Unachosema Mkuu Mr Rocky ni kweli kabisa, lakini pamoja na kuwa watoto wao ambao ni asilimia ndogo sana ya Watoto wa Tanzania hawasomi katika shule hizo lakini hakuna sababu yoyote ya kuiacha Elimu nchini ianguke kiasi hiki. Wanabwabwaja kwa dakika chache mjengoni kisha hakuna lolote la maana linalofanyika na huku elimu ikiendelea kuporomoka.
Mbatia aache utani.......
Nina mtihani wa majaribio wa darasa la saba ambao haufanyiki. Niliwahi kumpa profesa mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye alitumia saa mbili na nusu bila kupata jibu lolote la kuandika. Mtihani wenyewe haufanyiki, alisema Mbatia na kutoa ofa ya Sh10 milioni kwa profesa mwingine yeyote bungeni ambaye ataweza kufanya mtihani huo na kupata alama 100.
Mkuu BAK nani anayewaza hayo kwamba kuna mtoto wa mlala hoi kule chunya au kasulu ambaye anakalia jiwe au hana kitabu cha kiada au hana mwalimu wa kumfundisha au shule yake haina maabara
Wewe ndio unaona uchungu na elimu yetu ila waliokalia viti vya kunesa na kupigwa na kiyoyozi watoto wao wako shule za St nanihii na International School au wako Malaysia au South Africa au Uk wanasoma au wakiwa hapa bongo wako Feza au Tusiime na sio shule ya kijijini kwako ambako mwalimu akifuata mshahara shule inafungwa mpaka arudi
Bungeni mimi naitaga comedy maana hakuna wanachojadili wanapiga makofi na kugonga meza hata kwa upuuzi au kwa porojo za mchakato sijui tuko kwenye mpango ambako hizo comedy tumezisikia toka tunajua kuwa kuna bunge
And then viongozi wako kwenye ziara wanafuatilia utekelezaji wa ahadi na ilani za chama na kuangalia namna wanafunzi wanavyokaa chini kwenye vumbi wakati makampuni yao yanashindana kusafirisha mbao na magogo nje ya nchi kupata fedha za kigeni
Halafu BAK unajua ni aibu mbao zinatoka mikoani huko ila huko ndio kunaongoza kwa watoto kukaa kwenye mawe na sakafuni
muheshimiwa supika jimbo langu lina matatizo kede kede ya elimu watoto hawana madawati vitabu havitoshi kwingine hakuna kabisa walimu nao ni tatizo kwan kuna shule nying jimbon kwangu zina upungufu mkubwa wa walimu. Lakini mh waziri naomba nikuhakikishie kuwa naunga mkono bajeti asilimia mia moja(100% ) makofi pwa! Pwa! Pwa! Pwa!
Sijui tumefanikiwa kwenye nini?
huwa natamani sana kusikiliza Bunge la budget, lakini kila ninapokuwa kwenye hiyo channel nashitukia tu nimeshabadilisha na kuingia kwenye FOOD!Bunge letu ni Bunge lililojaa usanii wa hali ya juu. Kinachoendelea pale mjengoni kinasikitisha sana.
huwa natamani sana kusikiliza Bunge la budget, lakini kila ninapokuwa kwenye hiyo channel nashitukia tu nimeshabadilisha na kuingia kwenye FOOD!
Bora kujifunza kupika kuliko kusikiliza mapato na matumizi ya nchi yangu...... shame!
mbatia ana akili kidogo
mbatia ana akili kidogo
mbatia anajitahidi
Mnachagua wakwere kuongoza nchi halafu mnategemea nini. Mpaka hapo mtakapokubali kutawaliwa na watu wenye akili ndiyo mtaendelea
Kila kitu kiko hoi. Sio elimu, afya, maji, na miundombinu (usafirishaji per ce). Mgonjwa wa kufa huyu, hata drip haiendi!
mbatia ana akili kidogo
Hiyo ndio tofauti ya Mbatia na Lema. Wote si mawaziri vivuli, ila Mbatia anajua nini anafanya ila Lema ni box tupu limepewa nafasi kwasababu ni kabila moja na Mbowe.