Salaam,
Wakuu tujuzane kuhusu kuzitambu hizi pesa bandia.
Jana kuna raia kanipa, akihitaji bidhaa ya Tsh 500,
Haraka nilimuonya aache huo ujanja,
Alishangaa, nikamwambia fedha hyo si halali,
Kumbe naye kaliwa sasa anajaribu kushika masikio ya watu.
Nikamwambia ushatapigwa.
Siku moja kuna dada mdogo wangu alitoa 40,000 kupitia simu,
Sasa akasafiri mbali na kutaka kununua bidhaa, alihudumiwa ghafla mwenye duka alimfuata, akamwambia pesa hii si halali,
Kumbe muuza hakushtuka mapema mana ilikuwa mpya (hivyo hata dogo hakushtuka before)
Aliicheck akaichana tu na akampa nyiingine,
Vipande hivyo alivihifadhi, nilivyoviona, mimi pia niliacema mbona ni fedha halali tuu,
Kuangalia SAINI YA GAVANA, zinatofautiana na fedha zote kama 2000. 500. 1000 na 50000
Hiyo ndo imenifanya ukinipa noti ya 10000 mtaani kama sio benki, nakimbilia kuangalia saini ya gavana,
JE? MBONA ZINA UTEPE NA WATER MARK KAMA FEDHA HALALI
JE IPI MBINU AU TOFAUTI NYINGINE YA PESA BANDIA NA ZILE HALALI?
JE KUNA FEDHA BANDIA ZA THAMANI NYINGINE KAMA 5000. 2000 NK?
Asanteni.