Elimu kwenye Taifa letu...

Elimu kwenye Taifa letu...

mwananchit

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2008
Posts
242
Reaction score
298
Elimu hasa kwenye shule zetu za umma iko taabani, viwango vya elimu vinashuka, shule zetu zimegeuka kuwa viwanda vya kuzalisha ujinga. Uwezo wa wahitimu kuchambua mambo na kujenga hoja sio wa kuridhisha, na suala zima la ubunifu na uwajibikaji limekuwa hafifu. Kuna ongezeko la wasiojua kusoma na kuandika achilia mbali uwezo wa kuongea lugha za kimataifa ambazo zinatumika kufundishia. Ubunifu wenye tija kwenye nyanja karibia zote umekuwa adimu hivyo kuzidi kuchangia ongezeko la umaskini kwenye taifa letu.

Nini chanzo chake?

Nini kifanyike? (hapa tuchambue kwa mapana)

Naomba kuwasilisha.
 
Hii inaongeza ubaguzi ktk taifa letu, na wigo wa madaraja baina ya Watanzania. Hali inazidi kuwa mbaya zaidi maana siku hizi tuna shule za Wahindi (Indians School ), Shule za Waarabu (Yemen School ), yaani nashangaa hizi shule zimewezaje kupata usajili maana tulishatoka huko lkn sasa tunarudi huko kwa kasi ya kutisha na muda si mrefu tutakuwa na Chaga schools na Nyamwezi schools.

Vv
 
Back
Top Bottom