Ndg wana JF, tukiwa bado tunaangalia sakata la matokeo mabovu ya CSEE 2012, ambapo MaCCM yameendelea kuonyesha utendaji mbovu kwa kufuta matokeo hayo( nasema mbovu kb mpaka matokeo yanatangazwa kikao kilikaa Mwenyekiti akiwa Kawambwa, makamu akiwa Mulugo-kilaza, katibu akiwa Katibu Mkuu Moevt(Gesimba) na wajumbe wakiwa watendaji wa NECTA. Leo hii wanajifanya maamuzi yale yalifanywa na necta wakati saini zao zipo. Kudhihirisha kuwa siasa inaharibu elimu yetu, watendaji wakuu( curriculum implementers katika ngazi zote- waalimu wa msingi, sekondari na vyuo vya ualimu hawatimiziwi mahitaji yao kutokana na kauli za kisiasa.
Mfano mzuri ni siku Kamati ya Bunge ya Huduma za jamii ilipotembelea Moevt na bila aibu Waziri Kawambwa kamwambia Mkti mama Sitta kuwa waalimu wameshalipwa madai yao yote, walipobanwa Naibu Waziri karukia Kuwa Hatuwezi kuwalipa kwa kuwa hawana viambata vya madai yao. Walipotoa majibu hayo wiki moja ya nyuma yake Waziri , naibu Waziri, ACCOUNTANT General wa Wizara walikuwa na kikao na wakuu wa shule/vyuo na kuwaambia kuwa wamelipa watu 3 kati 740 madai mbalimbali.Na AG akasema madai hayo yanashughulikiwa Utumishi ati nae hajui kwa nini inakuwa hivyo. Je kwa nini kuwe na majibu tofauti kiasi hiki kwa watu wanaofanya kazi ofisi moja? na je kwa nini umma udanganywe hivyo wakati wakufunzi wanadai madeni mengine ya tangu 2006-mishahara , arreas , likizo, masomo , matibabu n.k?
Kwa kuwa ukweli wa suala hili wanalo waalimu wenyewe, napendekeza Waziri Kivuli wa Elimu atembelee vyuo vya Ualimu apate data kamili za madai ya walimu na kwa pamoja WAONDOE SHILINGI wakati wa kusoma Bajeti tarehe 27. Kusimamia ishu ya grading system kama ndio chanzo pekee cha kufeli wanafunzi ni kupotosha umma na hatua stahiki zisipochukuliwa "tutavuna mabua"
Kambi ya Upinzani tunawaamini sana mseme mseme mseme-Christowaja Mtinda komaa kama vipi bungeni hutarudi
(mods tafadhali uache huu ukweli ujulikane kwa watu)