Elimu sio vyeti, elimu ni utendaji

Elimu sio vyeti, elimu ni utendaji

Wewe nani?
Itakuwa tumezoeshwa kupima vibaya na kutegemea vyeti.
Fundi gari asiye na vyeti ni ufanisi kuliko kwenye vyeti.

Mtofautishe anayejua kuendesha baiskeli na asiyejua.
mimi zipompa,

mkuu una mifano ya kitoto kweli mpaka nimeshangaa.
 
Elimu ni uwezo wa kuyakabili mazingira na kuboresha maisha kwako na jamii.

Aliyeelimika ni yule anayeweza kujua hilo na kulitekeleza katika maisha yake kwa kiwango chake.

Maana yake, mtu mwenye uwezo wa kuelimika kwa 50% (kwa sababu za kibaiolojia kwa mfano) akajielimisha kama mtu mwenye uwezo wa kuelimika 70%, na kuelimika 90%, halafu akaitumia elimu yake kusaida 95% ya jamii yake atakuwa kaelimika maradufu ya mwenye uwezo wa kuelimika 90% (kwa sababu za kibaiolojia kwa mfano) akajielimisha 70% na kuelimika 50%, halafu akaikandamiza 95% ya jamii yake.

Nilipofika tu Marekani, kitu kimoja kilichonifanya niwaheshimu Wamarekani ni kumuona mtu mwenye clear "Down Syndrome" (Kiswahili nafikiri ni aina ya uzezeta) anafanya kazi vizuri Supermaket na anpendwa na kuheshimiwa na jamii iliyomzunguka, Nilishangaa hawa watu vipi?

Kumbe hiyo ni sababu moja anatushinda. Wanataka kutumia uwezo wa kila mtu.

Hawaamini kwamba yule mtu mwenye mtindio wa akili, yule mwenye Down Syndrome, hana mchango kwa jamii. Wote wanapewa kazi, wote wanapata kazi. Mtu anayetaka kufanya kazi anapat kazi.

Kazi ni haki.Ya kikatiba. Sasa kama mtu hana kazi afanye nini? Afanye jinai? Aibe na kukaba? Afe kwa njaa?

Mfano.

Unaweza kuwa na akili zote za vyeti vya dunia hii, lakini kama huna akili ya kujua ubinafsi uliokithiri ni mbaya na kutaka kujilimbikizia mali kwa kusaini mikataba mibaya kutaharibu maisha ya wengi, pamoja na vizazi vyako vijavyo, bado hujaelimika.

Na anaweza kuja mjinga mmoja asiye na cheti chochote, ambaye hata kusoma hajui, hajasoma vitabu vingi, lakini yeye anapanda miti ya matunda ambayo haitazaa matunda katika maisha yake, lakini anajua kwamba siku moja vizazi vijavyo vitakula matunda hayo, mtu huyu, anaweza kuwekwa katika mizani ya cross multiplication za "Noblesse Oblige" na mtu kupimwa kwa talanta alizopewa, mtu huyu akaonekana ameelimika zaidi.

Nilivyokwenda kwenye interview yangu ya kazi baada ya Chuo, nilikuwa najiamini sana. Nilikuwa nimepata maksi za juu kabisa katika darasa langu. Shuleni kila mtu darasani alikuwa ananifuata mimi, kuanzia programming mpaka presentations. Matokeo yalivyotoka nikatokea nimeongoza. Sio chuo cha kitoto, Uingereza hapo, 1999. Dot com boom iko in full effect.

Nikaitwa interview ya kwanza. Kila kitu kime check. Kampuni kubwa ya dot com. Mambo hayo nimesomea na kuyapiga kisawasawa. Tatizo moja tu, nilikuwa sina uzoefu wa muda mrefu zaidi ya ku volunteer kufundisha watoto kutumia computer wakati niko chuoni.

Nikafika kwenye interview. The most expensive building in The City. Kila ninapoenda nafunguliwa milango.

Nimeenda kwa CEO. Kapewa habari zangu Kipanga nakuja. Kabla sijakutana naye nimekutana na vipanga wenzangu wa zamani. Watu wamesoma motherboard ya kompyuta hata ukiwaamsha usiku wa manane wanaweza kukuchorea circuits zilivyoenda, wananiuliza maswali yote nawajibu sawa.

Nikakutana na CEO. Kanizungusha huku kule kuangalia lugha na saikolojia yangu kanikuta niko fit. Na flow kama Niagara.

Akaniuliza swali moja mpka leo nalikumbuka.

Hapo kashika vyeti vyangu ana admire nilivyo perform. Hana swali la kuuliza kuhusu vyeti. Maana nimepasua kisawasawa.

Akaniuliza swali moja sikulitegemea. Kwa sababu nilitegemea baada ya vyeti vile anipigie ngoma tu na kunilamba miguu.

Aliniuliza, nitaaminije kwamba uwezo wako unaoonekana kwenye karatasi unaweza kuja kuwa sawa na uwezo wako wa kiutendaji? Maana kuna wengi wenye uwezo wa kimakaratasi lakini ukiwaweka kwenye kazi wanapwaya?

Sikuwa na jibu zuri moja kwa moja kuonyesha uwezo wangu, kwa sababu nilikuwa ndo kwanza natoka shule.

Nikamwambia, ndiyo kwanza natoka shule, lakini nishakaa na watu, nishafundisha watoto, natoka kwenye mstari mrefu wa Engineers wanaojua na walionifundisha kuhusu mambo ya kompyuta kwa miaka mingi sana, nacheza chess na najua chess moves zinavyotaka kufikiri far ahead, na sioni ni vipi nitashindwa kufikia matakwa ya job decsription kama yalivyoandikwa.

Nikapata barua ya kualikwa kuanza kazi bila utata na bosi akawa ananitegemea sana.

Niliingia kwenye chumba cha interview nikiwa naamini kwamba sitatakiwa kujieleza sana, kwa sababu nilipasua mitihani karibu yote. Niliamini sana makaratasi yangu.

Usaili ule ulinifanya nielewe kwamba, kuwa na qualifications zote zinazotakiwa kimakaratasi is the bare minimum. Maswali ya usaili yalinifanya nijue kwamba kuna performance iliyo zaidi ya makaratasi inayotakiwa katika day to day performance in the workplace.
Nimekukubali kitu kimoja,,,japo umekaa nje au kusoma nje kwa muda kiasi lakin hujaweka "you know"nyiiingi kwenye bandiko lako...saf sana
 
Siwatetei hao ambao hawana vyeti
Naangalia Fikra ya nani aliyeelimika na mwenye elimu.

9000 je walitenda kwa ufanisi?

Mtu awezakuwa na vyeti vingi lakini akashindwa na aside na cheti au mwenye cheti feki. Walijua hilo?
Elimu ya taifa lako ni cheti, ndio maana kigezo cha kuajiriwa popote ndani humu uzoefu/utaalam sio kigezo cha msingi.

Mwenye cheti chenye alama za juu zaidi ndiye mwenye elimu zaidi, kwanini watu wasiache vyeti vyao halari wanunue/wachonge vyenye ujazo???
 
katika upimaji tuna angalia utendaji, ila huwezi fikia utendaji ukiwa huna vyeti. vyeti ndio msingi wa kupata kazi, hakuna namna ya kumtambua mtendaji mzuri ikiwa ujampa kazi
Unajua kwanini waliofaulu vizuri wanakuwa na hali mbaya sana wanapokosa kupewa ajira.
 
Hili ni swami muhimu sana
=elimu ni ujuzi unaoambatana na utendaji

Interviewer wengine wanakupeleka mpaka workstation kuprove vyeti vyako.
Kikawaida wanaita kipindi cha kutazamwa he unaweza? = probation period

Probation period,zinafanywa na watu weupe bana, hapa bongo tunazinguana tu, mtu anapatia desa hapo hapo na anaendelea na kazi.probation period miezi 6 nani atashindwa kufikia maono ya waajiriwa wake??
 
Kwa ajira ya kwanza Cheti kina akisi "potentiality" lakini si "effort" na si "maadili". Haya mawili ya mwisho ambayo yako kwenye utendaji hufahamika mtu akiwa kazini. Kabla ya hapo tunakwenda na cheti ikiambatana na "interview" kuangalia nani huenda "akatufaa" kwenye jukumu fulani. Elimu ni kutmia ujuzi wako kupata matokeo uliyowekewa au aliyojiwekea katika mazingira fulani (ikiwa ni pamoja na sheria husika).
 
Unajua kwanini waliofaulu vizuri wanakuwa na hali mbaya sana wanapokosa kupewa ajira.
mkuu acha porojo zako wote wenye hali mbaya ni walio foji (wewe kuwaona kazini ukajua wamefaulu). kwa takwimu walio faulu kihalali kuwa na hali ngumu ni uzembe wake tu.

acha kuchanganya akiyefoji cheti na kupata nafasi ya kazi wewe kumuona kama aliye faulu.
 
mkuu acha porojo zako wote wenye hali mbaya ni walio foji (wewe kuwaona kazini ukajua wamefaulu). kwa takwimu walio faulu kihalali kuwa na hali ngumu ni uzembe wake tu.

acha kuchanganya akiyefoji cheti na kupata nafasi ya kazi wewe kumuona kama aliye faulu.
Sidhani kama umenielewa.

Namaanisha waliofaulu viwango vya juu, wasibahatike kupata kazi.
 
Nimekukubali kitu kimoja,,,japo umekaa nje au kusoma nje kwa muda kiasi lakin hujaweka "you know"nyiiingi kwenye bandiko lako...saf sana
Kiswahili, kwa kufuata mantiki ya sarufi, matamshi na sheria za lugha, kina mantikikubwa sana kukishinda Kiingereza.

Kwa mfano, katika matamshi,Kiswahili kinatamkwa kama kinavyoandikwa,ni nadra sana kupata neno la Kiswahili linatamkwa tofauti na linavyoandikwa.Ukijua mfumowamatamshi ya Kiswahili, hata ukikutana na neno hujawahi kuliona utajua kulitamka. Hili linafanya matamshi ya lugha yafuate mantiki zaidi kuliko lugha kama ya Kiingereza ambayo sheria za matamshi ziko shaghalabaghala na ukikutana na neno jipya matamshi mpaka ufundishwe kwa maana unaweza kufikiri vingine na matamshi yakawa vingine.

Vivyo hivyo, aghalabu Kiswahili hufuata sheria zake mara karibu zote, sehemu ambazo Kiswahilihuchepukakutoka katika sheria zake ni chache sana ukilinganisha na lugha kama Kiingereza ambayo nusu ya lugha inafuata sheria, na nusu nyingine ni kuacha sheria.

Kwa wasomi wa lugha wanaojua hanari za George Bernard Shaw alivyokichamba Kiingereza kwa kukosa mantiki wataelewa kwamba sio kwamba nasema haya kwa sababu Kiswahili ni lugha yangu tu, hata George Bernard Shaw, mtunga michezo ya kuigiza aliyepewa tuzo nyingi, zikiwamo Nobel na Academy Award(mtu wa kwanza kupewa tuzo hizo mtu mmoja)

Kwaanayetaka kuona jinsi George Bernard Shaw alivyokichana Kiingereza anaweza kuangalia hapa

Ghoti - Wikipedia

Basi tu kwa sababu za kihistoria Kiingereza kimekuwa na nguvu sana.

Lakini kwa uzuri wa lugha, Kiswahili kimekizidi Kiingereza sana.
 
Elimu ya vyeti haina maana sana, maana inasababisha watu wanatafuta njia yoyote ya kupata vyeti - iwe kwa kukariri au hata ku forge vyeti. Namna nzuri ya kupima usomi wa mtu ni uwezo wake wa kutenda (competency based). Practicals ndo zinatakiwa ziwe msingi wa elimu yetu. Unakuta mtu ana vyeti vyenye A's nyingi sana, lakini utendaji wake ni bure kabisa. Lakini unakuta mtu ana C's nyingi sana, lakini utendaji wake ni super kabisa. Kwahiyo mimi japo ninavyo, siamini sana katika vyeti maana vinadanganya sana. Siku hizi ajira za private sector lazima ufanye aptitude test kwa sababu wamegundua kuwa watu wengi wenye vyeti vizuri hawa perform katika kazi wanazopewa
 
ELIMU SIO VYETI, ELIMU NI UTENDAJI

wangapi wana vyeti lakini hawatendi? na wengine hawatendi vizuri?

what happen to the so called prof. muhongo and magu? this show that "action speak better than words"

tusiwaze sana vyeti kwenye ufanisi. UZOEFU NI MWALIMU MZURI


>>>>>> think +ve from now|||||||| ALL PEOPLE
 
Elimu ya taifa lako ni cheti, ndio maana kigezo cha kuajiriwa popote ndani humu uzoefu/utaalam sio kigezo cha msingi.

Mwenye cheti chenye alama za juu zaidi ndiye mwenye elimu zaidi, kwanini watu wasiache vyeti vyao halari wanunue/wachonge vyenye ujazo???
BECAUSE HAWAJIAMINI.
 
tutajuaje wewe unaweza kufanya kazi kama huna cheti? mfano .. wewe ukadai kwamba unaweza kufanya kazi kama daktari lazima uoneshe vyeti.. VYETI KWANZA.
 
Elimu ni ujuzi na maarifa alionao mtu ambao umsaidie kuishi maisha bora na kueza kuziondoa changamoto zinazomzunguka.
Ujuzi na maarifa tunaeza kuvipata kwa kusoma au kujifunza hii iwe unajifunza mwenyewe au shuleni, kutoka kwa wajuzi wa mambo fulani na kupitia vipaji vya kuzaliwa.

Na kipimo sahihi cha elimu ni ule uhalisia wako kwenye kutenda siyo vyeti, vyeti ni utambulisho tu lakini havina umuhimu wowote kama huna ule ujuzi unaokutambulisha kwa hivyo vyeti vyako.
Kama una ujuzi na maarifa hata usipokuwa na vyeti hutopata shida yoyote lakini kama huna ujuzi wa kutosha hapa lazima ujifiche kwenye vyeti.
Ukiwa na vyeti na ujuzi hata ukichoma vyeti vyako hamna shida.

Ndiyo maana wapo watu waliamua kuacha kuendelea kusoma vyuoni na kuamua kutumia ujuzi walionao na leo hii ni mabilionea wakubwa.
Hawa hawana vyeti na ukiwauliza vyeti watakushangaa sana.

Elimu ni ujuzi na maarifa uliyonayo na hivi vinaonekana kwenye kutenda na kupata matunda na mafanikio kwako na jamii inayokuzunguka hii haijalishi una cheti au hauna.
Tanzania wapo wasomi wengi wakiwamo maprofesa hawa wana vyeti lukuki na CV zao zinavutia sana utajisemea hakika hawa wame elimika lakini kiuhalisia watu hawa ni mizigo mikubwa kwa jamii sababu mavyeti yao na ma-CV yao ya kuvutia hayaendani na utendaji na mchango wao kwenye maendeleo ya taifa au ni wana vyeti lakini hawakuelimika.

Ukiwa na cheti na ujuzi ni heri sana na ni heri pia ukiwa na ujuzi bila cheti sababu hakuna shida utapata, lakini shida ni pale una cheti ujuzi hauna na hapa ndiyo wanaojiita wasomi wengi Tanzania wamejaa kwenye kundi hili na mfumo wa elimu Tanzania unazalisha wahitimu wenye vyeti vizuri sana ujuzi hawana sasa hii ni janga la taifa.

Si ajabu kuona yule aliyehitimu fani ya computer engineering chuo Tanzania hajui CPU ya komputa ikoje, na tena si ajabu kuona cheti cha muhitimu huyo asiyeijua CPU ya komputa kinaonesha amefaulu kwa kiwango cha juu kabisa huko chuoni eti ni 'kipanga'.
 
Back
Top Bottom