Pana tajiri mmoja Mkubwa sana Nigeria ni motivation pia kuhusu ujasiliamali na mafanikio.Baada ya kumaliza masters ya uchumi UK akarudi nigeria amesaka ajira kwa miaka 10 bila mafanikio na kupelekea kukata tamaa kabisa ikampelekea kwenye ulevi wa pombe chafu akiwa kapoteza kabisa matumaini.Pombe uunganisha urafiki hasa mkikutana vilabuni,akapata rafiki ambae ni mlevi mwenzake wakawa wanaishi wote maana hata uwezo wa kodi hakuwa nao.Yule mlevi aliishi kwa kutegemea kusukuma torori mjini lagosi kubebea watu mizigo uhakika wa kipato utegemea na wingi wa Kazi akipata utumia yote kesho atapata zingine,yule mlevi akawa akimshwishi mchumi waende wakasukume wote mkokotoni kuliko kukaa ndani bila Kazi,kwa shingo upande na hana jinsi mchumi ikabidi aweke masters pembeni akashika torori aibu pembeni asife njaa ajira zimegoma.Wakawa wanaenda wote aibu ikamtoka Kazi ikaingia damuni maana hel ya kula na kulewa sio shida tena uhakika upo, baada ya uzoefu na kuijua Kazi mchumi akaamua kusave akipata utumia robo zingine anasave bank alifanya Kazi ya torori na kusave ndani ya mwaka kwenda kuchungulia akaunti bank hakuamini pesa aliyoikuta ndo akafanya mtaji wa kuanzia kufungua biashara sababu uzoefu wa kuwabebea wafanyabiashara mizigo akafungua duka lake likafanya vizuri plus uchungu na nidhamu ya Kazi na hofu ya kurudi chini kwenye ulevi akafanya vizuri biashara ikakua akafungua maduka mengine na mengine mtaji ukakua akaanza biashara za kuchukua vitu nje ya nchi vinapotoka na kuuza kwenye maduka yake akajenga magodauni ya mizigo akawa ajenti Mkubwa na kuzidi kufungua biashara tele tele zikampa utajiri Mkubwa saana Nigeria.
Funzo hapa tunaona Masters holder amechanganya elimu mbili ya darasani kujua umuhimu wa saving na hofu ya kesho akiwa mgonjwa au mzee je ataendelea kusukuma torori?
Point kubwa hapa ni kwamba wengi waliokwenye hizi shughuli ndogo ndogo hawazioni Kama ni fursa wanazoweza zikuza Ili waje wawe wafanyabiashara wakubwa kupitia savings.
Hizi shughuli zenye kudharauliwa na wengi ukizifanya kwa malengo ni rahisi kufikia malengo yako.