Elimu sio vyeti, elimu ni utendaji

mbm

JF-Expert Member
Apr 25, 2011
604
286
Jiamini, Jitambue Kuwa mbunifu

Elimu ni nin?
Nani aliyeelimika?

Utendaji kwa ufanisi na matokeo mazuri ya ulichotenda ndio kipimo cha mtu aliyeelimika.

Kuwa na vyeti vingi haisaidii kama hutendi kwa ufanisi. Itakuwa ni fashion tu.
Kusoma sana kunatakiwa kukusaidie sana katika ufanisi ukitenda?

Ombi ukichangia anza na kujibu hayo maswali. Tunapima je ?Umeelimika au unacheti!!
 
Elimu ni ujuzi ulioambatana na utendaji.
Ujuzi unaupataje?
Ntajuaje unaujuzi? Angalia utendaji wangu!
 
Nyie ndio watu mnaofanya tunamdharau baba nashite,

Kama kigezo ni utendaji, hawa 9000 walikuwa wanalala ofisini au hawaingii kabisa??!
Siwatetei hao ambao hawana vyeti
Naangalia Fikra ya nani aliyeelimika na mwenye elimu.

9000 je walitenda kwa ufanisi?

Mtu awezakuwa na vyeti vingi lakini akashindwa na aside na cheti au mwenye cheti feki. Walijua hilo?
 
Jiamini.jitambue.kuwa m bunifu

Elimu ni nin?
Nani aliyeelimika?

Utendaji kwa ufanisi na matokeo mazuri ya ulichotenda ndio kipimo cha mtu aliyeelimika.

Kuwa na vyeti vingi haisaidii kama hutendi kwa ufanisi. Itakuwa ni fashion tu.
Kusoma sana kunatakiwa kukusaidie sana katika ufanisi ukitenda?

Ombi ukichangia anza na kujibu hayo maswali.

Elimu ni uwezo wa kuyakabili mazingira na kuboresha maisha kwako na jamii.

Aliyeelimika ni yule anayeweza kujua hilo na kulitekeleza katika maisha yake kwa kiwango chake.

Maana yake, mtu mwenye uwezo wa kuelimika kwa 50% (kwa sababu za kibaiolojia kwa mfano) akajielimisha kama mtu mwenye uwezo wa kuelimika 70%, na kuelimika 90%, halafu akaitumia elimu yake kusaida 95% ya jamii yake atakuwa kaelimika maradufu ya mwenye uwezo wa kuelimika 90% (kwa sababu za kibaiolojia kwa mfano) akajielimisha 70% na kuelimika 50%, halafu akaikandamiza 95% ya jamii yake.

Nilipofika tu Marekani, kitu kimoja kilichonifanya niwaheshimu Wamarekani ni kumuona mtu mwenye clear "Down Syndrome" (Kiswahili nafikiri ni aina ya uzezeta) anafanya kazi vizuri Supermaket na anpendwa na kuheshimiwa na jamii iliyomzunguka, Nilishangaa hawa watu vipi?

Kumbe hiyo ni sababu moja anatushinda. Wanataka kutumia uwezo wa kila mtu.

Hawaamini kwamba yule mtu mwenye mtindio wa akili, yule mwenye Down Syndrome, hana mchango kwa jamii. Wote wanapewa kazi, wote wanapata kazi. Mtu anayetaka kufanya kazi anapat kazi.

Kazi ni haki.Ya kikatiba. Sasa kama mtu hana kazi afanye nini? Afanye jinai? Aibe na kukaba? Afe kwa njaa?

Mfano.

Unaweza kuwa na akili zote za vyeti vya dunia hii, lakini kama huna akili ya kujua ubinafsi uliokithiri ni mbaya na kutaka kujilimbikizia mali kwa kusaini mikataba mibaya kutaharibu maisha ya wengi, pamoja na vizazi vyako vijavyo, bado hujaelimika.

Na anaweza kuja mjinga mmoja asiye na cheti chochote, ambaye hata kusoma hajui, hajasoma vitabu vingi, lakini yeye anapanda miti ya matunda ambayo haitazaa matunda katika maisha yake, lakini anajua kwamba siku moja vizazi vijavyo vitakula matunda hayo, mtu huyu, anaweza kuwekwa katika mizani ya cross multiplication za "Noblesse Oblige" na mtu kupimwa kwa talanta alizopewa, mtu huyu akaonekana ameelimika zaidi.

Nilivyokwenda kwenye interview yangu ya kazi baada ya Chuo, nilikuwa najiamini sana. Nilikuwa nimepata maksi za juu kabisa katika darasa langu. Shuleni kila mtu darasani alikuwa ananifuata mimi, kuanzia programming mpaka presentations. Matokeo yalivyotoka nikatokea nimeongoza. Sio chuo cha kitoto, Uingereza hapo, 1999. Dot com boom iko in full effect.

Nikaitwa interview ya kwanza. Kila kitu kime check. Kampuni kubwa ya dot com. Mambo hayo nimesomea na kuyapiga kisawasawa. Tatizo moja tu, nilikuwa sina uzoefu wa muda mrefu zaidi ya ku volunteer kufundisha watoto kutumia computer wakati niko chuoni.

Nikafika kwenye interview. The most expensive building in The City. Kila ninapoenda nafunguliwa milango.

Nimeenda kwa CEO. Kapewa habari zangu Kipanga nakuja. Kabla sijakutana naye nimekutana na vipanga wenzangu wa zamani. Watu wamesoma motherboard ya kompyuta hata ukiwaamsha usiku wa manane wanaweza kukuchorea circuits zilivyoenda, wananiuliza maswali yote nawajibu sawa.

Nikakutana na CEO. Kanizungusha huku kule kuangalia lugha na saikolojia yangu kanikuta niko fit. Na flow kama Niagara.

Akaniuliza swali moja mpka leo nalikumbuka.

Hapo kashika vyeti vyangu ana admire nilivyo perform. Hana swali la kuuliza kuhusu vyeti. Maana nimepasua kisawasawa.

Akaniuliza swali moja sikulitegemea. Kwa sababu nilitegemea baada ya vyeti vile anipigie ngoma tu na kunilamba miguu.

Aliniuliza, nitaaminije kwamba uwezo wako unaoonekana kwenye karatasi unaweza kuja kuwa sawa na uwezo wako wa kiutendaji? Maana kuna wengi wenye uwezo wa kimakaratasi lakini ukiwaweka kwenye kazi wanapwaya?

Sikuwa na jibu zuri moja kwa moja kuonyesha uwezo wangu, kwa sababu nilikuwa ndo kwanza natoka shule.

Nikamwambia, ndiyo kwanza natoka shule, lakini nishakaa na watu, nishafundisha watoto, natoka kwenye mstari mrefu wa Engineers wanaojua na walionifundisha kuhusu mambo ya kompyuta kwa miaka mingi sana, nacheza chess na najua chess moves zinavyotaka kufikiri far ahead, na sioni ni vipi nitashindwa kufikia matakwa ya job decsription kama yalivyoandikwa.

Nikapata barua ya kualikwa kuanza kazi bila utata na bosi akawa ananitegemea sana.

Niliingia kwenye chumba cha interview nikiwa naamini kwamba sitatakiwa kujieleza sana, kwa sababu nilipasua mitihani karibu yote. Niliamini sana makaratasi yangu.

Usaili ule ulinifanya nielewe kwamba, kuwa na qualifications zote zinazotakiwa kimakaratasi is the bare minimum. Maswali ya usaili yalinifanya nijue kwamba kuna performance iliyo zaidi ya makaratasi inayotakiwa katika day to day performance in the workplace.
 
Elimu ni vyeti halali , kufuata utaratibu , na miongozo .
Tusipo kemea vyeti feki Kwa nguvu zote tutavuruga utaratibu,
Wizara zi pige kazi.
 
katika upimaji tuna angalia utendaji, ila huwezi fikia utendaji ukiwa huna vyeti. vyeti ndio msingi wa kupata kazi, hakuna namna ya kumtambua mtendaji mzuri ikiwa ujampa kazi
 
Comments zako ziko poa
Sasa una miaka mingapi kwenye field aka kazini?

Mwalimu Experience anakufundisha nini sasa hivi
 
Aliniuliza, nitaaminije kwamba uwezo wako unaoonekana kwenye karatasi unaweza kuja kuwa sawa na uwezo wako wa kiutendaji? Maana kuna wengi wenye uwezo wa kimakaratasi lakini ukiwaweka kwenye kazi wanapwaya?
Hili ni swami muhimu sana
=elimu ni ujuzi unaoambatana na utendaji

Interviewer wengine wanakupeleka mpaka workstation kuprove vyeti vyako.
Kikawaida wanaita kipindi cha kutazamwa he unaweza? = probation period
 
Elimu ni uwezo wa kuyakabili mazingira na kuboresha maisha kwako na jamii.

Aliyeelimika ni yule anayeweza kujua hilo na kulitekeleza katika maisha yake kwa kiwango chake.
Utayakabili mazingira Vipi bila kutenda? tena kwa ufanisi?
So
Ujuzi+Utendaji+Ufanisi= elimu
 
katika upimaji tuna angalia utendaji, ila huwezi fikia utendaji ukiwa huna vyeti. vyeti ndio msingi wa kupata kazi, hakuna namna ya kumtambua mtendaji mzuri ikiwa ujampa kazi
Wewe nani?
Itakuwa tumezoeshwa kupima vibaya na kutegemea vyeti.
Fundi gari asiye na vyeti ni ufanisi kuliko kwenye vyeti.

Mtofautishe anayejua kuendesha baiskeli na asiyejua.
 
Vyeti ni nyenzo inayokutafsiri ulicho soma lakini haioneshi utendaji
 
Elimu ni vyeti halali , kufuata utaratibu , na miongozo .
Tusipo kemea vyeti feki Kwa nguvu zote tutavuruga utaratibu,
Wizara zi pige kazi.

Naunga mkono sana vita vya vyeti feki.
Je wenye vyeti wanatendakwa ufanisi?
Sasa tufanyeje watende kwa ufanisi?

Je elimu inapatikana popote au mpaka chuo au shule tena darasani? Kwani kwenye daladala hupati elimu?
 
Vyeti ni msingi,vyeti ndio vinavyoonyesha kama umeelimika au la, then wakitaka kuprove vyeti vyako wata kuweka kwenye majaribio ya vitendo au wataangalia ufanisi wako wa kazi.

(MTOA MADA KAMA UMETUMBULIWA POLE,ILA NEXT TIME FUATA VIGEZO NA MASHARTI)
 
Back
Top Bottom