SoC02 Elimu wakati tulionao na tuendapo

Stories of Change - 2022 Competition

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
ELIMU WAKATI TULIONAO NA TUENDAPO

Kwa nchi nyingi za Afrika, elimi ni kurithisha maarifa, stadi na ujuzi kwa mwanafunzi katika eneo maalumu. Hata katika jadi ilikuwa ni hivyo hivyo ambapo walirithisha ujuzi, maarifa na stadi kwa vijana kwa kuzingatia umri na jinsia.

Katika mabadiliko ya dunia, elimu sasa ina sura mbili ya kurithisha na kukuza kile alichonacho mtu kichwani. Tanzania bado tupo katika mfumo wa jadi wa kurithisha tunamchukulia mtoto kama mtu asiye na chochote kichwani, hivyo anatakiwa kupewa maarifa, stadi na ujuzi.

Yapo mambo yanayokwamisha tuwe kwenye duara la elimu tegemezi, watumishi wasio hali, mambo haya yanafanya elimu ikose muelekeo sahihi kulingana na mabadiliko ya dunia, sera za nchi, uchumi wa serikali katika ajira, mazingira na watumishi kama ifuatavyo:

Kuendana na wakati. Mitaala inatakiwa ibadilike kufuata muelekeo wa elimu kidunia, sera za nchi na mahitaji ya jamii, badala tu ya kuingiza kitu kwa mwanafunzi sasa zinapaswa na kukuza kile kitu alichonacho mwanafunzi. Hii itajenga teknolojia na wawajibikaji maana wanafanya wanachokipenda. Mfano tuna watumishi hawakuwa na ndoto ya kazi wanazofanya ila mfumo wa elimu umewapeleka huko.

Ziwepo posho za mazingira magumu ya kazi. Ni ukweli yapo mazingira magumu katika utendaji, ndio maana wengi wanakimbilia mijini na maeneo nafuu. TAMISEMI iangalie namna ya kuweka utaratibu utaokuwa chini ya halmashauri kutoa posho za mazingira magumu. Mwl. J.K. Nyerere alipoanzisha vijiji vya ujamaa, alitambua, kuna changamoto kimazingira katika kutoa huduma za kijamii, hivyo ni bora watu wakae sehemu moja.
Sasa leo ni wakati mwingine serikali kupitia wizara ione tija katika hili.

Vyuo vya ufundi vijengwe vijijini. Unapotembelea katika wilaya zetu utakuta vijiji vingi kiwango cha elimu cha watu wake kipo chini( darasa la 7,kidato cha 2 na 4). Ni wazi rasilimali watu wa eneo husika ni duni, uwepo wa vyuo vya ufundi ingesaidia kuwapatia nafasi ya kupata utaalam na vyeti wakaingia katika mfumo rasmi wa uzalishaji kama udereva, ufundi, kilimo, uvuvi, uvunaji misitu, nishati endelevu, ufugaji nk.
Zipo halmashauri uchumi wake na hali ya maisha ni duni kutokana na elimu ni duni. Tuwekeze katika vyuo vya ufundi.

Elimu itazame upya ukomo wa maisha. Ni muhimu kufanya tafiti na uzuri sensa imepita, serikali kupitia wizara wafanye tathimini juu ya idadi ya madarasa anayopaswa kusoma mtu, umri wa kuanza hadi kumaliza, umri wa ajira, kustaafu na hali ya starehe ya maisha nchini. Umri wa elimu nchini ni mrefu ukilinganisha na ukomo wa maisha (miaka 7 shule msingi, miaka 4 sekondari, miaka 2 sekondari tena na chuo miaka 3,4, 5 na kuendelea ). Kuna haja ya kujenga taifa la wasomi ila wanao yafurahia maisha ya elimu na ukomo wao wa maisha.

Wizara isimamie haki na maslahi ya walimu sekta binafsi. Kuna anguko kubwa la mishahara, kuna wingi wa mikataba feki ila walimu hawalipwi hii mishahara wala hizo stahiki zilizoanishwa, BIMA hakuna. Serikali inapoteza pesa kwa wasomi waliokopa, wengi wapo sekta binasfi ila hawawezi kulipa madeni na serikali inakosa kodi katika mishahara ya walimu sekta binafsi kwa uduni wa mishahara na malipo yake hayapo katika mifumo rasmi.

Elimu iendane na soko la ajira la dunia. Tukubali serikali ina mzigo mkubwa wa vijana wanaotaka ajira, lazima tuwaandae vijana kifikra na kitaaluma ili waendane na soko la ajira ndani na nje. Ushauri, Serikali ione namna ya kuunganisha vyuo vyetu vya ndani na vyuo vya nje kitaaluma, kimkakati, kwa mbadilishano kupitia ufundishaji wa teknolojia ya mbali na mualiko. Tumudu lugha za mataifa, diplomasia, historia, utamaduni na sanaa.

Kozi za mafunzo ya ualimu msingi ngazi ya 4, 5 na 6 (NTA Diploma ) zilirudishwe walimu wa shule za msingi waweze kujiendeleza. Naishauri pia Wizara hili suala lipewe sekta binafsi kuliendesha kwani itafufua vyuo na serikali itanufaika kwa kuongeza umahili, kodi na kupanua wigo wa tafiti za elimu, ajira na matumizi ya teknolojia katika ufundishaji kwa kuwa sekta binafsi ni uwekezaji mkubwa usiotaka pesa ya serikali.

Wizara izingatie haya:
  • Usimamizi wa mitihani udhibitiwe kama wa utaratibu wa necta katika upakiaji wake.
  • Kuandaliwa kwa rasimali za ufundishaji na ujifunzaji kwani mitaala ipo.
  • Vyuo binafsi vipewe kuendesha hii kozi.
- Mafunzo ya ualimu kutengwe muda maalum wa kutengeneza zana maalum kabla ya kuhitimu. Inapaswa kila mwalimu anapohitimu awe na begi lake maalum lenye zana huko anapoenda akaanzie nazo katika ufundishaji wake. Kwa kutenga muda rasmi wa miezi 2 ya wanafunzi kujitengenezea zana mmoja mmoja, itafanya tupate walimu wenye nidhamu ya kutengeneza zana, kufaragua zana na kuwa tayari kutumia zana mana katoka nazo chuo.

Masomo ya ziada yasiwekewe vikwazo. Masomo ya ziada wakati wa masomo na wakati wa likizo yaachwe. Yanasaidia kumjenga mwanafunzi awe na uwezo wa kupambanua mambo, kuchambua mambo na kilinganisha mambo. Umpa nafasi ya kubadili mazingira ya ujifunzaji na kujipima katika mazingira mengine.

Inasaidia wahitimu kujiajiri na kujengwa kwa taasisi za ustawi wa jamii zenye kutoa huduma za elimu na malezi.
Kutafsiri vyema sera za elimu ili kutoua ushiriki wa wadau wa elimu hususani wazazi na walezi. Mfano, tafsiri ya elimu bila malipo imepunguza kwa kiwango kikubwa ushiriki wa wazazi katika maendeleo ya shule, kumekuwa na mvutano kati ya walimu na wazazi na kumekuwa na kutokuaminiana kati ya mwalimu na mzazi.

Uhamasishaji wa elimu ufanyike vijijini na miradi inapokuja wapewe wasomi waliopo katika maeneo hayo ili kuzidi kuonyesha umuhimu wa elimu katika vijiji hivyo. Maeneo ya vijijini bado elimu imekuwa ni sehemu tu ya kupeleka watoto wakakue na sio kwa malengo kwamba watapata maisha bora ndio maana asilimia kubwa ni darasa la saba hadi kidato cha nne na baada ya hapo wengi wanakuwa tu mtaani, ile thamani ya elimu haipo.
Uchumi wa viwanda ni lazima tutengeneze rasilimali watu wenye ujuzi husika. Hili ni suala la elimu kuendana na sera za nchi ya viwanda.

Viongozi waache kudharau michepuo ya elimu nchini. Kwasasa sanaa sio bora, bora sayansi huku ni kuua sekta binafsi za elimu nchini. Bunge kikatiba Mbunge inahitaji kujua kusoma na kuandika, mahakama haina wanasayansi.

Wito wangu kwa Watanzania, tushiriki kikamilifu katika elimu, sisi ndio wadau wakuu wa elimu nchini ni lazima tushiriki kimawazo, kimali na kinguvu na huu ni wajibu sio hiari.

Wito wangu kwa wizara, itazame haya kwa jicho la tatu.
Na mmmuhumba
0624 440 454
 
Habari yako ndugu Mmmuhumba.

Hongera kwa nakala nzuri yenye mawaidha na tija kwa jamii.

Kura yangu umepata!!

Nikiamini katika uchakataji wako wa mambo na uwezo wako wa fikra na ubunifu, naomba ukipendezwa, nipate mawazo yako au mapendekezo juu ya nakala ihusuyo


Ahsante!!
Asante sana ndugu Deo.
Nitaingia katika link iliyoiweka nami nitapata cha kushauri katika hilo.
Ubarikiwe ndugu.
 
Asante sana ndugu Deo.
Nitaingia katika link iliyoiweka nami nitapata cha kushauri katika hilo.
Ubarikiwe ndugu.
SUALA LA BIMA, nashauri:
1. Warudi upya katika jamii na kufanya kabisa kampeni rasmi ya watu wajue thamani ya BIMA NIHF Tanzania nzima kupitia mawakala wao wa mikoa na wilaya.
kwanini kampeni? Huduma ya afya ni jambo kubwa sana ila uhamasishaji wake umedolola nchini upande wa Bima. Ifanyike kampeni rasmi itayokutanisha watu na usajili uwepo hao hapo baada ya elimu.
2.Watizame NIHF kama ni mfumo wa Biashara na huduma kwa jamii. Waweke utaratibu wa muda wa kupiga debe kuongeza wanachama kila mwaka kwa kutembelea vijijini haswa ambapo maisha ni duni na wanahitaji kufikiwa maana vipato vyao ni vya msimu,, watambue muda wa mavuno ni muda ambao wakulima na wafugaji wanafedha, ni rahisi wanaposogezewa huduma kujisajili mana pesa ipo. BIMA zetu hawajatambua muda sahihi wa kupiga debe ipate wateja katika maeneo tofauti nchini.
3. Waongeze idadi ya wapata huduma katika BIMA na gharama zishuke kidogo. Nimeona watu wanatamani sana kujiunga na BIMA ya afya ila gharama, wengine wamelazimika kuongea na mawakala wawasajili na watu wasiotambuana nao ili tu wamudu gharama pangwa yaani wakala anapata mtu ila hajakamilika fedha analazima kumchuku na mtu nwingine wa nje ya familia na kuwapatia bima moja.
4. Dawa na huduma zizibitiwe kwa wanaufaika, uzuri sensa imepita itasaidia kutoa takwimu ya watu katika maeneo, wajiwekee malengo ya kufikia kihuduma.
5. Utaratibu wa malipo ya haraka kwa hospitali binafsi zinazotoa huduma za BIMA NIHF ewekwe ili kufanya hospitali binafsi zisione hasara ya mfumo wa Bima.
6. NIHF ijiwekeze katika makampuni ya hisa (wapate gawio) na miradi endelevu hapa nchini ili kukuza fedha na kujiimarisha kiutendaji na vifaa tiba.
7. Kuwepo na utaratibu wa kualika na kupokea wataalamu wa afya wanaopenda kuja Tanzania kusaidia wanafaika wa Bima. Hii itafanya tupate wadau toka nje, wataalamu wageni watao kuja kwa msimu kwa gharama zao kuja kutoa huduma za afya nchini na pia kupata kuungana na taasisi zingine za dunia zitazounga mkono Taasisi yetu.
8.Viongozi waipe hadhi NIHF. kwa kutoa zawadi za vifurushi ya BIMA ya NIHF na kwa kutoa misaada ya vifurushi vya BIMA ya NIHF. Hii itaipandisha hadhi katika jamii mfano kama Mbunge, Waziri, Mkuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa na wengine katika eneo lake anaweza toa lifurushi kwa wanamichezo, watu wenye mahitaji maalumu au mtu fulani aliyefanya tukio fulani nchini lenye tija na kuhamasisha makampuni yaliowekeza katika eneo lake kufanya hivyo.
Naamini kwa haya mawazo, Wizara na Taasisi husika lengwa wanaweza kutatua changamoto za mfuko wetu wa BIMA NIHF nchini.
Na mmmuhumba
0624 440 454
 
ELIMU WAKATI TULIONAO NA TUENDAPO

Kwa nchi nyingi za Afrika, elimi ni kurithisha maarifa, stadi na ujuzi kwa mwanafunzi katika eneo maalumu. Hata katika jadi ilikuwa ni hivyo hivyo ambapo walirithisha ujuzi, maarifa na stadi kwa vijana kwa kuzingatia umri na jinsia...
Makini muhim kusomwa
 
Ukiwa ni mdau wa elimu, utajifunza haya yaliyopo ni tija katika kujenga
1. Hamasa ya watumishi
2. Kuthibiti ubora
3. Kuleta elimu tegemezi na shindani
4. Kuboresha ufundishaji unazingatia umahili wa kutumia zana na vifaa
5. Kuleta maisha yenye starehe kwa watanzania, kumaliza wakiwa na umri mdogo na kuingia katika mfumo wa uzalishaji mali wakiwa wadogo.
6. Kuongeza wataalamu wenye moyo na wanachokifanya.
7. Kuendeleza vipaji na sanaa kwa ajili ya kufungua milango ya watanzania wachache kuwaza kuanzisha kitu kitachozalisha ajira.
8. Kuendana na wakati soko la ajira na upeo wa binadamu.
 
CCM inatengeneza kundi kubwa la wajinga wenye vyeti vya kuhitimu
 
Back
Top Bottom