Elimu duni na wasomi duni

fellali

Member
Aug 14, 2013
17
2
Elimu duni na wasomi duni
Elimu duni na wasomi duni

Elimu ndicho chomba pekee cha kumkomboa mwanadamu kifikra, kimtazamo na katika hali yote ya maisha kwa ujumla. Aidha, ni elimu hiyo hiyo inayompa mwanadamu uwezo wa kutambua mema na mabaya ikiwa ni pamoja na kukemea iwapo mwanajamii yeyote atatenda visisvyo ndani ya jamii husika.

Katika nchi zilizo endelea kwama vile marekani, china, uingereza n.k. wasomi ndiyo wamechangia kwa kiasi kukubwa kuleta mapinduzi ya kimaendeleo katika nchi zao. Wametumia elimu zao kuzikomboa nchi zao kutoka kwenye dimbwi la utegemezi.

Ni elimu hiyo hiyo imeufanya ulimwengu tuliomo sasa, ugeuke na kuwa kama kijiji kutokana na utandawazi. Suala la mawasiliano limeboreshwa zaidi tofauti hapo awali.

Turudi kwenye nchi yetu ni sahihi kabisa kuwa tunaowasomi wa kutosha wenye elimu ya juu na kati, isitoshe baadhi ya wasomi hawa wamepewa nafasi za juu katika serikali ya nchi yetu. Ni matumaini ya watanzania wengi kuwa wasomi hawa wanaweza kuikoa nchi kutoka katika bwawa la umaskini linaloikabili, kinyume chake watanzania wamekuwa wakishuhudia manyanga ya kila aina yanyofanywa na wasomi husika.

Tujikumbushie sakata la EPA walikuwa ni wasomi wazuri tu waliowaibia watanzania! vipi kuhusu mikataba feki ya Richmond, Dowans, Agreco n.k.; ni wasomi hawa hawa wameiingiza nchi kwenye mikataba feki ya ununzi wa Rada ambayo hadi sasa inahitaji matengenezo baada ya kuharibika, madini na sekta nyinginezo ambazo wasomi hawa wametumia kuliteketezea taifa.

Nchi imezidi kuwa maskini, kila kukicha msoto unaongezeka, watanzania wengi wanateseka wakati wachache wananufaika kwa kutumia matunda ya nchi nzima. Hivi kweli wasomi hawa wamepata elimu bora ya kulikomboa taifa au wamepata elimu duni yenye kulenga maslahi binafsi? Hivi hawa ni wasomi au wasomaji walioenda shule kutafyta vyeti ili vitumike kwa ajili ya maslahi binafsi?

Tujuavyo, elimu ndicho chombo pekee cha kumkomboa mwanadamu kifikra na kimtazamo; sasa hawa wasomi wetu elimu imewakomboa? ni msomaji gani anayeweza kupanga mbinu za kujiibia mwenyewe?

Lakini haya yote yanasababishwa na na tatizo la mfumo wa ajira wa nchi yetu wa kuangalia vyeti kuliko utendaji kazi wa mtu binafsi. Tumesahau kwamba nchi zote zilizo endelea haziangalii suala la vyeti bali ni utendaji kazi wa mtu binafsi.

Kipindi kichache kilichopita, kumeripotiwa kundi la wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na kufaulu lakini hawajui kusoma wala kuandika! sasa tujiulize ‘wameshindaje mitihani yao ya darasa la nne, saba na kidato cha nne? ni nani aliyewafanyia mitihani yao kama hawajui kusoma wala kuandika? kisha tujenge taswira mtu huyu baadae apewe madara kwenye serikali yetu, ni manyanga gani yatatokea kwenye ofisi atakayokabidhiwa? mtu kama huyu atalikomboa taifa au atalingamiza? bila shaka atatanguliza maslahi binafsi kuliko ya taifa, mikataba feki itakuwa mingi zaidi kwa kadri watakavyoongezeka.

Umefika wakati wa kubadilisha mfumo duni wa elimu ya nchi yetu. Tutengeneze mfumo utakaolenga kuiboresha sekta ya elimu na siyo kuididimiza. Mfano tumeshuhudia mabadiliko mengi ya mara kwa mara ya mitaara kwenye sekta hii ya elimu lakini ukweli ni kwamba hayakuwa maboresho ila madidimizo ya sekta ya elimu.

Hatahivyo, mfumo unaotumika kuwapata na kuwaandaa walimu haulengi kuiboresha sekta ya elimu ila tu unalenga kuwawezesha watu kupata sehemu ya kugangia njaa. Siku zote mfumo duni wa elimu hulenga kuzalisha wasomi wenye mawazo na fikra na mitazamo duni yasiyolenga kuiokoa nchi bali kuibomoa. Kama kuna watanzania ambao bado wanafikri kwamba tunaouwezo wa kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye dimbwi la wasomi duni, tuungane pamoja ili kuweza kuonyesha njia sahihi za kutumika katika kuiboresha sekta yetu ya elimu.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Na Felix Lugeiyamu.

 
Umenena mkuu. Hawa wenye elimu duni tena ya kuungaunga ndo wenye madaraka makubwa kwa wale wenye elimu bora kisa 'unamjua nani na si unajua nini'. Hatufiki na hatutafika. Mifano mizuri na hai ni sekta ya elimu. Wenye cheti ndo mabosi wa wenye masters na degree za kwanza! Na mnategemea wasomi hawa kuwashauri. Tukitaka kufika kwenye neema, ondoeni siasa kwenye mambo ya kitaalam na wasomi wapewe mamlamka na nafasi zinazolingana na elimu yao.
 

so you need proof. Tembelea ofisi za elimu na mashuleni uwaone hao wenye akili ndogo wanavyowaongoza wenye akili kubwa kisha uje hapa useme tena 'hear say'! Tunaopost mambo haya hatubuni tumefanyia tafiti ndo maana tunamalizia kwa kushauri nini cha kufanya. Ndo maana umekuja na jibu la mkato sio? Au ndo walewale watoto wa mjomba kupeana ofisi! Badilikeni bwana vinginevyo usanii hautakwisha nchi hii.
 
so you need proof. Tembelea ofisi za elimu na mashuleni uwaone hao wenye akili ndogo wanavyowaongoza wenye akili kubwa kisha uje hapa useme tena 'hear say'! Tunaopost mambo haya hatubuni tumefanyia tafiti ndo maana tunamalizia kwa kushauri nini cha kufanya. Ndo maana umekuja na jibu la mkato sio? Au ndo walewale watoto wa mjomba kupeana ofisi! Badilikeni bwana vinginevyo usanii hautakwisha nchi hii.
Hili mbona halina ubishi?...hata historia mbona inaonyesha hivyo?20 years ago...wataalamu wote willayani bosi wao mkubwa na wa kuogopwa kabisa alikuwa mweneykit wa chama wa wilaya....na alikuwa ana nguvu kweli kweli za kimaamuzi..hata kwenye mambo ambayo hata uwezo wake ulikuwa haumruhusu.Na kumbuka hawa wenyeviti walikuwa std 7 tu..
 
Back
Top Bottom