Elimu kwa Umma - Mkoa wa Morogoro

Joined
Mar 27, 2025
Posts
33
Reaction score
45
Baraza la Famasi kwa kushirikiana na Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma, Wizara ya Afya limeendelea na zoezi la kuelimisha umma kuhusu kazi na majukumu ya Baraza pamoja na kuhamasisha jamii juu ya matumizi sahihi ya dawa.

Kampeni hii iliyoanza juzi, imeendelea tarehe 06 Mei, 2025 katika Mkoa wa Morogoro na imeweza kufikia wananchi wengi zaidi kwa kutoa elimu katika Kituo cha bajaji na bodaboda cha Juwata, Soko la Mawenzi na Stendi Kuu ya mabasi ya Mkoa (Msamvu).

Aidha, katika zoezi hili jamii imepata wasaa wa kuuliza maswali na kupata majibu ya papo hapo ili waweze pia kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa.

“Nimeelimika na nitazingatia Matumizi Sahihi ya Dawa

 

Attachments

  • IMG_2696.jpeg
    1.2 MB · Views: 26
  • IMG_2684.jpeg
    649.9 KB · Views: 30
  • IMG_2693.jpeg
    1.2 MB · Views: 29
  • IMG_2702.jpeg
    1.2 MB · Views: 24
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…