipasavyo kutokana na maslahi duni...mtu kama Ras Simba sijui kwa nini serikali haimchomoi huko aliko afundishe walimu kadhaa stratergies zake anazotumia kufundisha English ,tukawa na ma Ras Simba kibao......??.mnhhhhhh....
Waliopewa hiyo dhamana wanawaza matumbo yao tuGood idea lakini kikubwa mfumo uwekwe wa kutafuta best talents katika ualimu. Selection proper ipite ikiwezekana wawekewe grading system kutokana na competencies zao ili iwe rahisi katika kuwaajiri.
kingine kuna masomo kama basic economics, business, improved civics, ICT and other soft skills yahimizwe kuanzia O'level maana ndipo dunia inaelekea.. Sijui hata hizi Wizara zinafanya nini kiukweli
Hilo la kufoji prac kwa wanafunzi wengi wanatumia kama mserereko yaani elimu yetu inazingatia sana ufaulu wa kwenye makaratasiKwa uzoefu wangu mpaka sasa, nimegundua tatizo la elimu yetu halipo kwenye mitaala bali lipo kwenye utekelezaji wa hiyo mitaala. Mfano wanafunzi hawasomi namna ya kufanya practicals ila wanajifunza kufoji ingawa mitaala imeeleza vizuri namna wanavyotakiwa kujifunza hizo practicals. Sasa baadae mwanafunzi akishindwa wanaanza kusingizia mitaala. Hasa shule zetu za kata ndio zinaongoza kwa kutofuata mitaala, Wanafunzi wanajisomea hovyo hovyo tu.
Elimu ya A level ni kwa ajili ya maandalizi ya kwenda hatua nyingine mbele na sio kuishia hapo, nchi ambazo hazina A level basi lazima mwaka wa kwanza chuo utumike kuwafundisha wanafunzi kozi ambazo walizikosa kwa kutosoma A level. General studies ya A level iko vyema katika kupanua uelewa wa mambo mengi lakini wanafunzi wanaichukulia poa, sasa hapo tatizo la mitaala lipo wapi?.