Elimu kuhusu Computer engineering, uliza swali lolote

Elimu kuhusu Computer engineering, uliza swali lolote

edneltz

Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
44
Reaction score
25
Napenda kuchukua nafasi hii kutoa elimu kuhusiana na hii course ya computer engineering maana ninaona wengi humu JamiiForums na hata wanafunzi wanaosoma hawaielewi na wanaichanganya na IT, COMPUTER SCIENCE.

Computer engineering ni zao la electrical engineering pamoja na computer science. Hivyo basi katika computer engineering vitu vifuatavyo husomwa. Electronics, automation, programming, network, instrumentation, control systems, communication systems etc.

Sasa kuna watu pia hata wanafunzi wanaosoma wanajua computer engineering ni kutengeneza computers ambacho sio kweli, wao wanadeal na how electronics inaunganishwa na programming pamoja na knowledges za computer.

Nawasilisha, mwenye swali lolote aulize nipo kwa kujibu.
 
Kwani hao wanaobishia ukweli huu, wewe unadhani wameisoma hiyo kozi?
Kama wataendelea kubishia ni hatua gani utawachukulia ikiwa elimu umewatolea na wao ubishi ndio jadi yao?
 
Kwani hao wanaobishia ukweli huu, wewe unadhani wameisoma hiyo kozi?
Kama wataendelea kubishia ni hatua gani utawachukulia ikiwa elimu umewatolea na wao ubishi ndio jadi yao?[/Q
Mimi ninatoa elimu tu na uelewa kwa watu.sio kwa ajili ya wanaobisha
 
Ulichoongea ni kweli lakin jiulize ni CE wangapi wana deal na actual programming plus electronics?? Wengi wanaishia kutengeneza websites tena kwa wordpress na drupal!!
 
Ulichoongea ni kweli lakin jiulize ni CE wangapi wana deal na actual programming plus electronics?? Wengi wanaishia kutengeneza websites tena kwa wordpress na drupal!!
Hilo ni tatizo ambalo tunalo Tanzania, kama kweli wangekuwa wanacomputerize hardware hakika Tanzania ingefika mbali kiteknlojia
 
Hizi kozi bila kujiongeza utaishia kupack vyeti kwenye kabati
 
Hizi kozi bila kujiongeza utaishia kupack vyeti kwenye kabati
Kwani vyeti ndo vinafanya kazi?.au knowledge uliyonayo? Cha msingi uwe na uelewa na ulichokisoma na uweze kurelate na maisha yanayokuzunguka hapo utawin
 
Degree nyingi wanachuo wanasoma tu,ila hawajui future yao
 
Elimu yetu kwa sehemu kubwa ni ya kujipatia vigezo vya kuajiriwa tu na sio kupata uelewa na kujifunza kuitumia ipasavyo kwenye maisha.

Inakua kazi kutofautisha msomi na asiyesoma hadi mtu anaposema ana vyeti.
 
Computer engineering kwa nchi za wenzetu wengi wanafanya kazi kwebye viwanda vya simu, computers, haswa upande wa hardware design.
Huku tz hatuna miundo mbinu inayo support hii course. Ndio maana watu wengi wa CE Wanaishia kufanya kazi na CS, IT.
 
Napenda kuchukua nafasi hii kutoa elimu kuhusiana na hii course ya computer engineering maana ninaona wengi humu jamii forums na hata wanafunzi wanaosoma hawaielewi na wanaichanganya na IT,COMPUTER SCIENCE.
Computer engineering ni zao la electrical engineering pamoja na computer science. Hivyo basi katika computer engineering vitu vifuatavyo husomwa.
-electronics, automation,programming, network, instrumentation, control systems, communication systems etc.
Sasa kuna watu pia hata wanafunzi wanaosoma wanajua computer engineering ni kutengeneza computers ambacho sio kweli,wao wanadeal na how electronics inaunganishwa na programming pamoja na knowledges za computer.Nawasilisha..mwenye swali lolote aulize nipo kwa kujibu.
Mkuu ahsante kwa thread hii, sasa kama hata wanaosoma huko wanazichanganya, fikiria sisi wazazi wa miaka hiyo mtoto kamaliza form4 anakuambia anataka asomee computer unampa ushauri gani huyo kijana. Yaani kipofu amuongoze kipofu. Nafikiri hapa ndipo wataalamu kama ninyi mnaweza kuelimisha umma. Halafu nchi hii inaonekana kila chuo kinajochiita chuo kina kozi ya computer hii nayo inaongoza confusion kwani kujua ubora wa vyuo hivi ni kitu kigumu.
 
Computer engineering kwa nchi za wenzetu wengi wanafanya kazi kwebye viwanda vya simu, computers, haswa upande wa hardware design.
Huku tz hatuna miundo mbinu inayo support hii course. Ndio maana watu wengi wa CE Wanaishia kufanya kazi na CS, IT.
Mkuu unaweza kutudadavulia tofauti ya CE, CS na IT tuelewekipi ni kipi hasa vijana wanakutaarifu kwamba wanataka kusoma "computer" bila hata kujua kunatofauti gani katika program hizo kuanzia level ya certificate, diploma hadi degree.
 
Mkuu unaweza kutudadavulia tofauti ya CE, CS na IT tuelewekipi ni kipi hasa vijana wanakutaarifu kwamba wanataka kusoma "computer" bila hata kujua kunatofauti gani katika program hizo kuanzia level ya certificate, diploma hadi degree.
Ili mtu aelewe vizuri inabidi uigawanye computer katika levels
Lets assume level zipo 4

1.Level ya hardware

2.Level ya chini ya software(level inayodeal na jinsi gani computer inaenda kufanya kazi katika level hii zaidi kuna algorithms za jinsi hardware inavyotakiwa kufanya kazi)
Mfano kama unatumia android smartphone...android OS ina operate katika level ya chini ya software

3.Level ya kati ya software(level ambayo software inapitia kuhakikiwa kabla ya kwenda kweny level ya juu)
Mfano Kwa android DVM ndio hutumika

4.Level ya juu ya software (level ambayo mtumiaji wa mwisho anaiona mfano application ya jamiiforum ni level ya juu)

Computer engineer ana deal na designing na maintenance katika level ya hardware
computer engineer anasoma module za engineering nyengine kama electronics na electrical engineering ili kufanikisha kazi yake kwa upande wa software anadokoa kidoko software engineering ambalo ni tawi la computer science

Computer scientist anadeal na theoretical part ya jinsi gani software itafanya kazi katika level zote hizo japo anaweza specialize katika level moja
Mfano computer scientist wa level ya chini ya software atadeal na machine learning na vitu kama AI
Wa level ya juu atadeal na vitu kama application software programming, database,computer networks,computer system,computer security

IT anadeal na utumiaji wa level ya juu ya software katika matumizi mbalimbali mfano biashara

Lakini kwa vyuo vingi mtu wa Computer engieering anasoma pia module za IT

Computer science anasoma pia module za IT na chuo kama MIT anasoma pia electrical engineering
 
Back
Top Bottom